MAKOSA YA MAHUJAJI Muandishi: TAWAKKAL JUMA HUSAYN. Imetafsiriwa na: Sheikh: YASINI TWAHA HASSANI. Imehakikiwa na: Sheikh:ABUBAKARI SHABANI RUKONKWA
بسم الله الرحمن الرحيم
2
YAJUE MAKOSA MBALIMBALI
YAFANYIKAYO KATIKA IBADA YA
HIJA
Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu, na Rehma
na Amani zimuendee kipenzi chetu Mtume
Muhammadna wakeze na sahaba zake na
watakaowafuata kwa wema hadi siku ya mwisho,
wabaad.
Ndugu yangu katika Uislamu unaekusudia kufanya ibada
ya Hija mwaka huu;
Awali ya yote yakupasa umshukuru Allah kwa kukupa
Tawfiyq ya kuiendea nyumba yake tukufu na kongwe
iliyoko Makkah ili kuitimiza nguzo hii ya tano ya
Uislamu, Hongera, lakini angalia kuwa ibada ya Hija
siku hizi imetawaliwa sana na makosa ya kinamna ya
kuyafanya matendo mbalimbali ya ibada hii. Mtume
(Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) kawaamuru
watu wachukuwe matendo na ibada ya Hija kutoka
kwake.
Katika makala hii nakutahadharisha juu ya makosa
mbalimbali ya Hija ambayo hupunguza thawabu na tija
ya ibada hii tukufu.
IHRAMU NA MAKOSA
3
YAKE Imethibiti katika Sahihul Bukhari na Muslimu kuwa Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) amewapangia waislamu wa sehemu na pembe mbalimbali za dunia sehemu zao za kuhirimia wanapotaka kufanya ibada ya Hija au Umra. Sehemu hizo ni kama zifuatazo: 1. Dhul Hulayfah kwa watu wa Madinah. 2. Juh’fa kwa watu watokao Sham. 3. Qarnul Manaazil kwa watu wa Najdi. 4. Yalamlam kwa watu watokao Yemen. 5.Dhatu irqi kwa watu watokao Iraqi. Kisha akasema: “Sehemu hizo ni kwa ajili ya wakazi wa sehemu hizo na kwa ajili pia ya wapitao sehemu hizo wasiokuwa wakazi wa sehemu hizo miongoni mwa wanaotaka kufanya ibada ya Hija au ‘Umra”. Kwa maana kuwa wewe mfano unatoka Afrika Mashariki sehemu yako ya kuhirimia niYalamlam kama unaelekea Makkah moja kwa moja, lakini ikiwa mathalani unakwenda Madina kwanza kwa ajili ya kuzuru Msikiti wa Mtume Muhammad (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) kama ilivyo kwa misafara yetu mingi ya Hija ndiyo baadaye uje uende Makkah kwa ajili ya Hija hapo sehemu yako ya kuhirimia itakuwa ni ile ya watu wa Madina yaani Dhul Hulayfah na si ile ya kwako ya kawaida uliopangiwa yaani Yalamlam. Kimsingi sehemu hizi ameziweka Mtume Muhammad (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) na ni mipaka ya kisharia haifai kuiruka pasina kuhirimia wala haifai
4
kuibadili kwa yeyote anayetaka kufanya ibada ya Hija au ‘Umra. Mwenye kwenda kuhiji anatakikana kuhirimia katika sehemu hizi ni mamoja awe anasafiri kwa njia ya nchi kavu, bahari au anga. Kwa bahati nzuri vyombo vya anga siku hizi huwatangazia Mahujaji kuwa sasa wamefika katika eneo la kuhirimia au Miyqaat. Na ni lazima Mahujaji wahirimie kabla ya kulipita eneo hilo. Ila ikiwa Mahujaji wanasafiri kwa ndege yawapasa wafanye haraka sana katika kuhirimia kwa kuwa ndege huchukua muda mfupi sana kulipita eneo la Miyqaat au la kuhirimia. Kosa hapa ni kuwa baadhi ya Mahujaji wanaokwenda moja kwa moja Makkah badala ya kuhirimia katika sehemu hizo wakiwa katika ndege au katika usafiri wowote walionao na si kusubiri hadi wateremke uwanja wa ndege wa Jiddah ndipo wahirimie. Haya ni makosa na ni kukhaalifu amri ya Mtume Muhammad (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake). Ni juu ya viongozi wa Hija kuweka wazi kama wanakwenda moja kwa moja Makkah au wanapitia kwanza Madina ili watu wajue wanatakiwa kuhirimia wapi. Kimsingi kosa hili linapotokea hadi anayekwenda kuhiji akawa ameshuka kiwanja cha ndege cha Jiddah ni juu ya Hujaji huyo kurudi hadi sehemu yake ya kuhirimia kama ataweza la sivyo Wanachuoni wengi wanaonelea kuwa analazimika atoe fidia ya kuchinja mnyama akifika Makkah na awagawie masikini wa Makkah wala hataruhusiwa yeye kumla mnyama huyo wala kuwapa matajiri kwa kuwa ni mnyama wa kafara ambaye anatakikana aliwe na masikini tu.
MAKOSA YA KIVITENDO
5
YANAYOAMBATANA NA KUTUFU AU KUZUNGUKA AL-KA’ABAH. Ilivyothibiti ni kuwa Mtume Muhammad (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) alianza kuzunguka Al-Ka’abah akianzia katika sehemu lilipo jiwe jeusi au Hajarul Aswad katika nguzo inayoitwa Ruknul Yamaani. Pia imethibiti kuwa aliitufu Al-Ka’abah nje ya eneo linaloitwa Hijr, na pia alikwenda mwendo wa haraka kidogo sawa na kukimbiakimbia pasina kunyanyua miguu sana. Mwendo huu unaitwa Raml na ilikuwa ni katika mara tatu tu za kwanza za kuizunguka Al-Ka’abah pale alipoingia Makkah na pia alikuwa wakati akitufu akiashiria, akiligusa jiwe jeusi na kulibusu na pia imethibiti kuwa aliashiria jiwe kwa Miijaninaye akiwa katika mnyama wake na akawa anaibusu Miijani au fimbo yake hiyo na akawa kila akipita pahala pa jiwe ana ashiria kwa mkono wake na pia imethibiti kuwa alikuwa akiigusa Ruknul Yamaani kwa mkono wake. Kimsingi unapokuwa umefika sehemu ya Hajarul Aswad au jiwe jeusi, na hii inaashiria kuwa paangaliwe wepesi, ikiwa mtu itamuwia wepesi hadi kulifikia jiwe jeusi pasina mikiki mikiki basi na alishike na kulibusu. Pia ifahamike kuwa kuliashiria au kulishika na kulibusu si kwa jingine zaidi ya kumwabudu Allah na kumtukuza wala si kwa kuitakidi kuwa jiwe hilo linadhuru au linaleta manufaa. Katika Sahihul Bukhari na Muslimu kutoka kwa: ‘Omar (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) kuwa yeye alikuwa akilibusu jiwe huku akisema; “Hakika mimi najua kuwa wewe hudhuru wala hunufaishi na lau kama si kumuona Mtume Muhammad (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) akikubusu nisingalikubusu”.
6
Kuna makosa ambayo baadhi ya Mahujaji hufanya yakiambatana na sehemu hii nayo ni; 1. Kuanza kuzunguka Al-Ka’abah kabla ya kufika sehemu ya jiwe jeusi, na kwa sasa kuna alama ya mustari maalumu inayoonyesha lilipo jiwe jeusi na kama ni usiku kuna taa ya rangi maalumu taa ya kijani yenye kuonyesha lilipo jiwe jeusi, Kuanza kuzunguka Al-Ka’abah kabla ya kufika lilipo jiwe jeusi aidha ni kutokujua au ni Mubalaa (kuzidisha) katika dini na ni kama kutanguliza kufunga Swawm ya Ramadhaan kwa kuanza kufunga siku mbili kabla. Baadhi ya Mahujaji hudai kuwa wao wanafanya hivi ili wasije wakakosea. Madai haya hayakubaliki kisharia kwani tunatakiwa tumfuate Mtume Muhammad (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) haki ya kumfuata wala haifai kutanguliza kauli au kitendo mbele ya Allah na Mtume Wake. 2. Kutufu ndani ya eneo linaloitwa Hijr kutokana na msongamano mkubwa wa watu. Kimsingi hili ni kosa kubwa kwa kuwa eneo la Hijr kisharia liko ndani ya Al-Ka’abah na tawafu inatakiwa iwe nje ya Al-Ka’abah na sio ndani ya Al-Ka’abah, Kwa hiyo kwa kupita ndani ya Hijr unapotufu unakuwa umetufu katika sehemu ya Al-Ka’abah na si Al-Ka’abah yote ambayo ndiyo inayotakiwa. 3. Kukimbia kimbia katika Tawafu zote saba. 4. Kusongamana na kupigana vikumbo kwa ajili ya kulifikia jiwe jeusi ili kulibusu, jambo ambalo mara nyingine husababisha watu kurushiana matusi na hata
7
kupigana na kwa kufanya hivyo wakawa wanaivunjia heshima nyumba tukufu ya Allah. Kutufu kwa namna hii kunapunguza daraja ya kutufu bali mara nyingine hata kuipunguza ibada nzima ya Hija. Amesema Allah: “Hija ni miezi maalumu na anayekusudia kufanya Hija katika miezi hiyo basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika hiyo Hija” (2:197). Misongamano kama hii haina ulazima bali inaondoa makusudio makubwa ya kutufu kwa kuondoa unyenyekevu na kumtaja Allah, ambayo ni miongoni mwa makusudio matukufu kabisa ya kutufu. 5. Itikadi ya baadhi ya Mahujaji kuwa jiwe jeusi linanufaisha au linadhuru kwa dhati yake hivyo utawakuta pindi wanapoliamkia wanajipangusa katika viwiliwili vyao au wanawapangusa watoto wao walionao katika ibada ya Hija au ‘Umra. Na yote haya ni kutokana na ujinga na ni upotevu wa wazi, Manufaa na Madhara yanatoka kwa Allah peke Yake, na imekwishatangulia kauli ya ‘Omar (Radhi za Allah ziwe juu yake) juu ya jiwe jeusi kuwa yeye alisema wakati akilibusu: “Hakika mimi najua kuwa wewe hudhuru wala hunufaishi na lau kama si kumuona Mtume Muhammad (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) akikubusu nisingalikubusu”. 6. Baadhi ya Mahujaji kung’ang’ania nguzo zote za Al-Ka’abah na mara nyingine wakawa wanazishika kuta zote za Al-Ka’abah na hata mara nyingine kuing’ang’ania sana Al-Ka’abah kwa kila sehemu au wakawa kila wakiigusa Al-Ka’abah wakawa wanajipangusia. Na huu ni ujinga na upotevu wa wazi,
8
Maamkizi ya jiwe jeusi ambalo liko katika Ruknul Yamaani upande wa Mashariki wa Ka’bah tukufu, au kuiamkia Ruknul Yamaani ya upande wa Magharibi ni ibada na Utukuzo kwa AllahMtukufu,hivyo inatupasa tufanye kama vile alivyokuwa akifanya Mtume wetu Muhammad (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake). Katika kitabu cha Musnad cha Imaam Ahmad kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Allah Amuwie Radhi yeye na Mzazi wake) kuwa yeye alizunguka Al-Ka’abah akiwa na Mu’aawiya Allah amuwie Radhi akawa Mu’aawiya akiziamkia nguzo zote, Ibn ‘Abbaas akamuuliza Mu’aawiya kwa kusema; kwa nini unaziamkia nguzo zote wakati Mtume Muhammad (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) alikuwa hafanyi hivyo? Mu’aawiya akasema hakuna cha kuachwa katika nyumba hii tukufu; Ibn ‘Abbaas akamwambia kwa hakika tuna sisi kutoka kwa Mtume wa Allah (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) kiigizo chema, Mu’aawiya akamwambia hakika umenena kweli.
MAKOSA YA KIMATAMSHI YANAYOAMBATANA NA KUTUFU AU KUZUNGUKA AL-KA‘ABAH
9
Imethibiti kutoka kwa Mtume Muhammad (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) kuwa yeye alikuwa akileta Takbira au akisema Allahu Akbar kila alipolifikia jiwe jeusi; na alikuwa akisema anapokuwa kati ya Ruknul Yamaani na jiwe jeusi;“Rabbanaa Aatinaa fiy Dun’ya hasanatan wafiyl Aakhirati hasanah” (2:201). Na akasema pia; “Hakika si vingine kumefanywa kutufu Al-Ka’abah, na kuzunguka Swafa na Mar’wa na kutupa mawe Jamaraat kuwa ni kwa ajili ya kusimamisha utajo wa Allah”. Miongoni mwa makosa yanayofanywa na baadhi ya watu wanapotufu Al-Ka’abah ni kuwa na dua maalumu kwa kila mzunguko, pasina kuomba dua nyingine, mpaka mara nyingine hufikia anapomaliza mzunguko kabla ya kumaliza dua huiacha dua hiyo hata kama limebaki neno moja tu katika dua hiyo basi hatolileta maadamu amemaliza mzunguko huo; hivyo atalikata neno hilo moja ili alete dua nyingine kwa ajili ya mzunguko mwingine. Na ikiwa atakuwa amekamilisha dua kabla ya kukamilisha mzunguko atanyamaza. Haikuthibiti kutoka kwa Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) kuwa yeye aliweka dua maalumu kwa ajili ya kila mzunguko wa Al-Ka’abah. Amesema Shaykhul Islaam Ibn Taymiyah (Allah Amrehemu): “Hakuna katika kutufu dhikri (utajo) au dua maalumu kutoka kwa Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake); si kwa amri yake wala kauli yake wala mafunzo yake, bali anachotakiwa mtu ni kuomba dua mbalimbali na kile kitajwacho na watu wengi kuwa kuna dua maalumu hilo za kuzungukia Al-Ka’abah halikuthibiti kutoka kwa
11
Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake).” Kwa hiyo basi atakiwalo mtu anayezunguka Al-Ka’abah ni kuomba kheri aitakayo miongoni mwa kheri za Dunia na Akhera, na amtaje Allah kwa dua yoyote ile iliyothibiti kisharia iwe ni Tasbihi au Tahmidi au Tahlili au Takbira au kusoma Qur-aan. Na miongoni mwa makosa ambayo yanafanwa na Mahujaji wakati wa kutufu ni kuwa na vijitabu vya dua ili waombe kwa dua hizo japo hawajui maana yake. Na mara nyingine huwa kuna makosa ya uchapishaji au ya kunakili ambayo hubadili maana nzima ya dua hiyo na kuwa mtu badala ya kuomba manufaa akawa anaomba madhara pasina yeye kujua. Lau angeomba mwenye kutufu anachokitaka na anachokijua na akakusudia maana yake ni bora zaidi na hili lina manufaa zaidi na ndiko hasa kumuiga Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) na kumfuata. Na miongoni mwa makosa yanayotokea wakati wa kutufu ni watu au kikundi cha watu kuwa chini ya mtu mmoja mwenye kuwaimbisha dua mbalimbali kwa sauti ya juu na wengine wakawa wanaitikia hivyo zikawa sauti ziko juu na ikawa ni vurugu mtindo mmoja, jambo ambalo hutokea kuwapa tashwishi Mahujaji wengine na wakawa wanashindwa waseme nini, Na hili huondoa unyenyekevu na kuleta maudhi kwa waja wa Allah katika pahala hapa patukufu, Ilishawahi kutokea kuwa Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) aliwatokea watu fulani waliokuwa wakiswali na huku kila mmoja akisoma kwa sauti, akasema Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake): “Kila mmoja wenu
11
anamnong’oneza Mola wake, basi msidhihirishiane sauti” (Imepokewa na Imaam Maalik katika kitabu chake cha Muwatwwaa). Ni uzuri ulioje lau huyu muongozaje wa watu Hija angeliwatangulia watu wake na akawaambia fanyeni hivi au vile, ombeni kimya kimya kadri mtakavyo na akawa akitembea nao ili asipotee mmoja wao na kwa kufanya hivyo wakatufu kwa unyenyekevu na utulivu huku wakimuomba Mola wao kwa kuogopa na kutumai wanachokipenda na wanachokijua maana yake na hivyo watu wengine wakawa wamesalimika na maudhi yao.
MAKOSA YANAYOFANYIKA KATIKA RAKAA MBILI BAADA YA KUTUFU Imethibiti kuwa Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) kuwa alipomaliza kutufu alielekea Maqaamu Ibraahim kisha akasoma sehemu ya Aayah ya 125 ya Suratul Baqarah. “Wattakhidhuu min maqaami Ibraahima muswallaa”. Kisha akaswali Rakaa mbili nyuma ya Maqaamu Ibraahim. Akasoma katika Rakaa ya kwanza Alhamdu (Suratul Faatihah) na Qul yaa ayyuhal kaafiruna (Suratul kaafiruna), na katika Rakaa ya pili akasoma Alhamdu (Suratul Faatihah) na Qul HuwAllahu ahad (Suratul Ikhlaas). Na miongoni mwa makosa ambayo baadhi ya watu huyafanya ni ile dhana yao kuwa ni lazima kuswali Rakaa hizo mbili karibu na sehemu ya Maqaamu, jambo ambalo huwapelekea kusababisha misongamano, kulundikana, kuudhiana na hata watu wengine wanaozunguka Al-Ka’abah kukosa njia ya kupitia. Kimsingi Rakaa hizi mbili baada ya mtu kumaliza kutufu
12
zinaweza kuswaliwa sehemu yoyote katika Msikiti wote wa Makkah na pia mwenye kuswali anaweza akaswali nyuma ya Maqaamu hata kwa mbali na hili litamwepusha na maudhi; hatoudhi wala kuudhiwa na ataweza kuswali kwa unyenyekevu zaidi na utulivu. Na miongoni mwa makosa vile vile ni kule baadhi ya wanaoswali nyuma ya Maqaamu Ibraahim baada ya kumaliza kutufu kuswali zaidi ya Rakaa mbili pasina sababu yoyote hali wanajua kuwa kuna ndugu zao wamemaliza kuzunguka Al-Ka’abah nao wanataka kuja kuswali hapo. Na miongoni mwa makosa vile vile ni kule baadhi ya wenye kutufu wanapomaliza kutufu kiongozi wao huwasimamisha akawa akiwaombea kwa sauti ya juu, wakawa kwa kufanya hivyo wakiwasumbua Mahujaji wengine wanaoswali nyuma ya Maqaamu Ibraahim na kuwakera. Allah Amesema; “Muombeni Mola wenu kwa unyen-yekevu na kwa siri, Hakika Yeye Hawapendi warukao mipaka” (7:55).
KUSA‘I KATI YA SWAFFAA NA MAR-WA NA MAKOSA YAKE
13
Imethibiti kutoka kwa Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) kuwa alipokuwa akikaribia Swaffaa alikuwa akisoma: “Inna Sswafaa wal Mar-wata min sha‘aairi LLaahi” (2:158). Kisha akapanda kilima cha Swaffaa hadi akawa anaiona Al-Ka’abah hapo huielekea na kunyanyua mikono yake akimhimidi Allah na akiomba atakacho, akimpwekesha, akimtukuza na akisema: “Laa ilaaha illa Llahu wahdahu laa shariyka lahu, lahul-Mulku walahul-Hamdu wa Huwa ‘alaa kulli shay’in Qadiyru, laa ilaaha illa Llahu Anjaza wa‘adahuu, wa Naswara ‘Abdahu, wa Hazamal ahzaaba wahdahuu”. Akiyasema maneno haya mara tatu, Kisha akashuka kutoka katika kilima cha Swaffaa, Kisha akatembea hadi alipofika sehemu ambayo kwa sasa kuna alama mbili za kijani alikimbia katikati ya alama moja hadi nyingine, Alipofika katika alama ya pili alianza tena kutembea kama kawaida, Na akitoka Mar-wa kuelekea Swaffaa alifanya mithili ya vile alivyofanya alipokuwa akielekea Mar-wa kutoka Swaffaa. Na miongoni mwa makosa yafanywayo na baadhi ya wenye kusa‘i ni pale wanapopanda Swaffaa au Mar-wa na kuelekea Al-Ka’abah na wakaleta Takbira tatu na wakaashiria Al-Ka’abah kwa vidole vyao kama wafanyavyo wakati wa kuswali kisha baada ya hapo wao hushuka kutoka kwenye Swaffaa au Mar-wa. Na hii ni kinyume na mafundisho ya Mtume wetu Muhammad (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake). Na miongoni mwa makosa ya Kusa‘i pia ni kule watu kukimbia sehemu zote za Swaffaa na Mar-wa. Na hili ni kinyume na mwenendo wa Mtume (Rehma na Amani za
14
Allah ziwe juu yake) kwani yeye alikuwa akikimbia katikati ya alama mbili za kijani tu na sehemu nyingine akawa anatembea tu. Huenda hili linasababishwa ima na ujinga na kutofahamu au mtu kutaka amalize Kusa‘iharaka.
MAKOSA YA KUSIMAMA KATIKA VIWANJA VYA ‘ARAFA Imethibiti kuwa Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) alikaa siku ya ‘Arafah katika viwanja vya ‘Arafah katika sehemu inayoitwa Namirah, Alikaa hapo hadi wakati wa Adhuhuri, Kisha akapanda mnyama wake hadi alipoteremka na kuswali Adhuhuri na Al‘Asri kwa Rakaa mbili mbili kila moja kwa Adhana moja na Iqaama mbili, Kisha akapanda mnyama wake kwa mara nyingine akaenda naye hadi sehemu alipotaka kusimama na hapo akasema: “Nimesimama hapa lakini ‘Arafah yote ni pahali pa kusimama”. Hapo Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) akawa akinyanyua mikono yake akiwa ameelekea Qiblah na kuomba, hadi Magharibi ikaingia na hapo akaanza kuelekea Muzdalifah. Na miongoni mwa makosa watu wanayofanya katika viwanja vya ‘Arafah ni; 1. Kufika mapema katika sehemu viliko viwanja vya ‘Arafah lakini wakawa nje ya Viwanja vya ‘Arafah hadi jua likazama. Kisha wakaondoka kwenda Muzdalifah hali ya kuwa hawajasimama katika Viwanja vya ‘Arafah, Na hili ni kosa kubwa ambalo
15
linapotokea mtu anakuwa ameikosa Hija kwani kusimama katika viwanja vya ‘Arafah ndiyo nguzo kubwa ya Hija ambayo Hija ya mtu haiswihi hadi mtu awe amesimama katika viwanja vya ‘Arafah. Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) amesema kuwa: “Hija ni ‘Arafah, atakayekuja usiku wa baada ya Mahujaji kusimama ‘Arafah lakini kabla ya kuchomoza Alfajiri ya tarehe 10 atakuwa ameidiriki ‘Arafah na Hija yake itakuwa sahihi”. Na sababu inayosababisha kosa la baadhi ya Mahujaji kutoidiriki ‘Arafa nao wakiwa karibu kabisa na viwanja hivyo ni kule wao kudanganyana wao kwa wao wakadhani kuwa wameshafika katika viwanja vya ‘Arafah kumbe kisharia wako nje ya viwanja hivyo vya ‘Arafah, Kimsingi Mahujaji hawana udhuru wa kuikosa ‘Arafah katika mazingira haya kwani kwa sasa kuna Mabango makubwa sana yenye kuonyesha Mipaka ya ‘Arafah kwa Kiarabu, Kingereza na lugha zingine. Yanaonyesha wazi wapi ni ndani ya ‘Arafah na wapi ni nje ya ‘Arafah, Pia kuna watu ambao huwaambia Mahujaji kuwa hapo walipo ni nje ya viwanja vya ‘Arafah kama wako nje ya ‘Arafah kimakosa. 2. Kuondoka kwao katika viwanja vya ‘Arafah kabla ya kuzama jua, Na hili ni kosa kubwa tena ni haramu kwa kuwa kufanya hivyo ni kukhalifu amri ya Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) kwani yeye Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) alikaa katika viwanja vya ‘Arafah hadi jua likazama na giza likaanza kuingia ndipo akaondoka kuelekea Muzdalifah, Ama kuondoka kabla ya jua kuzama hii ni katika vitendo vya kijahiliya
16
alivyokataza Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake). 3. Baadhi ya Mahujaji kuelekea Jabal ‘Arafah wakati wa kuomba dua hata kama kwa wao kufanya hivyo wanakipa Qiblah mgongo au kinakuwa upande wa kulia au wa kushoto. Na hili ni kinyume na mwenendo wa Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake), kwani Sunnah wakati wa kuomba dua hapo ni kuelekea Qiblah na si Jabal ‘Arafah au kilima cha ‘Arafah.
KUTUPA MAWE NA MAKOSA YAKE Imethibiti kutoka kwa Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) kuwa yeye alipiga Jamratul ‘Aqabah ambayo ni ya mwisho na inaelekea Makkah, Alipiga mawe na akachinja katika siku ya kuchinja, Akawa analeta Takbira au akisema Allaahu Akbar kwa kila kijiwe alichopiga, Vijiwe vyenyewe vinatakikana viwe saizi ya punje za karanga, kinyume cha hivyo kwa mfano kutupa mawe makubwa ni kuchupa mipaka katika dini, jambo ambalo hupelekea watu kuumizana na ni jambo ambalo liliwaangamiza waliokuwa kabla yetu kama alivyosema Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake). Wengine hufikia hadi kuipiga minara ile kwa kanda mbili na mawe makubwa!!!. Huku ni kuchupa mipaka ya Kisharia.
17
Miongoni mwa makosa yanayofanywa na Mahujaji katika kupiga mawe ni; 1. Baadhi ya watu kuitakidi kuwa ni lazima wachukue vijiwe kutoka Muzdalifah tu. Kwa itikadi yao hiyo wakawa wanajikalifisha na kuzichosha nafsi zao kwa kufanya hivyo. Hufikia hata inapotokea mmoja wao akawa amedondosha jiwe moja kwa bahati mbaya huwa ni mwenye kuhuzunika sana na akawa anawaomba alionao wampe mawe ya ziada waliyonayo kutoka Muzdalifah, Na hili ni jambo ambalo halina mashiko kwani Mtu anaweza kuyachukua mawe hayo kutoka sehemu yeyote ile, bali mtu anaweza kwenda nayo hata kutoka nyumbani kwao alikotoka. 2. Itikadi yao kuwa wanapopiga minara ile ya Jamarati wanakuwa wanampiga Shetani, Hivyo mara nyingine utawasikia wakisema kuwa tumempiga Shetani mkubwa au mdogo au tumempiga baba wa Mashetani wakimaanisha ule mnara mkubwa yaani Jamaratul ‘Aqabah na mfano wa hivi. Na mingi ya mifano ambayo haifai katika sehemu hii tukufu. Mara nyingine utawaona wakitupa mawe kwa nguvu sana, kwa vurugu, kelele na mara nyingine hata wakawa wanatukana wanapoipiga minara hiyo na kudhani kuwa wanamtukana Shetani, Mara nyingine hufikia hata wakawa wanavua viatu au wakawa wanaivurumishia minara ile mawe makubwa kabisa tena kwa hasira na kwa kufanya hivyo wakaweza hata mara nyingine kuwaumiza watu wengine. Hiki ni kituko na kichekesho, na kwa hakika chanzo cha mambo haya ya kuchekesha na kuhuzunisha ni watu
18
kuwa na ‘Aqiydah mbovu za kibid’ah na kutokuelewa ibada hizi zinatakiwa zifanywaje. 3. Kutupa mawe makubwa, viatu na hata miti. Hili ni kosa kubwa na linalokhalifu mafundisho ya Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) ya kauli na vitendo, Kama tulivyokwisha kusema sababu ya mambo haya ni khulluu au kuchupa mipaka katika dini na kuitakidi kuwa wanampiga Shetani hasa badala ya kufanya kama vile Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) alivyoamrisha. 4. Kuziendea sehemu za kupiga mawe kwa vurugu na papara bila hata kuwahurumia waja wengine wa Allah, jambo ambalo husababisha maudhi kwa Waislamu wengine na hata mara nyingine kutukana na kupigana au hata vifo! Hali hii hugeuza sehemu hizi tukufu na kuwa kama sehemu za vurugu, kutukanana na mapambano. 5. Kuacha kwao kuomba baada ya kutupa mawe mnara wa kwanza na wa pili katika yale masiku yanayoitwa: Ayyaamu Ttashriyq au masiku matatu ya kuanika nyama. Ilivyothibiti ni kuwa Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) alikuwa pindi akimaliza kupiga mawe minara miwili ya kwanza alikuwa akisimama baada ya kupiga kila mnara mmoja kati ya hii miwili ya mwanzo akielekea Qiblah na kunyanyua mikono yake na kuomba dua ndefu, Na miongoni mwa sababu za kuacha watu kufanya hivi ni ujinga au kupupia kwao kutaka kumaliza haraka kupiga mawe kutokana na msongamano wa kutisha.
19
6. Kutupa mawe yote kwa mkupuo mmoja, Na hili ni kosa kubwa sana, Wanachuoni wanasema kuwa ikiwa mtu atatupa mawe yote kwa mkupuo mmoja basi hiyo itahesabiwa kuwa ametupa jiwe moja. 7. Kuzidisha kwao dua wakati wa kutupa mawe, yaani dua ambazo hazikuthibiti wakati wa Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) kama kusema kwao; “Ee Mwenyezi Mungu yajaalie mawe hayo kuwa ni radhi kwako na ni ghadhabu kwa Shetani”. Mara nyingine wao huacha Takbira iliyothibiti kutoka kwa Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake). Na haya ni makosa kisharia. 8. Watu wengine hutaka kutupiwa mawe hata kama hawana udhuru wa kisharia, Hii inaweza kuwa ni kwa sababu ya kukwepa zahma na misongamano, Na hili linakuwa ni kinyume na mafundisho ya Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) na alivyoagiza, Linalotakiwa ni kuwa kila mwenye uwezo na afya njema akatupe mawe mwenyewe pasina kuwakilisha Mtu, Watu wafahamu kuwa Hija ni moja kati ya aina za Jihadi ambayo ni lazima mwenye kuhiji akabiliane na tabu mbalimbali na lazima aikamilishe ibada hii kama alivyoamrisha Allah na Mtume Wake.
21
MAKOSA YA TWAWAFU YA KUIAGA AL-KA’ABAH (TWAWAAFUL- WADA‘I) Imethibiti katika Sahihul Bukhari na katika Sahihu Muslimu kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Allah Amuwie Radhi) kuwa yeye amesema: “Watu waliamrishwa kuwa liwe jambo lao la mwisho wanapotaka kuondoka na kurudi makwao iwe ni kutufu nyumba ya Allah isipokuwa wanawake walio katika siku zao wamekhafifishiwa au kusamehewa hilo”. Kuhafifishiwa wanawake walioko katika siku zao hapa inamaanisha kuwa wao wanaruhusiwa wakiwa katika hali hiyo ya hedhi kuondoka kurudi makwao ikiwa hakutakuwa na muda wa kutosha kwao kusubiri hadi watwaharike ndipo watufu na kuondoka. Na miongoni mwa makosa wanayofanya Mahujaji yanayohusiana na ibada hii ya Twawaaful Wada‘i ni: 1. Kuondoka Minaa wakaenda Makkah na wakafanya Twawaaful Wada‘i kisha wakarudi tena Minaa kumalizia kutupa mawe ndipo baadaye waondoke, Na hili halifai kwa kuwa ni kinyume na alivyofanya Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake). Na hapa utaona inakuwa ni kama kutupa mawe ndiko kumekuwa jambo lake la mwisho kufanya kabla ya kuondoka na hii ni kinyume na alivyoagiza Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) kwani kaagiza kuwa jambo la mwisho kwa Mahujaji liwe ni kutufu Twawafu ya kuaga Al-Ka’abah. 2. Kukaa kwao kitambo Makkah baada ya kutufu Twawafu ya kuaga, jambo ambalo linawafanya
21
wazingatiwe kuwa jambo lao la mwisho walilofanya si kutufu, Na hili pia ni kinyume na amri ya Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) kwani Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) alikuwa akifanya Twawaful Wada‘i kisha anaondoka na hivi ndivyo walivyokuwa wakifanya Maswahaba zake, Isipokuwa wanachuoni wameruhusu mtu kubakia kidogo baada ya kuiaga nyumba tukufu kama kuna dharura kubwa kama ya kuingia wakati wa Swala au kuswalia jeneza au jambo lenye kuambatana na safari yake kama kununua kitu au kusubiri kidogo wenzake, Ama yule ambaye atakaa Makkah baada ya Twawaaful Wada‘i pasina dharura itabidi airudie Twawaafu baadaye. 3. Kutoka katika milango ya Al-Ka’abah hali ya kuwa wanapiga piga vichogo vyao wakidhani kuwa kwa kufanya hivyo wanaitukuza Al-Ka’abah kumbe wanazua katika dini na hivyo kumaliza ibada hii tukufu kwa kufanya bid’ah!!. 4. Kuielekea kwao Al-Ka’abah wakiwa mlangoni wamemaliza kutufu Twawafu ya kuaga na wakawa wanaomba dua zao kama wenye kuiaga Al-Ka’abah, Na jambo hili halikuthibiti kutoka kwa Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake). TNB: Nilazima watu wafanye Ibada kama alivyoagiza Allah na Mtume wake (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake). Ibada ni Tawqiyfiyah, yaani ni mambo ambayo Sharia inamlazimu mtu ayafanye kwa jinsi, namna,
22
viwango, na wakati kama ilivyofundishwa na Mtume (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) wala haifai kupunguza wala kuongeza jambo lolote. Muislamu unae tekeleza ibada tukufu ya hija uliza kama hujui, ni mwiko kufanya ibada kwa mazoea au kubahatisha. Tena kuna watu wazuri zaidi wa kuwauliza haya nao ni: wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu vya Makkah, Madina na Riyadh. Kwani wengi wao wanaifahamu vizuri ibada ya Hija kinadharia na kivitendo. Hijjan Mabruuran Wasa‘ayan Mashkuuran wadhamban maghfuuran.