
1
Kujitoa Muhanga Kunamuweka Mtu Mbali Na Allaah Mzungumzaji: Imaam Muhammad Swaalih bin bin ´Uthaymiyn Imefasiriwa na: Wanachuoni.com Imepitiwa na: Yunus Kanuni Ngenda
2
بسم الله الرحمن الرحيم
Utangulizi
Kuhusu matendo [ambayo mtu humuonyesha Allaah hasira
kwayo], ni pamoja na kuchana nguo, kupiga mashavu, kukokota
nywele na mfano wa hayo. Baadhi ya watu wanafanya hivi. Hata
hivyo lililo kubwa, chafu na baya zaidi ni kujiua. Kuna watu
wanaojiua wakati wanapopatwa na misiba wasiyoweza kukabiliana
nayo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametueleza
kuhusu mtu aliyejeruhiwa na hakuweza kuvumilia. Akafanya kitu
ambacho hakijuzu na Allaah Akamuwajibishia Moto.
Mwenye kujitoa muhanga ili kuepukana na msiba huu - hivi kweli
ataepukana nao? Jibu! Hapana. Hatouepuka. Anafikiria kuwa
atapata kupumua baada ya kujiua. Pamoja na kwamba sivyo. Akifa
ataadhibiwa Motoni kwa kile alichojiua nacho. Humo
atadumishwa milele.
Kwa ajili hiyo tunawakataza ndugu zetu wanaoenda Palestina ili
kujilipua kati ya mayahudi. Wanafikiri kwa kufanya hivo
wanajikurubisha kwa Allaah. Uhakika wa mambo ni kwamba hili
linawatia mbali na Allaah. Wanajiua wao wenyewe! Kujiua ni
miongoni mwa madhambi makubwa. Mtu ataadhibiwa Motoni kwa
kile alichojiua nacho. Pamoja na hivyo hatusemi kuwa hawa
wanaingia katika kundi la watu hawa kwa kuwa wanafanya hivo
kwa Ijtihaad. Wanafikiria kuwa kitendo hichi ni kizuri. Mtu
mwenye kufanya kitu kwa kuelewa makosa pengine akasamehewa.
Hata hivyo kitendo hichi ni haramu Kishari´ah na sio katika Jihaad
katika njia ya Allaah.
3
Kitendo hichi vilevile hakiingii akilini. Ni mayahudi wangapi
anawaua pale anapojilipua? Ikiwa ni wengi ni watu 50-100.
Matokeo yake mayahudi hufanya nini? Wataua mamia na wanazidi
kuwa wenye kuchupa mipaka kuliko unavowaona sasa kwa kuteka
mji.
Lakini watu wengi hawatazami matokeo. Hawafikirii mbali.
Talare: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com
Milipuko Inayofanywa Haijawapatia Waislamu Faida Yoyote
Zaidi Ya Madhara Juu Ya Madhara
Kuhusiana na yale yanayofanywa na baadhi ya watu kujitoa
muhanga kwa kujiweka mabomu na kuwaendea makafiri kisha
wanajilipua pindi wanapokuwa kati yao, huku inachukuliwa ni
kujiua - na tunaomba kinga kwa Allaah. Mwenye kuiua nafsi yake
atadumishwa Motoni milele kama ilivyokuja katika Hadiyth yake
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Huyu aliyeiua nafsi yake hakuleta faida yoyote kwa Waislamu
hata kwa wasiokuwa Waislamu. Kwa sababu akiua watu kumi,
ishirini, mia au mia mbili, Uislamu haufaidiki chochote kwa hilo.
Wala hilo haliwafanyi watu kuingia katika Uislamu. Tofauti na
kile kisa cha yule kijana, yeye alisababisha watu wote wakaingia
katika Uislamu. Hata hivyo haihitajiki kuua adui kumi, ishirini,
mia au mia mbili kwa ajili watu waingie katika Uislamu. Kinyume
chake huenda maudhi ya maadui ndiyo yakazidi kuwa mengi.
4
Jambo hili ambalo Waislamu hawa wanafanya linapelekea
makafiri kuzidisha maudhi yao dhidi ya Waislamu.
Mfano wa hili ni kama sasa jinsi mayahudi wanavofanya dhidi ya
wapalestina. Mpalestina mmoja anapojilipua na kuua [mayahudi]
sita mpaka saba, matokeo yake wanajilipiza kwa kuua wapalestina
sitini, sabini au zaidi. Kwa hali hiyo kunakuwa hakuna faida
yoyote kwa Waislamu wala hao waliojilipua. Ndio maana naona
yeyote atakayefanya kitendo kama hicho atakuwa amejiua bila ya
haki. Hili litasababisha yeye kuingia Motoni - na tunaomba kinga
kwa Allaah. Aliyefanya hivo sio shahidi.
Lakini ikiwa mtu atafanya kitendo hiki kwa ujinga na huku
akifikiria kuwa inajuzu, tunatumai kuwa hatopata madhambi. Hata
hivyo hatofikia daraja ya aliyekufa shahidi kwa sababu
hakufanya kama anayekufa shahidi anavyopaswa kufanya. Lakini
hatopama madhambi kwa kuwa amefanya hivo kwa kufahamu
makosa. Yule mwenye kujitahidi na akakosea, anapata thawabu
moja.