1
1
إياكم و الغلو
JIEPUSHENI NA KUCHUPA MIPAKA
MUANDISHI SHEKH: YASINI TWAHA
KIMEREJEWA NA SHEKH: ABUBAKARI SHABANI
2
2
Kwajina la Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma
mwenye kurehemu.
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu Mmoja, Rehma na
Amani za Allah zimuendee nabii Muhammad (s.a.w)
hakuna nabii baada yake, pamoja na ahli zake na
maswahaba zake na Waislamu woote watakao fuata
mwenendo wake hadi siku ya kiyama. Amma baad:
Hakika Uislamu ni Dini ya uadilifu na ya kati kwa kati
na kuacha kuchupa mipaka.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Na vivyo hivyo
tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani).
(Al-Baqara: 143).
Maana yake: Waadilifu walio bora.
Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Sema: Mola
wangu ameamrisha uadilifu). (Al-Aaraf: 29).
Na Uislamu ni Dini nyepesi yenye huruma na kuondoa
uzito.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Wala hakuweka
juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya
baba yenu Ibrahim. Yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni
Waislam tangu zamani). (Al-Hajj: 78).
Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Mwenyezi
Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya
iwezavyo). (Al-Baqara: 286).
3
3
Na akasema: (Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu
isipokuwa kwa kadiri ya alicho mpa. Mwenyezi Mungu
atajaalia baada ya dhiki faraji). (Attalaaq: 7).
Na Mtume (s.a.w) alikuwa ni mfano wa kimatendo
katika hii dini, kwa hakika yeye (s.a.w) alipo mtuma
Mudhi pamoja na Abaa Mussa kwenda Yemen
aliwahusia kwa kusema: (Fanyeni wepesi na msifanyi
uzito, wabashirieni watu yalio mazuri na wala
msiwakimbize, saidianeni na wala msitofautiane).
Kapokea hadithi hii imam Bukhari na Muslim.
Usio huu sio kwa wawili hawa tu, bali kwa kila alio
lazimishwa na sheria, inaonyesha jambo hilo kauli yake
Mtume (s.a.w): (Hakika Dini ni nyepesi, na hakuna
atakae fanya uzito isipokuwa itamshinda, fanyeni yalio
ya sawa sawa, fanyeni yalio ya karibu, wabashirieni watu
yalio ya kheri).
Kapokea hadithi hii imam Bukhari.
Hakika sheria ya Uislamu inapinga kuchupa mipaka
katika dini, kwa sababu jambo hilo huondoa Uislamu
katika usawa na uadilifu, kwa sababu hiyo kawakataza
Mwenyezi Mungu walio pewa kitabu kutochupa mipaka
katika dini yao, kwa sababu kuchupa mipaka hupelekea
katika ukafiri na upotevu na kumzulia Mwenyezi Mungu
kwa namna nyingi za uzushi.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Enyi Watu wa
Kitabu! Msipituke mipaka katika dini yenu, wala
msimseme Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa lilio
kweli). (An-Nisaa: 171).
Na akawakataza Mwenyezi Mungu wajawake waumini
4
4
kutochupa mipaka katika dini kwa kuharamisha yalio
mazuri, na akaeleza ya kwamba vitendo hivi nivya
wakeukao wasio pendwa na Mwenyezi Mungu.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Enyi mlio amini!
Msiharimishe vizuri alivyo kuhalalishieni Mwenyezi
Mungu, wala msikiuke mipaka. Hakika Mwenyezi
Mungu hawapendi wakiukao mipaka). (Al-Maaida: 87).
Mwenyezi Mungu atujaalie tuwe niwenye kufuata sheria
zaka bila kuchupa mipaka, tuwe watu wa kati kwa
kati,Rehma na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie
nabii Muhammad (s.a.w) pamoja na Ahli zake na
Maswahaba zake na Waislam woote hadi siku ya
Mwisho.