HUKUMU YA ANAEFUNGA HALI YA KUWA HASWALI.
SWAHILI.
IMEANDIWA NA:
DAUDI ABUBAKARI.
IMEPITIWA NA:
ABUBAKARI SHABANI
بسم الله الرحمن الرحيم
Utangulizi
Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe
vyote, na rehma na amani zimwendee Mtume wetu
Muhammad (s.a.w) na watu wake na Maswahaba wake wote.
Amma baad:
Fatawa ya Sheikh Uthaymiyn katika Hukmu ya Mfungaji
Saum ambaye Haswali.
Swali:-
Nini Hukmu ya Mtu anaefunga lakini Haswali?
Jibu:-
Mwenye kuacha swala huku anafunga sio Sahih Saumu yake
wala Haikubaliki,Kwa hakika mwenye Kuacha Swala ni Kafir
Murtad, kwa Kauli ya Allah inayosema
Anasema Allah "Wakitubu na Wakasimamisha Swala na
wakatoa Zaka basi hao ni ndugu zenu katika Dini" (Tawbah
Aya 11).
2
Na Kauli ya Mtume (s.a.w) aliposema"Ahadi iliyopo Kati yetu
na wao ni Swala na Yeyote atakaeacha Swala amekufuru"
Na akasema tena
"Kati ya Mtu na Shirk na Kufru ni kuacha Swala"
Na hii ni Kauli ya Jumla ya Maswhaba kwa yule asiyekuwa
pamoja nao.
Anasema Abdullah Ibn Shaqiyq (r.a) Naye alikuwa miongoni
mwa Tabi'in ambaye ni Maarufu;-"Walikuwa Maswhaba wa
Mtume (s.a.w) Hawakuona Kitu ambacho Mtu anaweza
kuacha akawa Kafir Kinyume na mwenye Kuacha Swala.
Na kwa hili anapofunga Mtu na hali ya kuwa Haswali
Swaumu yake ni yenye Kurudishwa haikubaliki wala Haina
manufaa mbele ya Allah siku ya Qiyamah,
Nasisi tunasema: Swala Kisha Saumu na Amma atakaefunga
akawa Haswali basi Saumu yake anarejeshewa
mwenyewe,Kwa hakika Kafir Haikubaliwi Ibada yake.
Pia Allah amewaandalia adhabu kali wenye kuswali ilihali
wanazisahau swala zao, amesema Allah mtukufu :
(Basi, ole wao wanao Sali Ambao wanapuuza Sala zao).
Katika hizi aya Allah ameeleza adhabu ambayo watafikia
wale ambao wanaswali ila swala zao wanazisahau na
kupuuzia mpaka muda wake unapita, sasa ikiwa hali yao
nikama hiyo wale wasio swali kabisa hawawezi kuwa waislam.
3
Tunamuomba Allah atudumishe katika swala na tuwe
niwenye kutekeleza swala katika wakati wake.