FADHILA ZA KULA DAKU
Kiswahili.
Imeandikwa na: Imaam Swaalih bin Fawzan Al-Fawzaan.
Imetafsiriwa na: Yasini Twaha Hassani
Imepitiwa na: Yunus Kanuni Ngenda
1
بسم الله الرحمن الرحيم
Utangulizi
Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe
vyote, na rehma na amani zimwendee Mtume wetu
Muhammad (s.a.w) na watu wake na Maswahaba wake wote.
Amma baad:
Mtu ni mwenye haja ya kula na kunywa. Kwa ajili hii Allaah
Hakumkataza mfungaji kula, kunywa na kufanya jimaa wakati
wa usiku isipokuwa tu wakati wa mchana, kuanzia pale
ambapo alfajiri inapoingia mpaka wakati jua linapozama.
Allaah Anapenda watu wale daku. Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam) amesema kuhusu daku:
“Kuleni daku. Hakika katika kula daku kuna baraka”.
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah (´Azza wa Jalla) na Malaika Wake wanawaswalia
wenye kula daku.”
(Ibn Hibbaan (3467),
Atw-Twabaraaniy i ”
Al-Awsatw” (6434) na
Abu Nu´aym (8/320). Hasan kwa mujibu wa al-Albaaniy
katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb” (1070).
Kwa nini daku?
Daku si ni chakula tu ambacho mtu anakula kwa matamanio?.
2
Kwa sababu nia yake ni kutekeleza maamrisho ya Allaah
ambayo ni kufunga, ili aweze kupata nguvu za kumuabudu
Allaah. Kwa ajili hio kila ambavyo daku itacheleweshwa ndio
bora zaidi:
”Na kuleni na kunyweni mpaka ibainike kwenu weupe (wa
Afajiri) kutokana na weusi (wa usiku).” (02:187)
Ama yule anayekula usiku mzima na kujaza tumbo lake kisha
analala nyuma na wala haamki kula daku pamoja na Waislamu
wenzake na wala haswali hata al-Fajr, huyu kwa hakika
hakutekeleza maamrisho ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
Amechofanya ni kutekeleza maamrisho na hawaa ya nafsi
yake. Yuko macho usiku mzima ambapo anakesha kwa
kumuasi Allaah na analala wakati ambapo anatakiwa kumtii
Allaah (´Azza wa Jalla).
CHANZO:
http://www.alfawzan.af.org.sa/node/%205824