1
بسم الله الرحمن الرحيم
CHANZO CHA KUDHIHIRIKA KWA BIDAA NA SABABU ZA KUDHIRI KWAKE. Imeandaliwa na kukusanywa na Yunus Kanuni. Imepitiwa na Abubakari shabani Rukonkwa. Kudhihirika kwa Bidaa katika maisha ya waislam, chini yake kuna mas'ala mawili: Mas'ala ya kwanza: Wakati wa kudhihirika Bidaa: Amesema Sheikhul Islaam Ibn Taimia- Allah amrehemu :- Elewa ya kwamba Bidaa kwa ujumla ambazo zinahusiana na elimu na Ibada, zimetokea na kuanzia katika Umma katika mwishomwisho wa (zama) Ukhalifa wa Makhalifa waongofu. Kama alivyotuhabarisha Mtume- swalla llaahu alayhi wasallam- pindi aliposema : Atakeishi miongoni mwenu baada yangu ataona ikhtilafu nyingi, basi ni juu yenu (kufuata) Sunna zangu na Sunna za Makhalifa waongofu baada yangu , na bidaa ya kwanza kudhihiri bidaa ya "qadari" na bidaa ya "irjaa" na bidaa ya "ushia" na ya "ukhawarij", Bidaa hizi
2
zilidhihirika katika karne ya pili na Maswahaba walikuwepo, na
waliwachukia wafanyaji bidaa,
Kisha ikadhihiri ya muu'tazila na ikatokea fitna baina ya
waislam na ikatokea ikhtilafu katika Rai na kumili katika Bidaa
na ufuataji wa matamanio, na ikadhihiri bidaa ya tasawwuf
(usufi) na bidaa ya kujengea juu ya Makaburi baada ya karne
bora, na kama hivyo kadri muda unavyokwenda zikazidi bidaa
nyingi katika aina tofauti tofauti.
Mas'ala ya pili:
Sehemu zilipodhihiri Bidaa. Miji ya kiislam inatofautiana katika
kudhihiri bidaa katika miji hiyo.
Amesema Shaykhul Islaam Ibn Taimia: Hakika katika miji
mikubwa ambayo walikaa maswahaba wa Mtume -swalla llaahu
alayhi wasallam-, na ikatokea katika miji hiyo Elimu na Imani ni
mitano: Khurasani na U'raqaani na Shaam, miongoni mwayo
ilipatikana elimu ya quran na hadithi na Fiq'hi na Ibada na
yanayoyafuatia hayo katika mambo ya Uislaam.
Na ikatokea katika miji hiyo bidaa asilia kinyume na mji wa
Madina; katika mji wa "Kuufat" ulitokea "ushia" na "Irjaa" na
ukaenea baada ya hapo katika miji mingine, Na mji wa Baswra
ikatokea "Qadaria" na "Muutazila" na ibada zenye kufisidika Na
mji wa "Shaam" kulikuwa na " Naswab" na " Qadaria", Ama
"Jahmiyyat" ilidhihirika katika mji wa "Khurasaan" na ni bidaa
yenye shari mno, Na ikawa kudhihirika/kutokea kwa Bidaa ni
kulingana na kuwa mbali na mji wa Mtume wetu
-swalla llaahu alayhi wasallam-,
3
Na baada ya kutokea mfarakano baada ya Mauaji ya Uthmaani -
radhi za Allah ziwe juu yake- ikatokea na kudhihirika bidaa ya
Haruriyat.
Na ama mji wa Madina ulikuwa umesalimika na kudhihirika
kwa bidaa hizi, pamoja na kuwa walikuwepo ambao
hawakudhihirika kwa hilo, wakawa mbele yao ni wenye
kufedheheka na wenye kulaumika, sababu kulikuwa katika mji
huo watu katika Qadaria(wapingaji wa qadari ) na wengineo,
lakini walikuwa ni wenye kutenzwa nguvu na wenye udhalili
kinyume na Ushia na Irjaa katika mji wa kuufat, na Muu'tazila
na Bidaa ya Nisaak katika mji wa Baswra, na Naswab huko
Shaam, hakika hizo zilikuwa dhahiri.
Imethibiti katika Swahihi, kutoka kwa Nabbiy- swalla llaahu
alayhi wasallam- kuhusu mji wa Madina, Masihi Dajjaal
hatoingia katika mji huo.
Elimu na Imani katika mji huo zimeendelea kudhihirika katika
zama za wanafunzi Imam Maalik, ambao ilikuwa ni watu wa
karne ya nne.
Ama katika "karne tatu bora" hakukuwa kabisa katika mji wa
Madina bidaa zilizodhihirika, na wala hakukutokea bidaa katika
misingi ya dini kabisa, kama vile ilivyokuwa katika miji
mingine.
4
SABABU AMBAZO ZIMEPELEKEA KUDHIHIRIKA KWA
BIDAA.
Katika mambo ambayo hayana shaka kabisa, hakika
kushikamana na kitabu cha Allah na Sunna za Mtume -swalla
llaahu alayhi wasallam- kuna kuokoka katika kuiingia Bidaa na
Upotevu(dhwalala). Amesema Allah- taala:-
(Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi
ifuateni, wala msifuate njia zingine, zikakutengeni na Njia yake.
Haya amekuusieni ili mpate kumcha mungu.)
[Surat Al-Anaam : 153]
Na hili, Mtume- swalla llaahu alayhi wasallam- ameliweka wazi,
kwa alivyopokea Ibn Mas'uud- radhi za Allah zimweendeeamesema:
Mtume- swalla llaahu alayhi wasallam- ametuchorea
msitari, akasema: "Hii ni njia ya Allah. kisha akachora mistari
5
kuliani na kushoto kwa huo msitari, kisha akasema: hivi ni vijinjia katika kila njia katika hivyo vijinjia Shetani analingania kwavyo, kisha akasoma:
(Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia zingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya amekuusieni ili mpate kumcha mungu)." [Ameipokea Imam Ahmad:( 1/435), Na Daarimiy (katika Sunan yake) kwa chapa ya Academy ya Pakistani 1414 Hijiria, hadithi nambari (208).] Yule atakaepinga na kujiweka mbali na kujiepusha na Kitabu cha Allah na Sunna za Mtume wake- swalla llaahu alayhi wasallam- ataingia katika hizo njia zingine na Bidaa zilizozushwa, Na sababu ambazo zimepelekea kudhihiri kwa bidaa, kwa mukhtasari katika mambo yafuatayo:- Na tunazifafanua kwa kifupi: 1-UJINGA ( UJAHILI) KATIKA HUKUMU ZA MAMBO YA KIDINI:- Kadri zama zinavyoongezeka na kadri watu wanavyozidi kuwa mbali na Athari za Ujumbe, elimu inapungua na ujinga unaongezeka, kama alivyotuhabarisha hilo,
6
Mtume- swalla llaahu alayhi wasallam- kwa kauli yake: "Atakae ishi miongoni mwenu baada yangu Ataona ikhtilaafu nyingi sana", na kauli yake: " Hakika Allah haichukui(kuiua/kuimaliza) elimu kwa kuichukua kutoka kwa waja, lakini anaichukua(anaimaliza) kwa kuwafisha Ulamaa(Wanazuoni), mpaka inafikia hatobakia mwanachuoni (Aalim), ndipo watu watachukua wakuu wa wajinga, watawauliza (hao wajinga) na (watawajibu)watawatolea fat'wa bila ya elimu, watapotea (hao wajinga) na watawapoteza watu......" Hawezi kuipima na kuijua Bidaa isipokuwa kwa njia ya Elimu na Ulamaa(Wanachuoni), Pindi zitakapokosekana elimu na Ulamaa inapatikana fursa ya kudhihirika kwa Bidaa na kuenea na watu wa bidaa kupata nguvu na nishati. 2-KUFUATA MATAMANIO YA NAFSI: Yule anayepingana na Kitabu cha Allah na Sunna za Mtume wake- swalla llaahu alayhi wasallam- ni mwenye kufuata matamanio. Kama alivyosema Allah -taala:- ( Na ikiwa hawakuitikii, basi jua kuwa wanafuata matamanio yao tu. Na nani aliyepotea zaidi kumshinda anaye fuata matamanio yake bila ya uwongofu utokao kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye
7
kudhulumu) [Surat Al-Qasas : 50] Na Amesema- taala-
( Je! Umemwona aliye fanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu akamwacha apotee pamoja na kuwa ana ujuzi, na akapiga muhuri juu ya masikio yake, na moyo wake, na akambandika vitanga machoni mwake? Basi nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu? Je Hamkumbuki?) [Surat Al-Jathiya : 23] Na Bidaa ni vazi la matamanio ya mfuataji. 3-TAA'SWUB NA RAI ZA WATU Taa'swub maana yake ni kukusanyika katika jambo na kulitetea na kulinusuru, Kuwa na Taa'swub na Rai za watu kunakaa kati ya "mtu" na "kufuata dalili na kuifahamu haki", Amesema Taala:
(Na wanapo ambiwa: Fuateni aliyo yateremsha Mwenyezi
8
Mungu; wao husema: Bali tutafuata tuliyo wakuta nayo baba zetu. Je, hata ikiwa baba zao walikuwa hawaelewi kitu, wala hawakuongoka?) [Surat Al-Baqara : 170] Na hiyo ndio shani ya wenye taa'sub, leo hii katika baadhi ya wanaofuata madhehebu na Masufi na Qubuuriy (wenye kuabudu makaburi), wakifanyiwa daawa (wakiitwa) wafuate Kitabu na Sunna na kuyaacha yale waliyonayo ambayo yanapingana na kitabu na Sunna, huwa wanahitajia madhehebu yao na masheikh zao na baba zao na mababu zao. 4-KUWAIGA MAKAFIRI Na hii ndio sababu kubwa sana ya nyingi katika Bidaa, Kama ilivyokuja kwenye hadith ya Abu Waaqid Al-laythiy, amesema: Tulitoka na Mtume- swalla llaahu alayhi wasallam- kuelekea Hunayn,hali ya kuwa wenye kusilimu karibuni, na washirikina walikuwa na Mti wa mkunazi wanauabudu, na wanatundika silaha zao, uanitwa " Dhaatu An-maatw", tukawa tumeupita huo mti, tukasema: Ewe mjumbe wa Allah, Tujaalie na sisi "Dhaatu Anmaatw" kama vile wao walivyokuwa na "Dhaatu Anmaatw"? Akasema Mtume -swalla llaahu alayhi wasallam: Allahu Akbar, huo mliosema ni mwenendo- naapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo mkononi mwake- (hiyo ni) Kama walivyosema Banuu Israail kumwambia Mussa: tujaalie na sisi mungu kama walivyo wao na miungu, Akasema (Musa) hakika nyinyi ni watu wajinga", mtafuata mienendo ya waliokuwa kabla yenu.
9
[ Ameipokea Tirmidhiy, hadith nambari(2180), na Twabarani katika " Al-muujam al-kabiyr"( chapa ya Muasasa wa Ihyaai al-turaath Ala'rabiy- ya pili 1405 Hijria),hadithi nambari(3291).] Katika Hadithi hii kuwaiga makafiri ndiko kulikowafanya Banii Israail na baadhi ya maswahaba (ambao waliokuwa wapya kusilimu kwao) kuomba ombi hili baya kwa Mtume wao, ambalo lilikuwa kuwajaalia kijiungu wakiabudu na watabaruku kwacho kinyume na Allah -tabaaraka wat-aala- NA HII NI SAWASAWA KABISA NA YANAYOTOKEA HIVI LEO, HAKIKA WENGI KATIKA WATU KATIKA WAISLAMU WAMEWAIGA MAKAFIRI KATIKA MATENDO YA KI-BIDAA NA KISHIRIKINA KAMA VILE SIKUKUU ZA KUZALIWA, NA KUSIMAMISHA BAADHI YA MASIKU NA WIKI KWA AJILI YA MATENDO FULANI MAALUMU, NA KUSHEREHEKEA KATIKA MINASABA YA KIDINI NA DHIKIRI, NA KUFANYA MAIGIZO NA MINASABA YA KUJIKUMBUSHA, NA MAMBO YA KUKAA MATANGA, NA KATIKA MAMBO YA MAZISHI, MAMBO YA KUJENGEA MAKABURI NA MENGINEYO.