1
ADABU ZA KULA
BISMI LLAHI RRAH MANI RRAHIIM
Utangulizi
Baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumtakia Rehma
na amani Nabii Muhammad (s.a.w) pamoja na familia yake na
Maswahaba zake na Waislamu wote watakao fuata mwenendo
wake mpaka siku ya mwisho tuna muomba Mwenyezi Mungu
atujaalie nasi tuwe miongoni mwahao Aamiin.
Kutoka kwa AbaHuraira (r.a) amesema: Amesema Mtume
Muhammad (s.a.w): (Hakika jambo la kwanza atakalo ulizwa
mja siku ya kiyama miongoni mwa neema, ataambiwa:
Jee! Sijakupa afya njema na kukunywesha maji ya baridi?).
kapokea hadithi hii Imam Tirmidhi.
MIONGONI MWA ADABU ZA KULA:
1: Kutaja jina la Mwenyezi Mungu Mwanzo wa kula kwako.
Kutoka kwa Bibi Aisha (r.a) kwamba Mtume (s.a.w) amesema:
(atapo kula Mmoja wenu ataje jina la Mwenyezi Mungu
Mtukufu, akisahau kutaja jina la Mwenyezi Mungu Mwanzo wa
kula, asema: kwa jina la Mwenyezi Mungu mwanzo wake na
mwisho wake). Kapokea hadithi hii Imam Tirmidhi, na Ahmad,
na Daramy.
2: kusema Bismi llahi, ni kila mtu, sio kwamba akisema Mmoja
anawatosheleza wengine anao kula nao, kwa sababu Sunna hii
niya kila mtu inatakiwa aiseme, wala usiifananishe na Salamu,
Hadithi ya Amru bin Salama (r.a) wakati aliambiwa na Mtume
(s.a.w): (Ewe kijana! Sema: Bismillahi, na ule kwa mkono wako
wa kulia, na ule mbele yako).
3
3: NAMNA YA KUSEMA BISMILLAHI WAKATI WA
KULA NA KUNYWA:
Aseme: Bismillah, wala asizidishe Arrahmani rrahiim. Laity
akisema: Bismillahi Rrahmani Rrahiim, atakuwa kenda kinyume
na Sunna.
Kwa hakika limepokelewa tamko la wazi la (Bismillah) katika
hadithi alio ipokea Imam Abii Daud na Tirmidhi, na
kaisahihisha Shekh Albani (r.h) kwa hadithi ya Bibi Aisha (r.a)
amesema: amesema Mtume (s.a.w):
(Atapo kula Mmoja wenu chakula, na aseme: Bismillah).
Na katika hadithi nyingine, kutoka kwa Amru (r.a) amesema:
nilikuwa kijana mdogo katika malezi ya Mtume (s.a.w) mkono
wangu ulikuwa hautulii kwenye sahani ya chakula, akaniambia
Mtume (s.a.w): (Ewe kijana! Utakapo anza kula, useme:
Bismillah).
Kapokea hadithi hii Imam Twabarani, na akasema Shekh Albani
upokezi wake ni sahihi, kwa sharti za Imam Bukhari na Muslim,
zingatia hili kwa sababu ni muhimu sana kwa wale wanao
tukuza Sunna, na wala hawakubali kuzidisha zaidi ya Bismillah.
Angalia Irwail-Ghaliil, (3/31).
Kwa haya machache tuna muomba Mwenyezi Mungu atujaalie
tuyafanyie kazi haya na mengine Inshaallah!.
Ewe Mola wetu zipeleke Rehma na Amani kwa Mtume wetu
Muhammad (s.a.w) pamoja Familia yake na Maswahaba haze na
Waislamu wote hadi siku ya mwisho. Aamiin.