Nakala

Shughuli za Mtume, Mungu ampe baraka, na dini nyingine inaweza kuelezewa vyema zaidi katika aya ya Kurani:





“Kuweni kwenu na dini yenu, kwangu mimi niwe na yangu.”





Peninsula ya Arabia katika zama za Mtume lilikuwa ni eneo ambalo imani mbalimbali zilikuwepo. Kulikuwa na Wakristo, Wayahudi, Wazoroastria, washirikina, na wengine wasiofungamana na dini yoyote. Mtu anapotazama maisha ya Mtume, anaweza kuteka mifano mingi ili kuonyesha uvumilivu wa hali ya juu ulioonyeshwa kwa watu wa imani nyingine.





Ili kuelewa na kuhukumu uvumilivu huu, mtu lazima aangalie katika kipindi ambacho Uislamu ulikuwa dola rasmi, na sheria mahususi zilizo wekwa na Mtume kwa mujibu wa kanuni za dini. Ingawa mtu anaweza kuona mifano mingi ya uvumilivu iliyoonyeshwa na Mtume katika miaka kumi na tatu ya kukaa kwake Makka, mtu anaweza kufikiri kimakosa kwamba ilitokana tu na kutaka kuinua hadhi ya Waislamu na hadhi ya kijamii ya Uislamu na kwa ujumla. Kwa sababu hii, majadiliano yatahusu kipindi ambacho kilianza kwa Mtume kuhama kwenda Madina, na hasa mara tu katiba ilipowekwa.





Swahiyfah


Mfano bora zaidi wa uvumilivu ulioonyeshwa na Mtume kwa dini zingine unaweza kuwa ni katiba yenyewe, inayoitwa ‘Swahiyfah’ na wana historia wa mwanzo.[1] Mtume alipohamia Madina, jukumu lake kama kiongozi wa kidini liliisha; sasa alikuwa kiongozi wa kisiasa wa dola, iliyotawaliwa na kanuni za Uislamu, ambazo zilitaka sheria za utawala ziwekwe wazi ili kuhakikisha maelewano na utulivu katika jamii ambayo hapo awali ilikuwa imefadhaishwa na miongo ya vita, ambayo lazima ihakikishe kuishi pamoja kwa amani Waislamu, Wayahudi, Wakristo na washirikina. Kutokana na hili, Mtume aliweka ‘katiba’ ambayo ilieleza kwa kina majukumu ya pande zote zilizokuwa zikikaa Madina, wajibu wao kwa kila mmoja wao kwa wao, na vikwazo fulani ambavyo viliwekwa kwa kila mmoja. Washiriki wote walipaswa kutii yale yaliyotajwa humo, na uvunjaji wowote wa vipengele vyake ulizingatiwa kuwa ni kitendo cha usaliti.





Nchi Moja


Kifungu cha kwanza cha katiba kilikuwa kwamba wakaaji wote wa Madina, Waislamu na vilevile wale walioingia kwenye mapatano hayo kutoka kwa Wayahudi, Wakristo, na waabudu masanamu, walikuwa “taifa moja bila ya kuwatenga wengine wote.” Wote walichukuliwa kuwa wanachama na raia wa jamii ya Madina bila kujali dini, rangi, au ukoo. Watu wa imani nyingine walilindwa dhidi ya madhara kama vile Waislamu, kama ilivyoelezwa katika makala nyingine, “Kwa Wayahudi wanaotufuata wanapata msaada na usawa. Hatadhurika wala adui zake hawatasaidiwa.” Hapo awali, kila kabila lilikuwa na mapatano na maadui ndani na nje ya Madina. Mtume aliyakusanya makabila haya tofauti chini ya mfumo mmoja wa utawala ambao ulishikilia mapatano yaliyokuwepo hapo awali baina ya makabila hayo binafsi. Makabila yote yalipaswa kutenda kwa ujumla bila kujali mapatano ya watu binafsi. Shambulio lolote dhidi ya dini nyingine au kabila lilionekana kuwa ni shambulio dhidi ya serikali na Waislamu pia.





Maisha ya watendaji wa dini nyingine katika jamii ya Kiislamu pia yalipewa hali ya ulinzi. Mtume akasema:





“Mwenye kumuua mtu ambaye ana mapatano na Waislamu hatasikia harufu ya Pepo.” (Saheeh Muslim)





Kwa vile wakubwa walikuwa pamoja na Waislamu, Mtume alionya vikali dhidi ya unyanyasaji wowote wa watu wa imani nyingine. Alisema:





“Jihadhari! Yeyote anayewadhulumu watu wachache wasiokuwa Waislamu, au anawapunguzia haki zao, au akawatwika zaidi ya uwezo wao, au akawanyang'anya chochote kwa hiari yao; Mimi (Mtume Muhammad) nitamlalamikia mtu huyo Siku ya Kiyama.” (Abu Dawud)





Kwa Kila Mmoja Dini Yake


Katika makala nyingine, inasema, “Wayahudi wana dini yao na Waislamu wana dini yao.” Katika hili, ni wazi kwamba jambo lolote lile isipokuwa uvumilivu lisingevumiliwa, na kwamba, ingawa wote walikuwa wanajamii, kila mmoja alikuwa na dini yake tofauti ambayo isingeweza kukiukwa. Kila mmoja aliruhusiwa kutenda imani yake kwa uhuru bila vizuizi vyovyote, na hakuna vitendo vya uchochezi ambavyo vingevumiliwa.





Kuna vifungu vingine vingi vya katiba hii ambavyo vinaweza kujadiliwa, lakini msisitizo utawekwa kwenye kifungu kinachosema, "Iwapo mzozo wowote au mabishano yatatokea, ni lazima yaelekezwe kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake." Kifungu hiki kilisisitiza kwamba wakazi wote wa dola lazima watambue mamlaka ya juu zaidi, na katika mambo yale yanayohusisha makabila na dini mbalimbali, haki isingeweza kutekelezwa na viongozi binafsi; bali ni lazima iamuliwe na kiongozi wa nchi mwenyewe au wawakilishi wake aliowateua. Iliruhusiwa, hata hivyo, kwa makabila ya watu binafsi ambao hawakuwa Waislamu, kurejelea maandiko yao ya kidini na wasomi wao kuhusiana na mambo yao binafsi. Wangeweza, kama wangeamua, kumwomba Mtume atoe hukumu baina yao katika mambo yao. Mwenyezi Mungu anasema katika Kurani:





“…Basi wakikujia, wahukumu baina yao au jipuuze nao....” (Kurani 5:42)





Hapa tunaona kwamba Mtume aliiruhusu kila dini ihukumu katika mambo yao wenyewe kwa mujibu wa maandiko yao wenyewe, ilimradi haikusimama kinyume na ibara za katiba, mapatano ambayo yalizingatia faida kubwa ya ushirikiano wa amani kuwepo kwa jamii.





Kuna mifano mingine mingi katika zama za uhai wa Mtume, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, pamoja na Swahiyfah inayoonyesha kivitendo uvumilivu wa Uislamu kwa dini nyinginezo.





Uhuru wa Mikusanyiko ya Kidini na Kujitegemea Kidini


Kwa kupata kibali cha katiba, Wayahudi walikuwa na uhuru kamili wa kufuata dini yao. Wayahudi wa Madina wakati wa Mtume walikuwa na shule yao ya elimu, iliyoitwa Bait-ul-Midras, ambapo walikuwa wakisoma Taurati, kuabudu na kujielimisha.





Mtume alisisitiza katika barua nyingi kwa wajumbe wake kwamba taasisi za kidini zisidhuriwe. Hapa katika barua iliyotumwa kwa mjumbe wake kwa viongozi wa kidini wa Mtakatifu Catherine katika Mlima Sinai ambaye aliomba ulinzi wa Waislamu:





“Huu ni ujumbe kutoka kwa Muhammad ibn Abdullah, kama agano kwa wale wanaofuata Ukristo, walio karibu na walio mbali, tuko pamoja nao. Hakika mimi, waja, wasaidizi, na wafuasi wangu nawa walinda, kwa sababu Wakristo ni raia wangu; na kwa Mungu! Ninashikilia dhidi ya chochote kisichowapendeza. Hakuna kulazimishwa kuwa juu yao. Wala majaji wao hawatakiwi kuondolewa katika kazi zao wala watawa wao kutoka katika nyumba zao za watawa. Hakuna mtu wa kuiharibu nyumba ya dini yao, kuibomoa, au kubeba chochote kutoka humo kupeleka kwenye nyumba za Waislamu. Na yeyote akichukua chochote katika haya basi ataharibu ahadi ya Mwenyezi Mungu na kumuasi Mtume wake. Hakika hao ni washirika wangu na wana hati yangu iliyo salama dhidi ya yale wanayoyachukia. Hakuna mtu wa kuwalazimisha kusafiri au kuwalazimisha kupigana. Waislamu wanapaswa kuwapigania. Ikiwa Mkristo wa kike ameolewa na Muislamu, haitafanyika bila idhini yake. Hatakiwi kuzuiwa kutembelea kanisa lake kuomba. Makanisa yao yanatangazwa kulindwa. Hawapaswi kuzuiwa kuyatengeneza wala kuweka utakatifu wa maagano yao. Hakuna hata mmoja katika nchi (Muislamu) atakayevunja ahadi mpaka Siku ya Mwisho (mwisho wa dunia).”[1]





Kama mtu awezavyo kuona, Mkataba huu ulikuwa na vifungu kadhaa vinavyoshughulikia masuala yote muhimu ya haki za binadamu, vikiwemo mada kama vile ulinzi wa walio wachache wanaoishi chini ya utawala wa Kiislamu, uhuru wa kuabudu na kutembea, uhuru wa kuwateua majaji wao wenyewe na kumiliki na kudumisha haki mali zao, kutoenda kwenye utumishi wa kijeshi, na haki ya kulindwa vitani.





Katika tukio jingine, Mtume alipokea ujumbe wa Wakristo sitini kutoka eneo la Najran, ambalo wakati huo lilikuwa sehemu ya Yemeni, kwenye msikiti wake. Wakati wa swala yao ulipofika, walielekea upande wa mashariki na wakaswali. Mtume akaamuru waachwe katika hali yao na wasidhuriwe.





Siasa


Pia kuna mifano katika maisha ya Mtume ambapo alishirikiana na watu wa imani nyingine katika uwanja wa kisiasa. Alimchagua asiye Muislamu, Amr-ibn Umaiyah-ad-Damri, kama balozi atakayetumwa kwa Negus, Mfalme wa Ethiopia.





Hii ni baadhi tu ya mifano ya ustahimilivu wa Mtume kwa imani nyingine. Uislamu unatambua kwamba kuna wingi wa dini katika dunia hii, na unawapa haki watu binafsi kuchagua njia wanayoamini kuwa ni ya kweli. Dini haitakiwi, na kamwe haikulazimishwa kwa mtu binafsi kinyume na matakwa yao wenyewe, na mifano hii kutoka katika maisha ya Mtume ni mukhtasari wa aya ya Quran ambayo inakuza uvumilivu wa kidini na kuweka muongozo wa maingiliano ya Waislamu pamoja na watu wa imani nyingine. Mungu anasema:





“…Hapana kulazimisha katika Dini.…” (Kurani 2:256)



Machapisho ya hivi karibuni

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL

Masuala kumi muhimu n ...

Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Muharram

UJUMBE KWA ALIYEICHOM ...

UJUMBE KWA ALIYEICHOMA KURANI