Nakala

Ikiwa mtu angeuliza, ‘Ni nani Mungu wako?’ Jibu la Muislamu lingekuwa, ‘Mwingi wa Rehema, Mgawaji wa Rehema.’ Kulingana na vyanzo vya Kiislamu, manabii, huku wakikazia hukumu ya Mungu, pia walitangaza rehema Yake. Katika maandiko ya Kiislamu, Mwenyezi Mungu anajitambulisha kama:





“Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mwenye kuyajua yaliyo fichikana na yanayo onekana. Yeye ndiye Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.” (Kurani 59:22).





Katika msamiati wa Kiislamu ar-Rahman na ar-Raheem ni majina binafsi ya Mungu Aliye Hai. Yote yamechukuliwa kutoka kwa nomino rahmah, ambayo inaashiria "rehema", "huruma", na "huruma ya upendo". Ar-Rahman inaelezea asili ya Mwenyezi Mungu ya kuwa Mwenye kurehemu, wakati ar-Raheem inaelezea matendo Yake ya rehema yaliyotolewa kwa viumbe Vyake, utofauti iliofichika, lakini ambao unaonesha rehema zake zote.





"Sema, ‘Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), au mwombeni (Rahman) Mwingi wa Rehema, kwa jina lolote mnalo mwita – Kwani Yeye ana majina mazuri....’" (Kurani 17:110)





Majina haya mawili ni baadhi ya Majina ya Mwenyezi Mungu yanayotumika sana katika Quran: ar-Rahman imetumika mara hamsini na saba, wakati ar-Raheem imetumika mara mbili zaidi (mia na kumi na nne).[1]  Moja huwasilisha hisia kubwa ya ukarimu na upendo, Mtume alisema:





"Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkarimu, na anapenda ukarimu. hutoa kwa upole asiyetoa kwa ukali." (Saheeh Muslim)





Zote pia ni sifa za kimungu zinazoashiria uhusiano wa Mungu na uumbaji.





"Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote; Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu." (Kurani 1:2-3)





Katika sala ambayo Waislamu huisoma angalau mara kumi na saba kwa siku, huanza kwa kusema:





"Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.  Sifa njema zote ni za Mwenyeezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote; Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu.."  (Kurani 1:1-3)





Maneno haya yenye nguvu yanaibua jibu la Mungu:





"Mja anaposema: ‘Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote’ Mimi (Mwenyezi Mungu) husema: ‘Mja wangu amenisifu.’  Anaposema: ‘Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu.,’ Mimi (Mwenyezi Mungu) husema: ‘Mja wangu amenitukuza.’" (Saheeh Muslim)





Majina haya mara kwa mara yanamkumbusha Muislamu kuhusu rehema ya Mwenyezi Mungu inayomzunguka. Sura zote isipokuwa moja tu za Maandiko ya Kiislamu zinaanza kwa maneno, ‘Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.’  Waislamu huanza kwa Jina la Mungu kuonyesha utegemezi wao wa mwisho juu Yake na kujikumbusha juu ya rehema ya Mungu kila wakati wanapokula, kunywa, kuandika barua, au kufanya jambo lolote la maana. Roho huchanua katika ulimwengu. Dua mwanzoni mwa kila tendo la ki ulimwengu huifanya kuwa la muhimu, ikiita baraka ya Mungu juu ya tendo hilo na kulitakasa. Kanuni hii ni mapambo maarufu katika maandishi na mapambo ya usanifu.





"Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu."  Maandishi ya Yousef, msanii wa Uholanzi.


Kutoa rehema kunahitaji mtu ambaye ameonyeshwa rehema. Anayeonyeshwa rehema lazima awe mhitaji. Rehema kamilifu ni kuwajali wale wanaohitaji, ambapo rehema isiyo na kikomo inaenea kwa wale wanaohitaji au wasio na uhitaji, inaenea kutoka kwa ulimwengu huu hadi maisha ya kushangaza baada ya kifo.





Katika mafundisho ya Kiislamu, wanadamu wanafurahia uhusiano binafsi na Mungu Mwenye Upendo, Mwenye Rehema, aliye tayari kusamehe dhambi na kuitikia maombi, lakini Yeye si mwenye huruma wa kibinadamu wa kuhisi huzuni na huruma kwa mtu aliye katika dhiki. Mungu haji kuwa mwanadamu ili kuelewa mateso. Badala yake, rehema ya Mungu ni sifa inayolingana na utakatifu Wake, inaleta usaidizi wa kimungu na upendeleo.





Rehema za Mungu ni nyingi sana:





"Sema: Mola Mlezi wenu ni Mwenye rehema iliyo enea.….’" (Kurani 6:147)





Kuenea kwa uwepo wote:





"…na rehema yangu imeenea kila kitu…." (Kurani 7:156)





Uumbaji wenyewe ni kielelezo cha upendeleo wa kimungu, rehema na upendo. Mungu anatualika kutazama athari za rehema yake karibu nasi:





"Basi ziangalie athari za rehema ya Mwenyezi Mungu, jinsi anavyo ihuisha ardhi baada ya kufa kwake!..." (Kurani 30:50)





Mungu Anawapenda wenye Huruma


Mungu anapenda huruma. Waislamu wanauona Uislamu kuwa ni dini ya rehema. Kwao, Mtume wao ni rehema ya Mwenyezi Mungu kwa watu wote.





"Na hatukukutuma, (ewe Nabii), ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote" (Kurani 21:107)





Kama vile wanavyoamini kuwa Yesu alikuwa rehema ya Mungu kwa watu:





"Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu." (Kurani 19:21)





Mmoja wa mabinti wa Mtume Muhammad rehma na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alimpelekea habari za mtoto wake aliyekuwa mgonjwa. Akamkumbusha kuwa Mwenyezi Mungu ndiye anaye toa, ndiye anaye twaa, na kila mtu ana muda maalumu. Akamkumbusha kuwa mvumilivu. Habari za kifo cha mwanawe zilipomfikia, machozi ya huruma yalitiririka machoni pake. Wenzake walishangaa. Mtume wa Rehema alisema:





"Hii ni huruma Mungu ameiweka ndani ya mioyo ya waja wake. Katika waja wake wote, Mungu huwahurumia tu wenye huruma." (Saheeh Al-Bukhari)





Wamebarikiwa wenye kurehemu, kwani watahurumiwa, kama Mtume Muhammad alivyosema:





"Mungu hatamrehemu mtu asiye na huruma kwa watu." (Saheeh Al-Bukhari)





Pia alisema:





"Mwingi wa rehema huwaonea huruma wenye kurehemu. Warehemu waliomo ardhini, na Yeye aliye juu ya mbingu atakurehemu." (At-Tirmidhi)





Wakati fulani katika maisha yetu, kila mtu anajiuliza maswali makuu: “Ni nani aliyetuumba,” na “Kwa nini tuko hapa?” 





Kwa hivyo ni nani aliyetuumba? Wakanaji Mungu wanasema Mshindo Mkubwa na mageuzi, huku wengine wote wanamzungumzia Mungu. Wale wanaojibu “Sijui” ni Wakanaji Mungu kwa makusudi, si kwa sababu wanakataa kuwepo kwa Mungu, bali kwa sababu wanashindwa kuthibitisha uwepo wake. Sasa, Mshindo Mkubwa unaweza kueleza asili ya ulimwengu, lakini hauelezi asili ya wingu la vumbi la kwanza. Wingu hili la vumbi (ambalo, kwa mujibu wa nadharia, limeungana na kisha kulipuka) lilipaswa kutoka mahali fulani. Isitoshe, lilikuwa na vipengele vya kutosha kutengeneza sio kundi letu la nyota tu, bali mabilioni ya makundi mengine ya nyota katika ulimwengu unaojulikana. Basi, hilo lilitoka wapi? Nani, au nini, iliunda wingu la vumbi la kwanza?





Vile vile, mageuzi yanaweza kueleza rekodi ya kisukuku, lakini hayawezi kueleza kiini ya maisha ya binadamu; nafsi. Sisi sote tuna nafsi moja. Tunahisi uwepo wake, tunaongelea kuwepo kwake na wakati mwingine kuomba wokovu wake. Lakini ni wenye dini tu ndio wanaweza kueleza ilitoka wapi. Nadharia ya uteuzi ya kiasili inaweza kueleza mambo mengi ya maisha yanayoonekana, lakini inashindwa kueleza nafsi ya binadamu..





Zaidi ya hayo, mtu yeyote anayechunguza utata wa maisha na ulimwengu hawezi kufanya mengi zaidi ya kushuhudia ishara na dalili za Muumba.[1] Ikiwa watu wanatambua ishara hizi ni jambo lingine—kama msemo wa kale unavyosema; kukataa sio mto tu nchini Misri. Hoja ni kwamba tukiona uchoraji, tunajua kuna mchoraji. Tukiona uchongaji, tunajua kuna mchongaji; tukiona sufuria, mfinyanzi. Hivyo tunapotazama uumbaji, je, hatupaswi kujua kuna Muumba?





Dhana ya kwamba ulimwengu ulilipuka na kisha ukatengenezeka kwa ukamilifu na uwiano kutokana na matukio ya kiholela na uteuzi wa kiasili ina tofauti ndogo na pendekezo la kwamba, kwa kuangusha mabomu ndani ya takataka, moja kati ya mabomu hizi italeta kila kitu pamoja na kuunda gari la Mercedes kamili.





Kama kuna jambo moja tunajua kwa uhakika, ni kwamba bila udhibiti, mifumo yote huharibika na kuchanganyika. Hata hivyo, Nadharia za Mshindo Mkubwa na mageuzi zinapendekeza kinyume kabisa, -  msukosuko huu ulizua ukamilifu. Je, si jambo la busara zaidi kusema kwamba Mshindo Mkubwa na mageuzi yalikuwa matukio yaliyodhibitiwa? Yaliyodhibitiwa, yaani, na Muumba?





Mabedui wa Arabia husimulia hadithi ya mhamaji anayepata jumba la kufurahisha karibu na chemchemi katikati ya jangwa. Anapouliza jinsi ilivyojengwa, mmiliki anamwambia iliundwa na nguvu za kimaumbile. Upepo uliunda miamba na kuivuma hadi kwa eneo la chemchemi hili, halafu ukaiweka pamoja kutengeneza jumba hili la kifalme. Kisha ukapiga mchanga na mvua ndani ya nyufa ili kuyaimarisha pamoja. Kisha, ulivuma vipande vya pamba ya kondoo pamoja kuunda mazulia na matandiko, na kuleta kuni pamoja na kuunda samani, milango, na madirisha, na kuziweka kwa jumba hilo katika maeneo yanayofaa. Mapigo ya Umeme yaliyeyusha mchanga na kuunda vioo na kuviweka kwenye fremu za madirisha, na kisha kubadilisha mchanga mweusi kuwa chuma na kuiweka kwa uzio na mlango kwa usawa kamili na ulinganifu. Mchakato huo ulichukua mabilioni ya miaka na ulifanyika tu mahali hapa duniani—kibahati tu.





Tunapomaliza kukodoa macho, tunapata uhakika. Ni wazi kwamba jumba hilo lilijengwa na kubuniwa, na halikutokea kibahati. Ni kitu gani (au mtu yupi), basi, tunapaswa kusema kuwa ndiye alisababisha asili ya vitu vya utata mkubwa zaidi, kama vile ulimwengu wetu na sisi wenyewe?





Hoja nyingine ya kukataa dhana ya Uumbaji inalenga kile ambacho watu wanaona kuwa ni kutokamilika kwa uumbaji. Hizi ni kama “Jinsi gani kunaweza kuwa na Mungu ilhali vitu kama hiki na kile vinatokea?”. Suala linalojadiliwa linaweza kuwa lolote kuanzia maafa ya kimaumbile hadi kasoro za kuzaliwa, kuanzia mauaji ya halaiki hadi saratani ya nyanya wa mtu. Hiyo siyo hoja. Hoja ni kwamba kumkataa Mungu kulingana na kile tunachokiona kuwa ni udhalimu wa maisha ni kufikiri kwamba Mungu hangetengeneza maisha yetu kuwa kitu chochote isipokuwa kamilifu, na kungekuwa na uimara na haki duniani.





Hmm … je, hakuna chaguo jingine?





Tunaweza kwa urahisi kupendekeza kwamba Mungu hakutengeneza maisha duniani kuwa pepo, bali ni mtihani, adhabu au tuzo ambazo zinapaswa kutokea katika maisha ya pili, ambapo Mungu anaweka haki Yake ya mwisho. Kwa kuunga mkono dhana hii tunaweza kuuliza ni kina nani waliopata dhuluma zaidi katika maisha yao ya kidunia kuliko wapendwa wa Mungu, ambao ni manabii? Na ni nani tunatarajia kuchukua vituo vya juu zaidi peponi, ikiwa sio wale wenye imani ya kweli wanapokabiliwa na shida za kidunia? Kwa hivyo kuteseka katika maisha haya ya kidunia sio lazima kutafsiriwa kuwa ni hasira ya Mungu, na maisha ya kidunia yenye furaha haimaanishi kuwa maisha ya baadaye yatakuwa hivyo.





Natumai kuwa, kutokana na hoja hii, tunaweza kukubaliana kuhusu jibu la “swali kuu” la kwanza. Ni nani aliyetuumba? Je, tunaweza kukubaliana kwamba ikiwa tumeumbwa, Mungu ndiye Muumba?





Kama hatuwezi kukubaliana juu ya hoja hii, pengine hakuna haja kubwa ya kuendelea. Hata hivyo, kwa wale wanaokubali, tuendelee kwenye “swali kuu” la pili-kwa nini tuko hapa? Nini, kwa maana nyingine, ndiyo kusudi la maisha?


 



Machapisho ya hivi karibuni

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL

Masuala kumi muhimu n ...

Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Muharram

UJUMBE KWA ALIYEICHOM ...

UJUMBE KWA ALIYEICHOMA KURANI