Nakala

Pindi mtu anaposilimu, Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zake zote zilizopita na matendo ya kishetani.  Mwanaume anaeitwa Amr alikuja kwa Mtume Muhammad, Baraka na rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na akasema, “Nipe mkono wako wa kulia ili nikupe kiapo cha uaminifu.”  Mtume akatoa mkono wake wa kulia.  Amr akarudisha mkono wake.  Mtume akasema: “Kimekupata nini, Wewe Amr?”  akajibu, “Ninakusudia kuweka sharti.”  Mtume akauliza: “Sharti gani umekusudia kulileta mbele?”  Amr akasema, “Kwamba Mungu anisamehe dhambi zangu.”  Mtume, baraka na rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akasema,: “Je, haujui kuwa kusilimu kunafuta dhambi zote zilizopita?”[1]





Baada ya kusilimu, mtu atatunzwa kwa matendo yake mazuri na mabaya kulingana na usemi ufuatao wa Mtume Muhammad: “Mola Wako, Mwenye baraka na aliye juu,ni mwingi wa rehema. Kama mtu ameazimia kufanya kitendo kizuri ila hakufanya, kitendo hicho kizuri kitanakiliwa kwake.  Na kama akikifanya, (atatunzwa) mara kumi hadi mia saba au mara nyingi zaidi (ya tunzo ya kitendo kizuri), kitanakiliwa kwake.  Na kama mtu ataazimia kufanya kitendo kibaya na hakukifanya, kitendo kizuri kitanakiliwa kwake.  Na kama akikifanya, kitendo kibaya kitanakiliwa kwake au Mola atakifuta.”[2]



Machapisho ya hivi karibuni

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL

Masuala kumi muhimu n ...

Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Muharram

UJUMBE KWA ALIYEICHOM ...

UJUMBE KWA ALIYEICHOMA KURANI