Nakala

Furaha ya kweli na amani inapatikana kwa kutii amri za Muumba na Mtegemezi wa ulimwengu huu. Mungu amesema katika Kurani:





"Kwa kweli, katika kumkumbuka Mungu mioyo hupata raha na utulivu." (Kurani 13:28)





Kwa upande mwingine, yule ambaye hatakifuata kitabu kitukufu atakuwa na maisha ya shida katika ulimwengu huu. Mungu amesema:





" Atakayeiacha Qur'ani,[1] atakuwa na maisha magumu, na tutamfufua kipofu katika siku ya Kiyama." (Kurani 20: 124)





Hii inaweza kuwa kielelezo ni kwanini watu wengine hujiua wakati wanafurahia raha ya mali inayoweza kununuliwa na pesa. Kwa mfano, angalia Cat Stevens (sasa Yusuf Islam), zamani alikuwa mwimbaji maarufu wa 'pop' ambaye alikuwa akipata zaidi ya dola 150,000 kwa usiku. Baada ya kusilimu, alipata furaha ya kweli na amani, ambayo hakupata katika mafanikio ya mali.[2]





Mwenyezi Mungu amesema kwenye Kurani:





"Hakika wale walio kufuru, na wakafa hali ni makafiri haitakubaliwa kutoka kwa yeyote wao fidia ya dhahabu ya kujaza dunia nzima lau wangeli itoa. Hao watapata adhabu chungu, wala hawatakuwa na wa kuwanusuru." (Kurani 3:91)





Kwa hivyo, maisha haya ndiyo nafasi yetu ya pekee ya kupata Pepo na kuepukana na Moto wa Jahannamu, kwa sababu mtu akifa akiwa hajaamini, hatakuwa na nafasi nyingine ya kurejea katika ulimwengu huu ili aweze kuamini.  Kama Mwenyezi Mungu alivyosema katika Kurani kuhusu yatakayowapata wasioamini Siku ya Hukumu:





"Na unge ona watakapo simamishwa kwenye Moto, wakawa wanasema: Laiti tungeli rudishwa, wala hatutakanusha tena Ishara za Mola wetu Mlezi, na tutakuwa miongoni wa Waumini!" (Kurani 6:27)





Lakini hakuna mtu atakaye pata nafasi hii ya pili.





Amesema Mtume Muhammad,rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Mtu mwenye furaha kuliko wote duniani miongoni mwa wale waliohukumiwa Motoni Siku ya Kiyama atatumbukizwa Motoni mara moja. Kisha ataulizwa, ‘Mwana wa Adamu, je! umewahi kuona kheri yoyote? Umeshawahi kuona baraka yoyote?'  Kisha atasema 'Hapana, kutoka kwa Mungu, Eee Mola!'"[1]





Mwenyezi Mungu amesema katika Kurani:





“Na wabashirie walio amini na wakatenda mema kwamba watapata mabustani yapitayo mito kati yake....” (Kurani 2:25)





Mungu pia amesema:





“Kimbilieni msamaha wa Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, iliyo wekewa walio muamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake....” (Kurani 57:21)





Mtume Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, ametuambia kuwa aliye chini kabisa katika daraja miongoni mwa watu wa Peponi atakuwa na mara kumi ya dunia hii,[1]  na atapata chochote atakacho tamani na mara kumi kama hiyo.[2]  Pia, Mtume Muhammad amesema: “Nafasi katika Pepo inayolingana na ukubwa wa mguu ingekuwa bora kuliko dunia na vilivyomo ndani yake.”[3]  Pia alisema: “ huko Peponi kuna vitu ambavyo jicho halijawahi kuona, hakuna sikio lililosikia, na hakuna akili ya mwanadamu iliyo fikiria.”[4]  Pia alisema: “Mtu mwenye huzuni zaidi katika ulimwengu wa wale walio kusudiwa kwa ajili ya Pepo atatumbukizwa mara moja katika Pepo. Kisha ataulizwa, ‘Mwana wa Adamu, je! uliwahi kupata taabu yoyote? Je! umewahi kupatwa na magumu yoyote?’ Kwa hiyo atasema, ‘Hapana, Wallahi, Ee Mola! Sikuwahi kukumbana na taabu yoyote, na sikupata shida yoyote.’”[5]





Ukiingia Peponi, utaishi maisha ya furaha sana bila magonjwa, maumivu, huzuni, au kifo; Mungu atakuwa atapendezwa nawe; nawe utaishi huko milele. Mwenyezi Mungu amesema katika Kurani:





“Na wale walio amini na wakatenda mema tutawaingiza katika Pepo zipitazo mito kati yake kwa kudumu humo milele....” (Kurani 4:57)



Machapisho ya hivi karibuni

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL

Masuala kumi muhimu n ...

Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Muharram

UJUMBE KWA ALIYEICHOM ...

UJUMBE KWA ALIYEICHOMA KURANI