Nakala

Kupumua, kula, kutembea, nk, ni kazi za asili za kibinadamu. Lakini watu wengi hawafikirii kuhusu jinsi vitendo hivi vya kimsingi vinavyotokea. Kwa mfano, unapokula matunda, huwa hutafakari kuhusu jinsi itakavyofanya kuufaidi mwili wako. Kitu pekee kwenye akili yako ni kula chakula cha kuridhisha; wakati huo huo, mwili wako umo katika michakato ya kina sana, usiyoifahamu ili  kukifanya chakula hiki kiwe chanzo cha afya.





Mfumo wa umeng'enyaji ambapo taratibu hizi za kina hufanyika huanza kufanya kazi pindi tu kipande cha chakula kinapowekwa kinywani. Huku ikishiriki katika mfumo tangu mwanzoni, mate hufanya chakula kiwe majimaji na hukisaidia kutafunwa na meno na kushuka  chini kwa umio.





Umio husafirisha chakula hadi kwa tumbo ambapo usawa kamili wa ajabu unafanya kazi. Hapa, asidi haidrokloriki iliyopo ndani ya tumbo humeng'enya chakula. Asidi hii ina nguvu sana hadi ina uwezo wa kumeng'enya sio chakula tu bali pia kuta za tumbo. Bila shaka, kasoro kama hiyo hairuhusiwi katika mfumo huu kamili. Kipengele kinachoitwa kamasi, ambacho hutolewa wakati wa umeng'enyaji, kinafunika kuta zote za tumbo na hupeana ulinzi kamili dhidi ya athari za uharibifu wa asidi ya hidrokloriki. Hivyo tumbo huzuiliwa kujimeng'enya yenyewe.





Jambo ambalo linastahili kuzingatiwa hapa ni kwamba mageuzi hayawezi kuelezea mfumo uliotajwa kwa ufupi hapo juu. Mageuzi yanaeleza kuwa viumbe tata vya leo vimebadilika kutoka kwa aina za seli za asili na mkusanyiko wa taratibu za mabadiliko madogo ya kimuundo. Hata hivyo, kama ilivyoelezwa wazi, mfumo ndani ya tumbo haukuweza kuundwa hatua kwa hatua. Kutokuwepo kwa kipengele hata kimoja kungeleta kifo cha kiumbe hicho.





Chakula kinapo pokelewa ndani ya tumbo, uwezo wa juisi za tumbo kuvunja chakula hufanyika kutokana na mfululizo wa mabadiliko ya kemikali. Sasa, tafaari kuhusu kiumbe katika mchakato wa mageuzi ambaye katika mwili wake mabadiliko ya kemikali yaliyotajwa hayajakamilika. Kiumbe huyu, kwa kutoweza kuendeleza uwezo huu kivyake, hataweza kumeng'enya chakula alicho kila na angekufa na njaa kutokana na uwepo wa chakula kisicho meng'enyeka ndani ya tumbo lake.





Aidha, wakati wa kutolewa kwa asidi hii, kuta za tumbo wakati huo huo zinapaswa kuzalisha  kamasi. Vinginevyo, asidi ndani ya tumbo ingeharibu tumbo. Kwa hivyo, ili uhai uendelee, tumbo lazima litoe mawili haya yote (asidi na kamasi) kwa wakati mmoja. Hii inaonyesha kuwa sio mageuzi ya hatua kwa hatua ambayo yamekuwa yakifanya kazi, bali ni uumbaji wa ufahamu na mifumo yake yote iliyoshikana.





Yote haya yanaonyesha ya kwamba mwili wa mwanadamu unafanana na kiwanda kikubwa kilichoundwa na mashine nyingi ndogo zinazofanya kazi pamoja kwa maelewano na ukamilifu. Kama vile viwanda vyote vina mtengenezaji, mhandisi na mpangaji, mwili wa mwanadamu una “Muumba Aliyetukuka.”



Machapisho ya hivi karibuni

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL

Masuala kumi muhimu n ...

Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Muharram

UJUMBE KWA ALIYEICHOM ...

UJUMBE KWA ALIYEICHOMA KURANI