DINI YA KWELI YA MWENYEZI MUNGU NI IPI?
ila mtu huzaliwa katika mazingira au hali ambayo si chaguo
lake mwenyewe. Hupachikwa dini ya familia yake au
mtazamo wa taifa lake toka mwanzoni mwa kuwepo kwake
katika dunia hii. Wakati anapofikia ujana wa (miaka 13 – 20), kwa
kawaida hulazimika kuamini kwamba imani ya jamii yake ndiyo
imani sahihi ambayo kila mtu anapaswa kuwa nayo. Ingawa wakati
fulani baadhi ya watu wanapokuwa wakubwa na wakaona imani
nyingine huanza kuuliza na kuhoji ukweli wa imani yao. Wale
wanaotafuta ukweli mara kwa mara hufikia mahali
wakachanganyikiwa wanapogundua kwamba kila dini, dhehebu, au
falsafa hudai ndio njia pekee iliyo sahihi kwa mwanadamu, kwani
makundi yote hayo yanahamasisha watu kufanya matendo mema.
Sasa ni ipi imani sahihi? Zote haziwezi kuwa sahihi, kwani kila moja
hudai kuwa nyingine zote si sahihi. Sasa katika hali hiyo, yule
anayetafuta ukweli vipi ataweza kuchagua njia iliyosahihi?
Mwenyezi Mungu ametupa sote akili na uwezo wa kutuwezesha
kufanya maamuzi sahihi na ya maana. Nayo ni maamuzi muhimu sana
katika maisha ya mwanadamu. Mustakabali wake unautegemea uamuzi huo,
kufuatana na hilo, kila mmoja wetu lazima achunguze ushahidi
uliotolewa bila kupendelea ndipo achague kile kinachoonekana kuwa
ni sahihi mpaka pale ushahidi mwingine utakapotokea.
Kama ilivyo kwa kila dini au falsafa, Uislamu nao unadai kuwa huo
ndio njia ya pekee iliyo sahihi kuelekea kwa Mwenyezi Mungu.
Katika hali hiyo ya Uislamu kudai kuwa ni njia sahihi si tofauti na
mifumo mingine. Kijitabu hiki kinakusudia kukupa ushahidi juu ya
ukweli wa dai hilo. Hata hivyo, mara zote ni lazima izingatiwe
kwamba, mtu anaweza kuipata njia ya kweli kwa kuweka kando hisia
na chuki, vitu ambavyo mara kwa mara hutupofua tusiuone ukweli.
Kisha, baada ya kufanya hivyo tu, ndipo tutakapoweza kutumia akili
zetu tulizopewa na Mwenyezi Mungu kufanya maamuzi ya kiakili na
yaliyo sahihi?
Kuna hoja mbali mbali ambazo zinaweza kutolewa ili kulipa nguvu
dai la Kiislamu kuwa ndio dini ya kweli ya Mwenyezi Mungu.
K
3
Zifuatazo ni hoja tatu zilizo wazi sana. Ya kwanza inaegemea juu ya
ukweli wa asili ya majina ya dini na upana wa maana zake. Hoja ya
pili inahusiana na mafundisho ya kipekee na yasiyotatanisha
yanayoonyesha uhusiano kati ya Mwenyezi Mungu, mwanadamu na
uumbaji. Hoja ya tatu inatokana na ukweli kwamba Uislamu ni dini ya
dunia nzima kwa watu wote na kwa nyakati zote. Hizi ndizo hoja tatu
za msingi ambazo kimantiki na kiakili zinalazimu ziwepo kwa dini
yeyote ile ili izingatiwe kuwa ni dini ya kweli ya Mwenyezi Mungu.
Kurasa zifuatazo zitaufafanua ufahamu huo kikamilifu.
4
JINA LA DINI
itu cha kwanza kabisa ambacho mtu anapaswa kukijua na
kukifahamu kwa kina kuhusu Uislamu ni juu ya maana ya
neno lenyewe “Uislamu.” Neno hilo ni la asili ya Kiarabu
lenye maana ya kutii au kusalimisha matakwa ya mtu kwa Mwenyezi
Mungu wa kweli wa pekee, ajulikanaye kwa Kiarabu kama “Allah”.
Mtu ambaye amesalimisha matakwa yake kwa Mwenyezi Mungu
(Allah) huuitwa “Mwislamu”. Dini ya Kiislamu haikupewa jina
kutokana na jina mtu au watu, wala halikuamuliwa na kizazi chochote
cha wanadamu kama vile Ukristo ambao ulipewa jina kutokana na
“Yesu Kristo”, Ubudha unatokana na jina la Gautama Buddha,
Kunfushian, unatokana na Confucius, Umaksi ulipewa jina la Karl
Marx; Uyahudi unatokana na jina la kabila la Yuda na Ubaniani
(Uhindu) unatokana na jina la Hindu. Uislamu (kutii amri za Mwenyezi
Mungu) ni dini aliyopewa Adam, mtu wa kwanza na mtume wa
kwanza wa Mwenyezi Mungu, na Uislamu ndio dini ya mitume wote
waliotumwa na Mwenyezi Mungu kwa wanadamu. Kwa kuongezea,
jina la Uislamu lilichaguliwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe na
limetajwa wazi wazi katika kitabu cha mwisho cha Allah (Quran).
Allah alimfunulia mwanadamu katika kitabu cha mwisho
alichomfunulia Mwanadamu. Katika ufunuo wa mwisho, uitwao kwa
Kiarabu Al-Quran Allah ameeleza yafuatayo:-
“… Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na kukutimizieni neema
Yangu, na Nimekupendeleeni Uislamu uwe Dini yenu…” [Quran 5:3]
“Na anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitakubaliwa
kwake…” [Quran 3:83]
Kwa hiyo, Uislamu haudai kuwa ni dini mpya iliyoletwa Arabuni na
Mtume Muhammad katika karne ya saba, lakini Uislamu ni
mwendelezo wa sehemu ya mwisho ya dini ya Allah, kama
ilivyofunuliwa toka mwanzo kwa Adam na mitume waliomfuatia.
Hadi kufikia hapa tutatoa maoni kwa ufupi kuhusu dini nyingine mbili
zinazodai kwamba ndizo njia sahihi. Hakuna sehemu yoyote katika
Biblia ambayo utakuta kwamba Mwenyezi Mungu amewafunulia
K
5
watu wa Mtume Musa au vizazi vyao kwamba dini yao inaitwa
Uyahudi, au kwa wafuasi wa Kristo kuwa dini yao inaitwa Ukristo.
Kwa maneno mengine, majina “Uyahudi" na "Ukristo” hayakutokana
na asili ya Mwenyezi Mungu wala hayani idhini yake. Jina Ukristo
halikuwepo hadi muda mrefu baada ya kuondoka Yesu ndipo jina hilo
lilipotolewa kwa dini ya Yesu.
Sasa nini lililokuwa jina la kweli hasa, la dini ya Yesu, ambalo
linajipambanua na jina lake? (Majina yote mawili Yesu na Kristo
yanatokana na maneno ya Kiebrania, kupitia Kigiriki na Kilatini.
Jesus ni Kingereza na kwa Kilatini cha Kigiriki ni Iesous, ambalo kwa
Kiebrania ni Yeshua au Yehoshua' (Joshua). Neno la Kigiriki Christos
ni tafsiri ya Kiebrania kwa neno “Messiah”, jina la heshima
linalomaanisha “Mpakwa mafuta.” Dini yake inaakisi mafundisho
yake, ambayo aliwaamrisha wafuasi wake kuyakubali kama misingi
ya kuwaongoza katika uhusiano wao na Mwenyezi Mungu. Katika
Uislamu, Yesu ni mtume aliyeletwa na Allah na jina lake la Kiarabu
ni Issa. Kama ilivyo kwa mitume ya kabla yake, yeye naye
aliwalingania watu wasalimishe matakwa yao kwa matakwa ya
Mwenyezi Mungu (jambo ambalo ndilo linalosimamiwa na Uislamu).
Kwa mfano katika Agano Jipya inasemekana kwamba Yesu
aliwafundisha wafuasi wake kusali kwa Mwenyezi Mungu kama
ifuatavyo:-
“Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje,
[Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.] (Luka
11:2/Mathayo 6:9).
Wazo hili lilisisitizwa sana na Yesu katika maelezo yake mengi
yaliyoandikwa katika Biblia. Kwa mfano, amefundisha kuwa,
waliojisalimisha kwa Mwenyezi Mungu, hao peke yao ndio
watakaopata uzima wa milele. (Peponi).
Yesu pia alifafanua kwamba yeye mwenyewe amejisalimisha kwa
matakwa ya Mwenyezi Mungu.
6
“Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme
wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye
mbinguni.” (Mathayo 7:21).
“Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo
nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti
mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.” (Yohana
5:30).
Kuna maelezo mengi katika Biblia yanayoonesha kwamba Yesu
aliweka wazi kwa wafuasi wake kwamba yeye siye Mungu.
Kwa mfano, aliposema kuhusu saa ya mwisho alisema:
“Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika
walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba. (Marko 13:-32).
Kwa hiyo, Yesu kama walivyokuwa Mitume waliopita kabla yake na
yule aliyekuja baada yake, alifundisha dini ya Kiislamu:
kujisalimisha kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu mmoja aliye wa
kweli.
7
MWENYEZI MUNGU NA UUMBAJI
wa vile jambo la mtu kujisalimisha kikamilifu kwa Mwenyezi
Mungu linamaanisha kiini cha kuabudu, ujumbe wa msingi
wa dini ya Mwenyezi Mungu, Uislamu ni kumwabudu
Mwenyezi Mungu peke yake. Vilevile Uislamu unawataka watu
waachane na kuabudu binadamu, eneo au kitu zaidi ya Mwenyezi
Mungu. Kwa vile vitu vyote ukimtoa Mwenyezi Mungu muumbaji wa
vitu vyote, ni uumbaji wa Mwenyezi Mungu; inawezekana kusemwa
kwamba Uislamu kimsingi unamlingania mtu aache kuabudu viumbe
na kumwita amwabudu muumbaji wake pekee. Yeye ndiye pekee
anayestahiki kuabudiwa na watu, kwa sababu ni kwa matakwa yake
yeye tu ndipo maombi yote hujibiwa.
Kutokana na hilo, endapo mwanadamu atauomba mti na maombi yake
kujibiwa, basi akumbuke kwamba si mti uliojibu maombi yake bali ni
Mwenyezi Mungu, ndiye aliyeruhusu maombi hayo yawe kama
alivyoomba. Mtu anaweza kusema, “jambo hilo lipowazi”. Hata
hivyo, kwa wale wanaoabudu miti, inawezekana isiwe hivyo. Vivyo
hivyo, wale wanaomwabudu Yesu, Budha, au Krishna au mtakatifu
Kristofa, au mtakatifu Jude au hata Muhammad, maombi yao
hayajibiwi na hao, bali yanajibiwa na Mwenyezi Mungu. Yesu
hakuwaambia wafuasi wake wamwabudu yeye bali aliwaambia
wamwabudu Mwenyezi Mungu, kama inavyoeleza Quran:
"Na (kumbukeni) Mwenyezi Mungu atakaposema: "Ewe Isa bin
Maryamu! Je, wewe uliwaambia watu: 'Nifanyeni mimi na mama
yangu kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu'?" Aseme (Nabii
Isa): "Wewe umetakasika na kuwa na mshirika. Hainijuzii mimi
kusema ambayo si haki yangu (kuyasema, kwa kuwa ni ya uwongo).
(Quran 5:116)
Yesu hajajiabudu yeye mwenyewe alipokuwa anaabudu, lakini
alimwabudu Mwenyezi Mungu. Yesu amenukuliwa ndani ya Biblia
akisema,
“…Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye
peke yake.” (Luka 4:8).
K
8
Kanuni hii ya msingi ipo katika sura ya kwanza katika Quran
ijulikanayo kama Suratul-Fatiha, aya ya nne
“Wewe tu ndiye tunayekuabudu, na Wewe tu ndiye tunayekuomba
msaada.” (Quran 1:5)
Na katika sehemu nyingine ndani ya Kitabu cha ufunuo wa mwisho,
ambacho ni Quran, pia Mwenyezi Mungu amesema:
“Na Mola wenu Anasema: “Niombeni Nitakujibuni.” (Quran 4:60)
Ni muhimu mno kusisitiza kwamba msingi wa ujumbe wa Uislamu
(umetaja kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake) pia umetangaza
kwamba Mwenyezi Mungu na viumbe vyake ni tofauti kabisa.
Mwenyezi Mungu hayuko sawa na viumbe vyake wala si sehemu ya
viumbe vyake, na wala viumbe vyake si sawa Naye na wala si sehemu
ya Uungu.
Hili lawezekana kuonekana ni jambo lililowazi, lakini kitendo cha
mwanadamu kuabudu viumbe, badala ya Muumba kwa kiasi kikubwa
Kinatokana na ujinga au kupuuza, ufahamu huu. Ni imani ya baadhi
ya watu kwamba kuwepo kwa Mwenyezi Mungu kupo kila mahala
katika viumbe vyake au kuwepo kwa uungu wake kupo au
kulikuwepo katika baadhi ya sehemu za viumbe vyake, jambo
lilowahalalishia waabudu viumbe vya Mwenyezi Mungu na kusema
kuwa wanamwabudu Mungu. Hata hivyo, ujumbe wa Uislamu kama
ulivyoletwa na Mitume ya Mwenyezi Mungu, ni kumwabudu
Mwenyezi Mungu peke yake na kuacha kuabudu viumbe vyake kwa
moja kwa moja au kwa kutumia njia yoyote ile.
Katika Quran Mwenyezi Mungu amesema wazi wazi:
“Na bila shaka Tulimpeleka Mtume katika kila umma ya kwamba:
“Muabuduni Mwenyezi Mungu na mwepukeni (Iblisi) muovu.”
(Quran 16:36)
Wakati wale wanaoabudia masanamu wanapoulizwa; kwa nini
wanaabudu masanamu yaliyotengeneza na Wanadamu? Jibu la siku
9
zote ni kuwa; kwa hakika wao hawaiabudu ile picha ya jiwe bali
wanaabudia Mwenyezi Mungu aliyopo katika masanamu hayo.
Wanadai kwamba masanamu hayo ni sehemu za kumuelekea
Mwenyezi Mungu tu na si Mwenyezi Mungu mwenyewe! Mtu
aliyekubali wazo la kuwa Mwenyezi Mungu kwa namna yoyote ile
yupo ndani ya viumbe vyake atalazimika kukubali hoja hii ya kuabudu
masanamu. Wakati, mtu aliyeufahamu vizuri msingi wa ujumbe wa
Uislamu na utekelezwaji wake kamwe hawezi kukubali kuabudia
masanamu hata kama kutajengewa hoja za kimantiki.
Wale waliodai ungu tangu zamani mara kwa mara wameelekeza
madai yao katika imani potofu ya kwamba Mwenyezi Mungu yu
katika mwanadamu. Tukienda hatua moja mbele, wanadai kuwa
Mwenyezi Mungu yu pamoja nao kuliko alivyo kwetu sisi tuliobakia,
kwa hiyo, wanadamu wanapaswa kunyenyekea kwao na kuwaabudu
wao kama vile Mwenyezi Mungu aliye katika mwanadamu au
Mwenyezi Mungu aliejiingiza kwa wanadamu. Vilevile wale
wanaotangaza uungu wa watu wengine baada ya kufa kwao wamepata
ardhi yenye rutba miongoni mwa wale wanaoamini imani potofu ya
kuwa Mwenyezi Mungu yupo ndani ya mwanadamu.
Hadi sasa hivi, lazima iwe wazi kabisa kwamba mtu aliyeelewa
msingi wa ujumbe wa Uislamu na vidokezo vyake kamwe hawezi
kukubali kumwabudu mwadamu mwenzake katika hali yoyote ile.
Dini ya Mwenyezi Mungu, kwa asili, ni wito uliowazi wa kumwabudu
Muumba na kukataa kuabudu viumbe kwa namna yoyote ile. Na hii
ndio maana ya wito wa Uislamu.
"Laa Ilaha Ill Allah" (Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila
Allah).
Kutamka kwa dhati ibara hii na kumkubali Mtume, moja kwa moja
kunampelekea mtu kuwa katika Uislamu, na imani ya dhati kwa
tamko hilo humuhakikishia mtu kuingia Peponi. Kwa hiyo, Mtume wa
mwisho wa Uislamu (S.A.W) amenukuliwa akisema kuwa, “Yeyote
asemaye: Hakuna Mungu wa haki ispokuwa Allah, na akafa akiwa na
imani hiyo ataingia Peponi.”
10
Imani juu ya tamko hili la kiitikadi inamtaka mtu kusalimisha
matakwa yake kwa Mwenyezi Mungu kwa namna zilizofundishwa na
Mitume ya Mwenyezi Mungu. Vilevile tamko hilo linamtaka muumini
aache kuabudu miungu ya uongo.
11
UJUMBE WA DINI ZA UWONGO
una madhehebu, makundi ya kidini, dini, falsafa, na harakati
nyingi duniani, yote hayo yanadai kuwa ndio njia sahihi au
ndio njia ya pekee ya Mwenyezi Mungu. Sasa vipi mtu
ataweza kugundua ni kundi lipi lililosahihi au kama yote ni sahihi?
Njia moja ya kupata jibu la swali hilo ni kuondoa tofauti za kijuu juu,
katika mafundisho ya wadai mbali mbali ili kuufikia ukweli, na
kutambua kitu kikuu kinachoabudiwa na kitu hicho ndicho hasa
wanachokilingania, moja kwa moja au sio moja kwa moja. Dini za
uongo zote, kikawaida, zina hoja moja maarufu iliyo ya msingi juu ya
Mwenyezi Mungu, aidha wanadai wanaume wote ni miungu, au
wanaume fulani tu ndiyo miungu au maumbile (nature) ndiyo
Mwenyezi Mungu au Mwenyezi Mungu ni kitu kilichopo tu katika
dhana za watu.
Kwa hiyo, kuna uwezekano wa kusema kwamba, msingi wa ujumbe
wa dini za uongo ni kwamba Mwenyezi Mungu anaweza kuabudiwa
kwa mfumo wa umbaji wake. Dini za uongo huwaita watu waabudu
viumbe vya Mwenyezi Mungu kwa kuviita viumbe hivyo au sehemu
ya viumbe hivyo ni Mwenyezi Mungu. Kwa mfano, Nabii Issa (Yesu)
aliwaita, wafuasi wake wamwabudu Mwenyezi Mungu, lakini wale
wanaodai kuwa wao ni wafuasi wa Yesu leo hii wanawalingania watu
wamwabudu Issa (Yesu), wakidai kwamba yeye ni Mwenyezi Mungu.
Budha alikuwa mrekebishaji ambaye alianzisha kanuni mbali mbali za
kibinadamu katika dini ya Kihindu. Hakudai kuwa yeye ndiye Mungu
mwenyewe, wala hakupendekeza kwa wafuasi wake kwamba yeye
awe wa kuabudiwa. Leo hii, Mabudha wengi mno walio nje ya India
wanamfanya yeye (Budha) kuwa ni Mwenyezi Mungu na wanasujudia
masanamu yaliyotengenezwa kwa sura yake.
Kwa kutumia msingi wa kutambua kitu kinachoabudiwa, tunaweza
kuzigundua kwa urahisi dini za uongo na asili ya vyanzo vyake.
Kama Mwenyezi Mungu alivyosema katika Quran:
K
12
“Hamuabudu badala yake (Mwenyezi Mungu ila majina (matupu)
mliyoyapanga nyinyi wenyewe na baba zenu (mkayaita hayo
masanamu). Mwenyezi Mungu hakuteremsha dalili kwa hayo.
Haikuwa hukumu ila hii ya Mwenyezi Mungu tu; Ameamrisha
msimuabudu yoyote ispokuwa Yeye tu. Hiyo ni Dini madhubuti,
lakini watu wengi hawajui”. (Quran 12:40)
Watu wanaweza kutoa hoja kwamba dini zote zinafundisha mema,
kwa hiyo, kuna haja gani ya kujali kuifuata dini mojawapo? Jibu ni
kwamba dini za uwongo zote zinafundisha dhambi kubwa sana ya
kuabudu viumbe. Kuabudu viumbe ni dhambi kubwa kabisa awezayo
kuifanya mwanadamu kwa sababu tendo hilo linapingana na lengo la
kuumbwa kwake.
Mwanadamu ameumbwa ili kumwabudu Mwenyezi Mungu tu kama
Allah alivyosema katika Quran:
“Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu”. (Quran 51:56)
Matokeo yake, kuabudu viumbe; jambo ambalo ni asili ya kuabudu
masanamu ni dhambi pekee isiyosameheka. Mtu atakayekufa katika
hali hiyo ya kuabudu masanamu, ameshaangamiza majaaliwa yake ya
ahera. Hii si rai ya mtu, bali ni ufunuo wa kweli ulioelezwa na
Mwenyezi Mungu katika ufunuo wake wa mwisho kwa wanadamu:
“Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa; na Husamehe
yasiyokuwa haya kwa amtakaye. (4:48 na 116)
13
DINI YA MWENYEZI MUNGU NI YA ULIMWENGU MZIMA
wa vile matokeo ya kufuata dini ya uwongo ni hatari sana,
dini ya kweli ya Mwenyezi Mungu ni lazima ifahamike dunia
nzima, iwe imepatikana dunia nzima wakati uliopita na
lazima idumu milele na iwe inafahamika milele na ipatikane dunia
zima. Kwa maneno mengine, dini ya kweli ya Mwenyezi Mungu
haiwezi kuwa na mipaka kwa watu fulani tu, eneo, au kipindi fulani
tu. Wala si jambo la kimantiki kwamba dini kama hiyo iamuru
mazingira yasiyo na maana yoyote katika uhusiano kati ya
mwanadamu na Mwenyezi Mungu kama vile, kubatiza, au imani
kwamba mwanadamu ni mwokozi, au ni mpatanishi. Katika kanuni
kuu ya Uislamu na ambayo maana yake ni (kusalimisha matakwa ya
mtu kwa Mwenyezi Mungu) ndipo inapopatikana mizizi ya Uislamu
kuwa wa dunia nzima. Wakati wowote mwanadamu anapotambua
kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja na ametofautiana na viumbe vyake,
na mtu huyo akajisalimisha kwa Mwenyezi Mungu, Mtu huyo
anakuwa Mwislamu kimwili na kiroho na anastahiki Pepo.
Kwa hiyo, mtu yoyote katika muda wowote hata yule aishiye maeneo
ya mbali anaweza kuwa Mwislamu, mfuasi wa dini ya Mwenyezi
Mungu, Uislamu, kwa kukataa moja kwa moja kuabudu viumbe na
kuamua kumgeukia Mwenyezi Mungu peke yake.
Ni lazima ikumbukwe, hata hivyo, ili kujisalimisha kwa matakwa ya
Mwenyezi Mungu kikweli kweli, mtu ni lazima achague baina ya haki
na batili. Kwa hakika, binadamu amejaaliwa uwezo na Mwenyezi
Mungu sio tu wa kutofautisha kati ya wema na uwovu bali vilevile
kuchagua kati ya vitu viwili hivyo.
Huu uwezo wa kupewa na Mwenyezi Mungu unabeba majukumu
muhimu sana, nayo ni kuwa, mwanadamu atajibu kwa Mwenyezi
Mungu juu ya chaguo alilolichagua. Kinachofuata mwanadamu
anapaswa ajaribu kwa kutumia uwezo wake wote afanye mema na
aache maovu.
Ufahamu huu umeelezwa katika ufunuo wa mwisho kama ifuatavyo:
K
14
“Katika walioamini (Mitume ya zamani huko) na Mayahudi na
Wakristo na Wasabai; yoyote (miongoni mwao) atakayemwamini
Mwenyezi Mungu (sasa kama anavyosema Nabii Muhammad) na
akaamini Siku ya Mwisho na akafanya vitendo vizuri, basi watapata
thawabu zao kwa Mola wao, wala haitakuwa khofu juu yao, wala
hawatahuzunika. (Quran 2:62)
Ikiwa kwa sababu yoyote ile, wanadamu watashindwa kuukubali
ujumbe wa mwisho baada ya kuelezwa bayana, watakuwa katika
hatari kubwa mno. Mtume wa mwisho amesema:
"Yoyote miongoni mwa Wakristo na Wayahudi atakayesikia habari
zangu na akaendelea na imani ya kukakanusha kile nilichokuja nacho
na akafa katika hali hiyo atakuwa ni miongoni mwa wakazi wa
Motoni."
(Sahih Muslim [English Translation], Vol.1 p.91 N0, 284)
15
KUMTAMBUA MWENYEZI MUNGU.
wali linalojitokeza hapa ni: vipi itarajiwe kuwa watu wote
watamwamini Mwenyezi Mungu mmoja wa kweli, ukizingatia
watu hao wana asili za jamii na tamaduni tofauti tofauti? Ili
watu wawajibike kwa kumwabudu Mwenyezi Mungu mmoja wa
kweli, wanahitaji wapate elimu ya kumtambua Mwenyezi Mungu.
Ufunuo wa mwisho unafundisha kwamba wanadamu wote wana athari
ya kumtambua Mungu mmoja wa kweli athari ambayo iliwekwa
katika nafsi zao ikiwa ni kama sehemu ya asili yao waliyoumbiwa
nayo.
Katika sura ya saba ya Quran (Al-Aaraf, aya ya 172 – 173), Mwenyezi
Mungu ameeleza kwamba wakati alipomuumba Adam alijaalia kizazi
cha Adam kuwepo ulimwenguni na Mwenyezi Mungu akuchukua
ahadi toka kwao na kuwaambia: “Je, Mimi siye Mola wenu?"
Wakasema: “Ndiye; tunashuhudia (kuwa Wewe ndiye Mola wetu)."
Kisha Allah akaeleza sabababu za kuwalazimisha wanadamu wote
wakiri kwamba yeye ndiyo muumba wao na ndiye Mwenyezi Mungu
wa kweli wa pekee anayestahiki kuabudiwa. Amesema:
“Msije mkasema Siku ya Kiyama kuwa sisi tulikuwa tumeghafilika na
hayo (hatuyajui). (Quran 7:172)
Hii inamaanisha kwamba, hatuwezi kudai katika siku hiyo kwamba
tulikuwa hatujui kuwa Allah ndiye Mungu wetu na kwamba hakuna
mtu aliyetwambia kwamba tulipaswa kumwabudu Allah peke yake.
Allah akaendelea kuelezea kuwa:
“Au mkasema, Baba zetu ndio walioshirikisha zamani, nasi tulikuwa
kizazi nyuma yao, basi Utatuangamiza kwa sababu ya yale
waliyoyafanya waovu?” (Hamuwezi kusema haya kwani nyote
Tumekufahamisheni, nyinyi na wao). (Quran 7:173).
S
16
Kwa hiyo, kila mtoto huzaliwa na imani ya kumtambua Mwenyezi
Mungu na mwelekeo wa kumwabudu Mwenyezi Mungu pekee. Imani
hii ya kuzaliwa nayo na mwelekeo huo huitwa kwa Kiarabu “Fitrah”.
Mtume Muhammad (S.A.W) ameeleza kwamba Allah amesema,
“Niliwaumba waja wangu katika dini sahihi, lakini shetani
aliwapoteza.” Vilevile Mtume amesema, “Kila mtoto huzaliwa katika
Fitrah. Kisha wazazi wake wanamfanya aidha awe Myahudi, Mkristo
au Mmajusi (waabudio moto).’’ Ikiwa mtoto ataachwa peke yake,
atamwabudu Mwenyezi Mungu kwa namna yake mwenyewe, lakini
watoto wote huathiriwa na mazingira. Kwa hiyo, ni kama vile mtoto
anatii sheria za kimaumbile, ambazo Allah ameziamrisha kimaumbile,
katika hali hiyo hiyo nafsi yake pia inatii maumbile ya kuwa Allah ni
Mola na Muumba wake. Lakini, ikiwa wazazi wake watajaribu
kumfanya afuate njia tofauti, mtoto anakuwa hana nguvu za kutosha,
hasa hasa katika hatua zake za mwanzo za maisha yake, za kuzuia na
kupinga matakwa ya wazazi wake.
Katka hali kama hizo, dini ambayo mtoto anaifuata, ni tamaduni na
malezi, na Mwenyezi Mungu hamuhesabu wala hamuadhibu kwa dini
hiyo mpaka atakapofikia umri fulani maishani mwake. (baleghe).
17
DALILI ZA MWENYEZI MUNGU.
atika hatua zote za maisha ya wanadamu, kutoka utoto hadi
kufikia kufariki, dalili za Mwenyezi Mungu mmoja wa kweli
zinaonyeshwa kwao katika pande zote za dunia na katika
nafsi zao mpaka inapowabainikia kwamba kuna Mwenyezi Mungu
mmoja tu wa kweli (Allah). Mwenyezi Mungu amesema katika
Quran:
“Tutawaonyesha (ukweli wa) Maneno Yetu haya katika nchi za mbali
na katika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie kwamba haya ni
kweli…” (Quran: 41:53)
Ufuatao ni mfano wa ufunuo wa Mwenyezi Mungu kwa dalili ya kosa
la mtu mmoja la kuabudu sanamu. Katika maeneo ya kusini mashariki
mwa msitu wa Amazoni huko Brazili, Amerika ya Kusini watu wa
kabila la wasiostaarabika walijenga kibanda kipya ili kuhifadhi
sanamu la mtu liitwalo Skwatch, likiwa ni Mungu mkuu wa viumbe
vyote.
Siku iliyofuatia kijana mmoja aliingia kibandani kutoa heshima kwa
Mungu huyo, na alipokuwa ameinama (kukisujudia) kile alichofunzwa
kuwa ndicho Muumba na Mpaji wake, ghafla mbwa mkondefu
mwenye viroboto na mafunza aliingia pole pole mule kibandani. Yule
kijana aliinua kichwa chake kwa kitambo kidogo akamtazama yule
mbwa, akiinua mguu wake wa nyuma na kulikojolea lile sanamu.
Yule kijana alimfukuza yule mbwa nje ya kile kibanda kikatili, lakini
mara tu ghadhabu zake zilipoisha alitambua kwamba lile sanamu
kamwe haliwezi kuwa Mola wa Ulimwengu wote. Mwenyezi Mungu,
lazima atakuwa yupo sehemu nyingine, alihitimisha. Ni jambo la
kushangaza kama linavyoweza kuonekana, mbwa kulikojolea lile
sanamu ilikuwa ni alama kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa kijana
huyo. Alama hii imebeba ujumbe mtakatifu kwa kuwa kile
alichokuwa akikiabudu kilikuwa cha uwongo. Huo ni ukombozi
kutoka utumwa wa kufuata mafundisho ya utamaduni wa kuabudu
mungu wa uongo. Matokeo yake, mtu huyu amehiyarishwa: aidha
K
18
amtafute Mwenyezi Mungu wa kweli au aendelee katika njia yake ya
makosa.
Allah (S.W) anataja utafutaji wa kumtafuta Mwenyezi Mungu
unaomuhusu Mtume Ibrahimu kuwa ni mfano wa jinsi ya wale wote
wanaofuata dalili zake wataongozwa katika njia sahihi.
“Na namna hivi Tulimwonyesha Ibrahimu ufalme wa mbingu na ardhi
(kuwa ni wa Mungu), na ili awe miongoni mwa wenye yakini. Na
usiku ulipomwingilia (Ibrahimu na hali kakaa na makafiri), akaona
nyota, alinena (makusudi kutaka kuwavuta watumie fikra zao):
“(Nyota) hii ni Mola wangu.” Ilipotua (ikapotea), alisema (kuwaambia
wale makafiri kama kwamba yu pamoja nao katika ibada ile):
“Sipendi waola wanaopotea (hawawepo ila wakati makhsusi tu).” Na
(usiku wa pili) alipouona mwezi unachomoza alisema (kuwaambia
wale marafiki zake wa kikafiri): “Huu (mwezi) ndio Mola wangu.”
Ulipotua alisema: “Asiponiongoza Mola wangu, bila shaka nitakuwa
miongoni mwa watu wapotofu. (Na mola huyu hawezi kuniongoza
kwani anakuwa hayupo wakati mwengine).” Na (siku ya tatu)
alipoliona jua linachomoza alisema (kuwaambia): “Hili (jua) ndilo
Mola wangu. Huyu (mola) mkubwa kabisa,” lilipotua alisema: “Enyi
watu wangu! Mimi simo katika hayo mnayoyashirikisha (na Mungu)
“Mimi nimeuelekeza uso wangu kwa Yule aliyeziumba mbingu na
ardhi. Hali ya kuwa nimewacha dini za upotevu. Mimi (ni Mwislamu)
wala si miongoni mwa washirikina.” (Quran 6:75-79)
Kama tulivyosema hapo mwanzoni, Mitume wametumwa kwa kila
taifa na kila kabila ili kuiwezesha imani ya kimaumbile ya
mwanadamu juu ya Mwenyezi Mungu na ule mwelekeo wa
kumwabudu Yeye, pia kuutia nguvu ukweli mtatakatifu kwa dalili na
alama za kila siku zinazooneshwa na Mwenyezi Mungu. Ingawa
mafundisho mengi ya Mitume hao yamebadilishwa, baadhi ya sehemu
zinazofunua ujumbe wa zimebakia bila kuvurugwa na zinahudumia
katika kuwaongoza watu katika kuchagua kati ya haki na batili.
Athari za ujumbe uliofunuliwa na Mwenyezi Mungu kwa muda mrefu
zinaweza kuonekana katika "Amri Kumi" za Torati ya Wayahudi
ambazo baadaye ziligeuzwa na kuwa katika mafundisho ya Kikristo,
19
vilevile, kuwepo kwa sheri dhidi ya uuaji, wizi na uzinzi katika jamii
nyingi kote kote katika zama za kale na za sasa za ulimwengu.
Matokeo ya alama za Mwenyezi Mungu kwa wanadamu wa zama zote
zikiwa na ufunuo wake kupitia Mitume yake, wanadamu wote
wamepewa nafasi ya kumtambua mungu wa kweli wa pekee.
Matokeo yake, kila nafsi itahesabiwa kwa imani yake juu ya
Mwenyezi Mungu na kwa kukubali kwake dini ya kweli ya Mwenyezi
Mungu, iitwayo Uislamu, ambayo inamaanisha utiifu mkamilifu kwa
matakwa ya Allah.
20
HITIMISHO
aelezo yaliyotangulia yamefafanua kwamba jina la dini ya
Kiislamu linaeleza wazo kuu na la msingi la Uislamu, ni
kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba jina
"Uislamu" halikuchaguliwa na mwanadamu, bali lilichaguliwa na
Mwenyezi Mungu, kwa mujibu wa vitabu vitakatifu vya Uislamu.
Vilevile imeoneshwa kwamba ni Uislamu pekee unaofundisha
kwamba Mwenyezi Mungu ni mmoja na Sifa zake na unaamrisha
kumwabudu Mwenyezi Mungu tu bila ya mshirika. Mwisho, kutokana
na utakatifu wa mwelekeo ulioingizwa pole pole kwa mwanadamu ili
amwabudu Mwenyezi Mungu na dalili zilizooneshwa na Mwenyezi
Mungu kwa miaka mingi kwa kila mtu, Uislamu unaweza kufikiwa na
watu wote kwa nyakati zote.
Kwa ufupi, maana ya neno Uislamu (kujisalimisha kwa Allah),
Uislamu kikamilifu unakiri upweke wa Mwenyezi Mungu na ufikiwaji
wa Uislamu kwa watu wote katika nyakati zote kukinaisha watu
kuunga mkono dai la Uislamu la kwamba toka mwanzoni mwa
Ulimwengu katika lugha zote imeelezwa kwamba, Uislamu pekee
ndio uliokuwa na utakaoendelea kuwa dini pekee ya kweli ya
Mwenyezi Mungu.
Tunahitimisha kwa kumuomba Allah, Mtukufu, atuweke katika njia
iliyosahihi ambayo ametuongoza kwayo, na atupatie baraka na rehema
zake, kwani yeye ni Mwingi wa msamaha. Shukrani ziende kwa
Allah, Mola wa ulimwengu wote, na rehema na amani ziende kwa
Mtume Muhammad (S.A.W) na kwa Mitume ya Allah yote na kwa
wafuasi wao waliowema.
M