Nakala

1


بسم الله الرحمن ال رحيم


Historia Ya Krismasi Na Hukumu Ya Kusherehekea Na Kupongezana Imetafsiriwa Na: ‘Abdun-Naaswir Hikmany Imepitiwa na :Abubakari Shabani Rukonkwa


2


Historia ya Krismasi


Wakati wa zama za kale, siku ya mwisho ya majira ya


baridi huko sehemu za Kusini kulisherehekewa mfano


wa usiku ambao mungu wa Mama Watakatifu alijifungua


mtoto akijulikana kuwa ni mungu wa Jua. Pia (siku hii)


inaitwa Yule, siku ambayo inasherehekewa mno kwa


kurushwa pashpashi. Ambapo kila mtu atacheza na


kuimba ili kuliamsha jua kutokana na usingizi wake


mnono wa majira ya baridi.


Wakati wa Warumi, iliadhimishwa kwa kumsifu


Satunusi (mungu wa mavuno) na Mithrasi


(mungu wa kale wa nuru), huo ni mtindo wa kuabudia


jua ambao umekuja ukitokea Syria hadi Urumi. Karne


kabla ya madhehebu ya Sol Invictus, ilitangaza ya


kwamba, majira hayo ya baridi sio ya milele, na kwamba


maisha yanasonga mbele, na ni mualiko wa kubaki


kwenye nguvu nzuri.


Siku ya mwisho ya majira ya baridi huko sehemu za


mviringo za Kusini ni baina ya siku ya 20 au 22


Disemba. Warumi waliadhimisha Saturnalia baina ya


tarehe 17 na 24 Disemba.


3


Wakristo wa kale


Ili kuepuka kuchunguzwa wakati wa sherehe ambazo ni


za wapagani, Wakristo wa kale walikaa majumbani


mwao pamoja na mtakatifu Saturnalia. Kwa vile idadi ya


Wakristo iliongezeka na mila zao zikaenea, sherehe


zikachukua shuruti za Kikristo. Lakini, Makanisa ya kale


hakika hayakusherehekea mwezi wa Disemba kwa


kuzaliwa Kristo hadi alipokuja Telesforusi Telesphorus,


ambaye alikuwa askofu wa pili wa Roma kutoka mwaka


125 hadi 136 M, askofu huyo ndiye aliyetangaza


kwamba huduma za Kanisa zifanywe wakati huu ili


kuadhimisha “Kuzaliwa kwa Bwana wetu na Mwokozi”.


Hata hivyo, kwa vile hakuna mtu hata mmoja aliye na


uhakika wa mwezi ambao amezaliwa Kristo, kawaida ya


Uzawa ulikumbukwa Septemba, ambao ulikuwa ni


wakati wa Sherehe za Kiyahudi za Trumpetsi


(kwa sasa ni Rosh Hashanah).


Ukweli ni kuwa, kwa zaidi ya miaka 300, watu


walielewa kuzaliwa kwa Yesu katika tarehe tofauti.


Katika mwaka 274 M, kikomo cha jua kiliangukia tarehe


25 Disemba. Mfalme wa Roma aitwaye Aurelian


alitangaza tarehe hiyo kama ni “Natalis Solis Invicti”,


‘Sherehe Ya Kuzaliwa Jua Lisiloshindikana’. Katika


mwaka 320 M, Papa Julius I aliitangaza tarehe 25


Disemba kama ni tarehe rasmi ya kuzaliwa Yesu Kristo.


Mnamo mwaka 325 M, Krismasi ilitangazwa rasmi,


lakini kiujumla haikutiliwa maanani. Mtakatifu


Constantine, ambaye ni Mfalme wa mwanzo wa dhehebu


la Ukristo la Kirumi, aliitanguliza Krismasi kama ni


4


sherehe isiohamishika kwa tarehe 25 Disemba. Pia


aliitanguliza Jumapili kama ni siku kuu ndani ya siku


saba za wiki, na aliitanguliza (Pasaka) kama ni sherehe


yenye kuhamishika. Mnamo mwaka 354 M, Askofu


Liberius wa Rumi, alitoa amri rasmi kwa wafuasi wake


kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu ndani ya tarehe 25


Disemba.


Hata hivyo, ingawa Constantine aliifanya rasmi tarehe 25


Disemba kama ni sherehe ya kuzaliwa Kristo, Wakristo


wakiitambua kama ni tarehe ya sherehe iliyofanana na


mapagani, hawakushiriki katika mambo mazuri


(kwa siku hii) iliyopangwa na Askof.


Krismasi ilishindwa kupata utambulisho wa


kilimwengu miongoni mwa Wakristo hadi kipindi cha


hivi karibuni.


Huko Uingereza England, Oliver Cromwell alizipiga


marufuku sherehe za Krismasi baina ya miaka 1649 na


1660 kupitia kwa inayoitwa Sheria za Rangi


Samawati Blue Laws, akiamini kwamba iwe ni siku ya


kumuabudu mungu tu.


Hamu ya kuifurahia sherehe ya Krismasi ilikirimiwa pale


Waprotestanto (Wakristo wasiokubali baadhi ya


mafundisho ya Kanisa la Kirumi) walipokimbia


uchunguzi kwa kutorokea sehemu za makoloni yote


duniani. Hata hivyo, Krismasi bado haikuwa ni sikukuu


halali hadi miaka ya 1800.


Na, weka akilini, hakukuwa na picha ya Baba Krismasi


(Santa Claus) kwa wakati huo.


5


Krismasi inaanza kuwa maarufu Umaarufu wa Krismasi ulianza ghafla mnamo mwaka 1820 kutokana na kitabu cha Washington Irving The Keeping of Christmas at Bracebridge Hall ‘Kuiadhimisha Krismasi Kwenye Jukwaa La Bracebridge’. Mnamo mwaka 1834, Malkia wa Uingereza aitwaye Victoria, alimkaribisha mumewe wa Kijerumani Prince Albert ndani ya Ngome ya Windso Windsor Castle, akimuonesha tamaduni za mti wa Krismasi Christmas tree na Nyimbo Za Kumsifu Yesu Kristo carols ambazo ziliadhimishwa Uingereza kwa Mfalme wa Uingereza. Mwaka 1834, wiki moja kabla ya Krismasi, Charles Dickens alichapisha Nyimbo za Kumsifu Yesu za Krismasi Christmas Carols (ambapo aliandika kwamba Scrooge alimuamrisha Cratchit kufanya kazi, na kwamba Baraza Kuu la Marekani US Congress lilikutana Siku ya Krismasi). Ilikuja kuwa ni maarufu mno hadi kufikia kwamba sio makanisa wala serikali kukana umuhimu wa sherehe za Krismasi. Mnamo mwaka 1836, Alabama ilikuja kuwa ni taifa la mwanzo ndani ya Marekani kutangaza Krismasi kama sikukuu halali. Mnamo mwaka 1860, mfananishi illustrator wa Marekani aitwaye Thomas Nast alichukua kutoka hadithi za Kiingereza kuhusu Mtakatifu Nicholas, muangalizi mtakatifu wa watoto, kumtengeneza Baba Krismasi Father Christmas. Mwaka 1907, Oklahoma ilikuwa ni ya mwisho miongoni mwa mataifa ya Marekani kutangaza Krismasi kama ni sikukuu halali. Mwaka baada ya mwaka, nchi za dunia


6


nzima zilianza kuitambua Krismasi kama ni siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu. Nakuombea Krismasi Njema Have a merry Christmas Leo, mambo mengi yasiyokuwa ya Kikristo yananasibishwa ndani ya Krismasi. Yesu alizaliwa mwezi wa Machi, bado siku yake ya kuzaliwa inasherehekewa Disemba ya 25, wakati wa solstice. Sherehe za Krismasi zinamalizikia siku kumi na mbili za Krismasi (Disemba 25 hadi Januari 6), ni idadi hiyo hiyo ya siku ambazo zilisherehekewa na wapagani wa ki-Rumi wakale kwa kuadhimisha kurudi kwa jua. Hivyo, hakuna mshangano wowote kwamba Wakristo waliosafi puritans – au Wakristo wasiotaka mabadiliko conservative – watahamaki kwa Krismasi kuwa “sio ya kidini kama ilivyotakikana kuwa,” wakisahau kwamba Krismasi haikusherehekewa hata kidogo hadi siku za hivi karibuni. Yesu Alisemaje Kuhusu Krismasi? Mazoea ya Krismasi Mti ulio bora wa Krismasi unanunuliwa. Ukipambwa kwa madoido yenye kung’ara pamoja na kumetameta, unasimamishwa karibu na dirisha. Maduka yanajazana wanunuzi wakisaka zawadi na vile viduchu vinasubiri kwa hamu kubwa ya Baba Krismasi Santa.


7


Ni mshughuliko na ni homa ya Krismasi Christmas fever, umewahi kufikiri kabla? Je, Biblia au Yesu aliwahipo kusababisha homa ya Krismasi? Tafakari juu ya mchanganuo ufuatao kuhusu Krismasi, na ukweli utakuja kuwa wazi zaidi na zaidi. Je, Krismasi Ina Ushahidi wa Biblia? Neno ‘Krismasi’ halipo ndani ya Biblia. Biblia ilifunga midomo ya sherehe yote inayohusiana na Krismasi, isipokuwa kwa kitu kimoja; upambaji wa mti. Biblia wenyewe inashutumu upambaji wa miti (ya Krismasi): “Mila za watu si chochote, wanakata mti kutokana na msitu, na mchongaji anauchonga kwa patasi yake, wanaupamba kwa fedha na dhahabu, wanaugandanisha kwa nyundo na misumari ili usipate kutikisika” (Jeremia 10-3,4). Wazungu wa ki-Pagani kabla ya Ukristo, waliamini miujiza kwamba miti ya kijani ina nguvu maalum za ulinzi. Hakika, matumizi ya Miti ya Krismasi imeanza hivi karibuni tu mwa karne ya 17 huko Strasbourg, Ufaransa na kutoka huko ukaenea hadi Ujerumani, Uingereza na baadaye Marekani. “Ibada ya miti ilikuwa ni jambo la kawaida kwa dini miongoni mwa watu wa Tyutoniki Teutonic na Skandinavia Scandinavia wa Ulaya ya kaskazini kabla ya kuingia kwenye Ukristo…Walowezi wa ki-Jerumani walileta mila za Mti wa Krismasi kwenye makoloni ya Kimarekani mnamo karne ya 17. Kufikia karne ya 19, matumizi yake yalienea sehemu tofauti”.


8


(AngaliaEncyclopedia ya Compton, Toleo la 1998). Je, Yesu Alizaliwa Disemba ya 25? Si tarehe ya Disemba 25 wala tarehe nyengine yoyote iliyotajwa ndani ya Biblia kuhusu kuzaliwa kwa Yesu. Ilikuwa ni hivyo hadi kufikia mwaka 530 C.E kwamba mtawa monk aitwaye Dionysus Exigus, aliweka tarehe isiyobadilika ya kuzaliwa kwa Yesu kuwa ni Disemba 25. “Kulingana na taratibu za ki-Roma, alikosea kuipanga tarehe ya kuzaliwa kwa Kristo (yaani, miaka 754 baada ya kupatikana nchi ya Rumi) kama ni Disemba 25, mwaka 753”. (Angalia: Encyclopedia Britannica, toleo la mwaka 1998) Tarehe hii ilichaguliwa ili iendane pamoja na sikukuu ambazo zimeshagandana na imani za kipagani. Mapagani wa Kirumi walisherehekea Disemba 25 kama ni ya kuzaliwa kwa ‘mungu’ wao wa nuru, aitwaye Mithra. “Mnamo karne ya pili M, hiyo sherehe ya Mithra ilikuwa ni ya kawaida zaidi ndani ya Ufalme wa Rumi kuliko Ukristo, ambayo ilizaa mifanano iliyo mingi” (The Concise Columbia Encyclopedia, toleo la mwaka 1995). ‘Waungu’ wengine wakipagani waliozaliwa Disemba ya 25 ni: Hercules mtoto wa Zeuz (Wagiriki); Bacchus, ‘mungu’ wa mvinyo (Warumi); Adonis, ‘mungu’ wa Kigiriki, na ‘mungu’ Freyr wa Ugiriki-mapagani wa Roma.


9


Je, Vipi Kuhusu Baba Krismasi Santa Claus? Kama viumbe visivyokuwa binaadamu aliens watafika duniani katika wakati wa Krismasi, bila ya shaka wataamini Krismasi kuwa ni sherehe ya kufurahikia kuzaliwa kwa Baba Krismasi Santa. Majina ya ‘Santa Claus’, hayamo popote ndani ya Biblia. Hata hivyo, Mtakatifu Nikolas Saint Nicholas (Baba Krismasi Santa Claus) alikuwa ni mtu halisi, askofu, ambaye alizaliwa miaka 300 baada ya Yesu. Kwa mujibu wa hekaya za kale, alikuwa ni mtu mwenye huruma mno na alitenga nyakati za usiku kwenda kutoa zawadi kwa mafukara. Baada ya kifo chake mnamo Disemba ya 6, watoto wa shule huko Ulaya walianza kusherehekea siku hiyo kwa karamu kila mwaka. Baadaye Malkia Victoria aliibadilisha sherehe hiyo kutoka Disemba ya 6 kuwa ni Disemba ya 24 kuamkia Krismasi.


11


Je, Yesu au Wafuasi Wake Waliwahi Kusherehekea Krismasi? Kama Yesu alimaanisha kwa wafuasi wake kusherehekea Krismasi, angeliifanyia kazi yeye mwenyewe na kujikusanya pamoja na wafuasi wake. Hakuna sehemu iliyotajwa ndani ya Biblia kwamba kuna mfuasi yeyote aliyewahi kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu kama Wakristo wanavyofanya leo. “Kanisa halikupatapo kuweka sikukuu kwa ajili ya sherehe za tukio la Krismasi hadi ilipofika karne ya 4” (Angalia:Encyclopedia ya Grolier) Hivyo, tunaona kwamba sio Biblia wala Yesu na wafuasi wake waliosema kitu kuhusu sherehe za Krismasi ambazo sasa zinahusisha viingilio vya sherehe, biashara, na matumizi yaliyochupa mpaka, ni utovu wa akili kwa mfananisho wowote wa imani. Hukumu Ya Krismasi Na Mwaka Mpya Shukrani Ziende kwa Allaa Shaykh Al-Islaam bin Taymiyah (Allah Amrehemu) alisema kwenye fafanuzi yake katika Aayah (tafsiri ya maana): {{Na wale ambao hawashuhudii shahada za uongo (az-zuur)…}} [Al-Furqaan 25: 72]. Ama kuhusu sherehe za mushrikiyn: wanakusanya pamoja mambo yenye kutia wasiwa.si, mahitaji ya mwili


11


na uongo, hakuna chochote ndani yake ambacho kina faida ya kidini, na mwisho wa kutosheleza hizo shahawa, ni maumivu. Hivyo, vitendo vyao ni vya uongo, na kuvishuhudia kunamaanisha kuvifanya. Hii Aayah peke yake inawapandisha daraja na kuwapa moyo (wale ambao hawashuhudii uongo), ambayo ina maana ya kuwahimiza watu kuachana na kushiriki kwenye sherehe zao (mushrikuun) na aina nyenginezo za uongo. Tunafahamu kwamba ni vibaya kushiriki kwenye sherehe zao kwa sababu wanaitwa az-zuur (waongo). Inamaanisha kwamba ni haraam kufanya hivi kwa sababu zilizo nyingi, kwa sababu Allah Ameiita ni az-zuur. Allah Anamlaumu yule anayezungumza uongo (az-zuur) hata ikiwa hamna yeyote atakaeathirika nao, kama ilivyo ndani ya Aayah ikikataza Dhwihaar (aina ya talaka ambapo mume anamwambia mkewe “Wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu”), ambapo Yeye Anasema (tafsiri ya maana): {{…Wanasema neno baya na la uongo (zuuran)… }} [Al-Mujaadalah 58: 2]. Na Allah Anasema (tafsiri ya maana): {{…basi jiepusheni na uchafu wa masanamu na jiepusheni na usemi wa uongo.}} [Al-Hajj 22:30]. Hivyo yule ambaye anafanya az-zuur analaumiwa kwa mtindo huu. Ndani ya Sunnah: Anas bin Maalik (Allah Amrehemu) amesema: “Mtume wa Allah (s.a.w) alikuja (Madiynah) na walikuta siku mbili ambazo kipindi cha Jaahiliyyah watacheza (na


12


kujipumzisha).” Mtume wa Allah (s.a.w) akasema: “Allah Amekupeni kilicho bora zaidi kuliko mambo hayo: Yawm adh-Dhuhaa (‘Iyd al-adh haa) na Yawm al-Fitr (‘Iyd al-Fitr).” [Imesimuliwa na Abuu Daawuud]. Hii inaonesha wazi kwamba Mtume (s.a.w) bila ya shaka alizuia Ummah wake kusherehekea sherehe za kikafiri, na alihakikisha kuziondosha kwa njia zozote zinazowezekana. Ukweli wa kwamba dini ya Watu wa Kitabu inakubaliwa, haina maana kwamba sherehe zao zinakubalika au ziendelezwe na Ummah, kama yalivyo matendo yao mengine ya kikafiri yasivyokubalika, na dhambi zao pia hazikubaliki. Hakika, Mtume (s.a.w) alifikia hadi kuamrisha Ummah wake kujitofautisha nao kwenye mambo mengi ambayo ni mubaah (yanaruhusiwa) na kwa taratibu nyingi za ibada, kwa sababu tu; kwamba vinapelekea kuwa sawa nao kwenye mambo mengine pia. Hii kuweka tofauti; ni kuonesha kizuizi katika nyanja zote, kwa sababu namna utakavyokuwa tofauti na watu wa Motoni, ndivyoutakavyokuwa mchache wa kutenda matendo ya watu wa Motoni. Ushahidi wa mwanzo ni Hadiyth ya: “Kila watu wana sherehe zao, na hii ndio sherehe yetu” ambayo ina kusudio maalum kwamba; watu wote wana sherehe zao wenyewe, kama Allah Anavyosema (tafsiri ya maana): {{Na kila ummah ulikuwa na Qiblah walichokielekea…}} [Al-Baqarah 2: 148] na


13


{{Na kila (ummah) katika nyinyi (bin Aadam) Tumeujaalia shari'ah yake na njia yake yake}}. [Al-Maaidah 5: 48]. Hii inamaanisha kwamba kila taifa lina njia zake wenyewe. Hiyo laam ndani ya li-kulli (“kwa kila”, “katika nyinyi”) ina maana kwa watu maalum. Hivyo, kama Mayahudi wana sherehe na Wakristo wana sherehe, ni za kwao wenyewe, na sisi hatuna sehemu yetu ndani ya hizo sherehe, kama vile tusivyotumia Qiblah kimoja au sheria zao. Ushahidi wa pili ni: masharti aliyoweka ‘Omar bin al-Khattwaab (r.a) na kukubaliana pamoja naSwahaabah na Fuqaaha wote baada yao ni: kwa wale Watu wa Kitabu ambao wamekubali kuishi chini ya hukumu za Kiislamu (ahl adh-dhimmah) wasisherehekee sherehe zao wazi wazi ndani ya Daar al-Islam (ardhi zilizo chini ya hukumu za Kiislamu). Kama Waislamu wamekubaliana kuwazuia ahl adh-dhimmah kusherehekea wazi wazi, ni namna gani itakuwa sahihi kwa Waislamu kushereheka nao wazi wazi? Kama Muislamu atawasherehekea, jee sio zaidi ya kafiri anavyofanya wazi wazi? Sababu iliyokuwepo ya sisi kuwazuia wasisherehekee sherehe zao wazi wazi ni kwa sababu ya machafu yaliyokuwemo humo. Kwa sababu ya dhambi au alama ya dhambi. Katika kesi yoyote, Muislamu anazuiwa kutenda dhambi au kujaribu kutenda dhambi. Hata kama hakuna uadui wowote kwa Muislamu kuwa nao pamoja katika kusherehekea wazi wazi isipokuwa kafiri kupata nguvu ya kuendelea na matendo yake. Inakuwaje Muislamu anatenda hivyo? Uadui


14


uliokuwemo (ndani ya sherehe zao) utaelezwa chini, insha Allah. Al-Bayhaqiy amesimulia ikiwa na isnaad swahiyh kwenye Baab karaahiyat ad-dukhuul ‘ala ahl adh-dhimmah fi kanaa’isihim wat-tashabbuh bihim yawmi nawruuzihim wa maharjaanihim (Sura kuhusu karaha ya kuingia kwenye makanisa ya ahl adh-Dhimmah (Makafiri walio katika nchi ya Kiislam) katika kuadhimisha Mwaka wao Mpya na sherehe nyengine): Kutokana na Sufyaan ath-Thawri na kutokana na Thawr bin Yaziyd na kutokana na ‘Atwa’ bin Diynaar ambao wamesema: ‘Umar amesema: “Musijifunze lugha ya wasiokuwa Waarabu, musiingie pamoja na mushrikiyn kwenye makanisa yao katika siku za karamu zao, kwani laana (za Allah) zinawashukia juu yao.” ‘Omar bin Al-Khattwaab amesema: “Jiepusheni na maadui wa Allah kwenye sherehe zao.” Imesimuliwa kutokana na Abuu Usaamah ikiwa na isnaadiliyo sahihi kwamba: ‘Awn alituambia kutokana na Mughiyrah kutokana na ‘Abdullaah bin ‘Amr: “Yeyote anayeishi ndani ya ardhi ya wasiokuwa Waarabu na kusherehekea Mwaka wao Mpya na sherehe zao, na kujifananisha nao hadi anafariki akiwa na hali hiyo, atakusanywa pamoja nao kwenye Siku ya Malipo.” ‘Umar alikataza kujifunza lugha zao, na hata kuingia kwenye makanisa yao katika siku ya sherehe yao, jee ni vipi kwa kufanya baadhi ya mambo wanayoyafanya kwenye siku hizo, au kufanya vitu ambavyo ni sehemu ya dini yao? Je, sio kufanya baadhi ya vitu wanavyofanya kwenye sherehe zao ni (uovu) zaidi ya kuingia tu kwenye sherehe zao? Kama laana za Muumba zitaanguka juu yao kwenye siku ya


15


sherehe yao kwa sababu ya yale wanayofanya, je, adhabu hiyo haitokuwa sawa kwa yule anayefanya yale wanayotenda wao, au sehemu ya hayo? Je, sio maneno ya: “Jiepusheni na maadui wa Allah, kwenye sherehe zao” yana maana kwamba tusikutane nao au kushirikiana nao kwenye siku hizi? Je, ni vipi kwa mtu ambaye hakika anasherehekea sherehe zao? ‘Abdullaah bin ‘Amr amesema kwa uwazi: “Yeyote anayeishi ndani ya ardhi ya wasiokuwa Waarabu na kusherehekea Mwaka wao Mpya na sherehe zao, na kujifananisha nao hadi anafariki akiwa na hali hiyo, atakusanywa pamoja nao kwenye Siku ya Malipo.” Hii inamaanisha kwamba yule anayejikusanya nao kwenye mambo yote haya ni kafiri, au kwamba kufanya hivi ni miongoni mwa dhambi kubwa (kabaa’ir) kwamba itampelekea mmoja wao Motoni; maana ya iliyopita ni ile iliyo wazi kutokana na mpangilio wa maneno. Alitaja – Na Allah Ndie Ajuaye Zaidi – yule anayeishi kwenye ardhi yao, kwa sababu wakati wa ‘Abdullah bin ‘Amr na Swahaabah wengineo, walikuwa wakizuia sherehe zilizo wazi za kikafiri ndani ya ardhi za Waislamu. Na hakuna Muislamu aliyewaiga kwenye sherehe zao; hilo (la kusherehekea) pale ambapo wanapoishi kwenye ardhi za kikafiri. ‘Aliy (r.a) alikataa hata kulitambua jina la sherehe zao ambazo zilikuwa mahsusi kwa ajili yao, je, itakuwaje kwa kushereheka nao kisawasawa? Ahmad ametaja maana ya simulizi zilizopokelewa kutokana na ‘Omar na ‘Aliy (r.a) kwenye mada hii, na wafuasi wake walijadili masuala ya sherehe. Imaam Abul-Hassan al-‘Aamidiy alisema: mwandishi anayejulikana kwa jina la Ibn al-Baghdaadi alisema


16


ndani ya kitabu chake Umdat al-Haadhwir wa Kifaayat al-Musaafir: “Hairuhusiwi kuingia kwenye sherehe za Wakristo na Mayahudi.” Ahmad alitamka hili kwenye simulizi ya Muhannaa, na ushahidi wake wa hilo ni Aayah (tafsiri ya maana): {{Na wale ambao hawashuhudii shahada za uongo (az-zuur)… }} [Al-Furqaan 25: 72]. Alisema: (Hizi sherehe ni) ash-Sha’aaniyn pamoja na sherehe zao. Alisema: Waislamu wazuiliwe kuingia kwenye masinagogi (makanisa ya Kiyahudi) na makanisa (ya Wakristo).” Kutokana na Iqtidhwa’ as-Swiraat al-Mustaqiym Mukhaalifat Aswhaab al-Jahiym iliyoandikwa na Shaykh al-Islaam bin Taymiyah, uk. 183. Kuwatakia kheri ya Krismasi Makafiri na hata sikukuu nyengine za dini tofauti ni haraam kwa mujibu wa makubaliano ya wengi, kama Ibn al-Qayyim (Allah Amrehemu) alisema kwenye Ahkaam Ahl adh-Dhimmah. “Kuwatakia kheri Makafiri katika mwenendo ambao ni kwa ajili yao ni haraam kwa makubaliano ya wengi, kama ilivyo haraam kuwatakia kheri katika sherehe zao na funga zao kwa kusema ‘Kila la kheri katika sherehe’ au ‘Nakutakia sherehe njema’, na mengineyo. Hata kama yule anayesema haya ameepushwa na ukafiri, lakini bado imekatazwa. Ni kama vile kumpa hongera mtu kwa kuuhami msalaba, au zaidi ya hivyo. Ni kama mfano wa dhambi iliyo kubwa sawa na kumpa hongera mnywaji ulevi, au kumuua mtu, au kuwa na mahusiano ya kinyama, na mengineyo.


17


Wengi miongoni mwa wasio na heshima ya dini yao wanaangukia kwenye kosa hili; hawakai kufikiria ubaya wa vitendo vyao. Yeyote anayempa hongera mtu kwa kutovukwa na adabu au bid’ah au ukafiri amejiweka wazi na laana pamoja na ghadhabu za Allah.” Kuwapatia hongera makafiri kwenye sherehe za kidini ni haraam kama alivyokwenda mbali Ibn al-Qayyim kwa kufananisha na kwamba yule anayetoa salamu hizo amekubali au ameidhinisha matendo yao ya kikafiri, hata kama mtu hatovifanya mwenyewe vitu hivyo. Lakini Muislamu asikubali mienendo ya kikafiri wala kumpa hongera yeyote kwa ajili yao, kwa sababu Allah hakubali matendo yoyote kati ya hayo, kama Alivyosema (tafsiri ya maana): {{Mkikufuru, basi Allah hana haja nanyi; lakini Haridhii kufuru kwa waja Wake; na kama mkishukuru; hayo Yanamridhisha kwenu.}} [Az-Zumar 39:7]. {{…Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na kukutimizieni neema Yangu, na Nimekupendeleeni Uislamu uwe Dini yenu…}} [Al-Maaidah 5:3]. Hivyo kuwapa pongezi kunazuiwa, hata ikiwa ni mwenzio kazini au vyenginevyo. Kama wao watatutakia kheri kwa kuadhimisha sherehe zao, hatutakiwi kujibu, kwasababu hizi sio sherehe zetu, na kwasababu sio sherehe ambazo zinakubalika na Allah. Sherehe hizi ni uzushi ndani ya dini zao, na hata zile ambazo zimetajwa huko kabla zimetenguliwa na dini ya Kiislamu, ambayo Ameileta Allaah kwa wanaadamu wetu kupitia kwa bwana Muhammad (s.a.w).


18


Allah Anasema (tafsiri ya maana):{{Na anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitakubaliwa kwake. Naye Aakhirah atakuwa katika wenye khasara (kubwa kabisa)}} [Aaali-‘Imraan 3:85]. Ni haraam kwa Muislamu kukubali mialiko katika sherehe kama hizo, kwa sababu ni zaidi ya kuwatakia kheri kama inavyoonesha kushiriki katika sherehe zao. Vile vile, Waislamu wanazuiwa kuwaiga makafiri katika kuadhimisha huko kwa kushiriki kwenye tafrija parties, au kwa kubadilishana zawadi, au kutoa peremende au chakula, au kuacha kufanya kazi, n.k. Kwa sababu Mtume (s.a.w) alisema “Yeyote anayewaiga watu ni mmoja wao.” Shaykh al-Islaam bin Taymiyah amesema ndani ya kitabu chake Iqtidhwaa’ asw-Swiraat al-Mustaqiym Mukhaalifat Aswhaab Al-Jahiym: “Kuwaiga katika baadhi ya sherehe zao inamaanisha kwamba mtu amefurahia imani zao za uongo na vitendo vyao, na anawapa matumaini kwamba wanaweza kuwa na nafasi ya kuwanyanyasa na kuwapeleka ovyo wanyonge.” Yeyote anayefanya mambo kama haya ni mtenda dhambi, ikiwa anafanya kwa ukarimu au urafiki, au kwa sababu anaona hayaa kukataa, au kwa sababu nyengine yoyote. Kwa sababu ni unafiki ndani ya Uislamu, na kwa sababu inawafanya makafiri kujisikia fakhari kwa dini yao. Allah Pekee ndiye tunayemuomba kuwafanya Waislamu kuwa fakhari na dini yao, kuwasaidia kuwa thaabiti katika kushikamana na dini yao, na kuwafanya kuwa washindi dhidi ya maadui zao, kwani Yeye Mwenye Nguvu ndiye Mwenye Kuweza.



Machapisho ya hivi karibuni

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL

Masuala kumi muhimu n ...

Masuala kumi muhimu na mafupi kuhusu mwezi wa Muharram

UJUMBE KWA ALIYEICHOM ...

UJUMBE KWA ALIYEICHOMA KURANI