Nakala

Wote tunasoma biblia mchana na usiku,





ila wewe unasoma nyeusi mimi ninasoma nyeupe.





                              —William Blake, The Everlasting





Injili





Hakika, hisia za Blake katika nukuu ya hapo juu sio jambo jipya. Agano Jipya lina utofauti wa kutosha kwa kuzalisha tafsiri mbali mbali, imani na dini, zote zinazodaiwa ni za Biblia. Kwa hivyo, tunamwuona mwandishi mmoja akitoa maoni ya kufurahisha :





Unaweza na hauwezi,





Utakuwa na hautakuwa,





Utafanya na hautafanya,





Na utalaaniwa ikiwa uta,





Na hautalaaniwa ikiwa hauta.[1]





Kwa nini kuna kutofautiana katika maoni hayo? Mwanzo kabisa, kambi tofauti za kitheolojia hazikubaliani ni vitabu gani vinapaswa kuingizwa katika Biblia. Kambi moja ya Apocrypha ni maandiko ya mwingine. Pili, hata kati ya vitabu hivyo ambavyo vimetangazwa kuwa vitakatifu, maandishi mbali mbali ya vyanzo hayana usawa. Upungufu huu wa usawa uko kila mahali ambapo The Interpreter’s Dictionary of the Bible inasema, "Ni salama kusema kuwa hakuna sentensi moja katika NT (Agano Jipya) ambayo inafanana kabisa na MS [andiko].''[2]





Siyo sentesi hata moja?  Hatuwezi kuiamini sentesi moja ya biblia?  Ngumu kuamini.





Labda





Ukweli ni kwamba kuna zaidi ya maandiko 5700 ya Kigiriki katika Agano Jipya lote au sehemu.[3]  Tena, “hakuna usawa katika maandiko haya mawili katika maelezo hayo yote….  Na baadhi ya tofauti hizi ni za muhimu sana”[4] Katika maandiko takriban elfu kumi za Vulgate ya Kilatini, ongeza aina zingine nyingi za zamani (i.e., Syriac, Coptic, Armenian, Georgia, Ethiopia, Nubian, Gothic, Slavonic), sasa tuna nini?





Maandiko mengi





Maandiko mengi ambayo yalishindwa kuendana katika maeneo na mara kwa mara kupingana. Wasomi wanakadiria idadi mbalimbali za maandiko yapo mamia kwa maelfu, wengine wanakadiria kuwa juu ya 400,000.[5]  Bart D.  Ehrman’s katika maneno yake maarufu, “Labda ni rahisi kuliweka jambo kwa kulinganisha: kuna utofauti mwingi katika maandiko yetu kuliko maneno katika Agano Jipya.”[6]





Hii imetokea vipi?





Utunzaji dhaifu.  Udanganyifu.  Uzembe.  Upendeleo wa Mafundisho.  Fanya uchaguzi.





Hakuna maandiko yoyote ya asili yaliyosalimika tangu kipindi cha Ukristo wa mwanzo.[7]/[8]  Maandiko kamili ya zamani zaidi (Vatican MS. No. 1209 na Sinaitic Syriac Codex) ni za karne ya nne, miaka mia tatu baada ya uongozi wa Yesu. Lakini nakala za asili? Zilipotea. Na nakala za asili? Pia zimepotea. Maandiko yetu ya zamani zaidi, kwa maneno mengine, ni nakala za nakala za nakala za hakuna mtu anayejua-ni-nakala ngapi za asili.





Ndio sababu aishangazi kutofautiana





Katika mikono mizuri, kunakili makosa hakushangazi. Ila, maandiko ya Agano Jipya hayakuwa katika mikono mizuri. Katika kipindi cha chimbuko la Ukristo, waandishi walikuwa wasio na mafunzo, wasioaminika, wasio na uwezo, na wakati mwingine hawajui kusoma na kuandika.[9]  Wale ambao walikuwa na ulemavu wa kuona wangeweza kufanya makosa ya kiherufi na maneno yanayofanana, wakati wale ambao walikuwa na ulemavu wa kusikia wanaweza kuwa walifanya makosa katika kunakili maandiko wakati yalipokuwa yanasomwa kwa sauti. Mara kwa mara waandishi walikuwa wakifanya kazi kupita kiasi, na kwa hivyo kupelekea kufanya makosa ambayo yanaambatana na uchovu.





Kwa maneno ya Metzger na Ehrman, "Kwa kuwa wengi, ikiwa sio wote, hao [waandishi] walikuwa wageni katika sanaa ya kunakili, idadi kubwa ya makosa bila shaka yaliingia kwenye maandishi yao wakati wanayatengeneza.”[10]  Mbaya zaidi, waandishi wengine waliruhusu ubaguzi wa kimafundisho kuathiri uwasilishwaji wao wa maandiko.[11] Kama Ehrman asemavyo, "Waandishi ambao walinakili maandishi hayo waliyabadilisha." [12]  Hasa zaidi, "Idadi ya mabadiliko ya makusudi yaliyofanywa kwa maslai ya muandishi ni ngumu kuyatathmini."[13]  Na Pia la zaidi, "Kwa maoni ya kiufundi ya ukosoaji wa waandishi - ambayo ninahifadhi kwa muhimu mkubwa - waandishi hawa 'walichafua' maandishi yao kwa sababu za kitheolojia."[14]





Makosa yaliletwa kwa njia ya nyongeza, kufutwa, kubadilisha na kurekebishwa, kwa kawaida inakuwa maneno au mistari, lakini mara kwa mara inakuwa aya nzima.[15] [16] Kwa hakika, "mabadiliko mengi na nyongeza ziliingia kwenye maandishi,"[17] na matokeo yake kuwa "mashahidi wote wanaojulikana wa Agano Jipya wamechanganywa kwa kiwango kikubwa au kidogo, na hata maandiko kadhaa za mwanzo hayana makosa mengi."[18]





Katika Kumnukuu Yesu vibaya, Ehrman anatoa ushahidi wenye kushawishi kwamba hadithi ya yule mwanamke aliyechukuliwa katika uzinzi (Yohana 7: 53-8: 12) na aya za kumi na mbili za mwisho za Marko hazikuwa kwenye injili ya asili, lakini ziliongezwa na waandishi wa baadaye.[19]  Cha kuongezea, mifano hii "inawakilisha sehemu mbili tu kati ya maelfu ya sehemu ambazo maadiko ya Agano Jipya yalibadilishwa na waandishi."[20]





Kwa hakika,vitabu vyote vya biblia vilighushiwa.[21]  Hii haimaanishi kuwa maudhui yake siyo sahihi, lakini kwa hakika haimaanishi kuwa yapo sawa. Sasa ni vitabu gani vilighushiwa? Waefeso, Wakolosai, 2 Wathesalonike, 1 na 2 Timotheo, Tito, 1 na 2 Petro, na Yuda — ambavyo ni vitabu tisa kati ya ishirini na saba vya Agano Jipya na waraka—kwa kiwango kimoja au kutuhumiwa kwa kiwango fulani.[22]





Vitabu vya kughushi? Kwenye Biblia?





Kwa nini hatushangai? Kwa haya, hata waandishi wa injili hawajulikani. Kiuhakika, hawatambuliki.[23]  Wasomi wa kibiblia ni adimu, kama wapo, waandishi wa uandishi kwa injili ya Mathayo, Marko, Luka, au Yohana. Kama vile Ehrman anatuambia, "Wasomi wengi leo wameacha utambulisho huu, na wanatambua kuwa vitabu hivyo viliandikwa na Wakristo wanao okuongea (na kuandika) vizuri Kigiriki wakati wa nusu ya pili ya karne ya kwanza."[24] Graham Stanton anathibitisha, "Injili, tofauti na maandiko mengi ya Wagiriki na Warumi, haijulikani. Vichwa ya habari vinavyojulikana ambavyo vinatoa jina la mwandishi (‘Injili kulingana na…’) havikuwa sehemu ya maandiko ya asili, kwaajili hiyo viliongezwa mwanzo wa  karne ya pili. ”[25]





Hivyo, ikiwa kuna chochote, wanafunzi wa Yesu walikuwa na uhusiano gani na uandishi wa injili? Kidogo au hakuna wowote,kama tunavyojua. Ila hatuna sababu ya kuamini kuwa waliandika vitabu vyovyote vya Biblia. Kwa kuanza, hebu tukumbuke kuwa Marko alikuwa msaidizi wa Petro, na Luka alikuwa mwenzake Paulo. Mistari ya Luka 6: 14-16 na Mathayo 10: 2-4 huorodhesha wanafunzi kumi na wawili, na ingawa orodha hizi zinatofautiana juu ya majina mawili, Marko na Luka hawapo kwenye orodha yoyote. Kwa hivyo ni Mathayo na Yohana tu ndio walikuwa wanafunzi wa kweli. Lakini, hata hivyo wasomi wa sasa wanawakataa kuwa kama waandishi.





Kwanini?





      Swali zuri. Yohana akiwa maarufu zaidi kati ya hao wawili, kwa nini tunamkataa kuwa mwandishi wa Injili ya "Yohana"?





Umm … kwasababu alikufa?





Vyanzo vingi vinakubali kuwa hakuna ushahidi, isipokuwa tu ushuhuda wenye kutiliwa shaka wa waandishi wa karne ya pili, kupendekeza kwamba mwanafunzi Yohana ndiye mwandishi wa Injili ya "Yohana."[26] [27] Labda mkanusho mkubwa ni kuwa mwanafunzi John anaaminika kufa ndani au karibu ya 98 CE.[28]  Ila, Injili ya Yohana iliandikwa karibu ya 110 CE.[29]  Kwa hiyo hakuwa Luka (mwenza wa Paulo), Marko (msaidizi wa Petro), na Yohana (asiyejulikana, na pia kwa hakika sio yule aliyekufa kwa kipindi kirefu), hatuna sababu ya kuamini injili yoyote iliandikwa na wanafunzi wa Yesu. . . .





 



Machapisho ya hivi karibuni

Uislamu Ni dini ya ma ...

Uislamu Ni dini ya maumbile na akili na furaha

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL