Nakala

Biblia ni maandiko matakatifu ya Uyahudi na Ukristo. Biblia ya Kikristo ina Agano la Kale na Agano Jipya, huku matoleo ya Kikatoliki na ya Kiorthodoksi ya Mashariki ya Agano la Kale yakiwa makubwa kidogo kwa sababu ya kukubalika kwa vitabu fulani ambavyo havikubaliwi kama maandiko na Waprotestanti. Biblia ya Kiyahudi inajumuisha tu vitabu vinavyojulikana kwa Wakristo kama Agano la Kale. Zaidi ya hayo, mipangilio ya vitabu vinavyokubalika vya Wayahudi na vya Wakristo vinatofautiana sana.[1] Mtume Muhammad ametabiriwa katika Agano la Kale na Agano Jipya.





 Yesu na Mitume wake wanaaminiwa kuwa waliongea Kiaramu. Kiaramu kiliendelea kutumika katika matumizi makubwa hadi takriban 650  BK, kilipobadilishwa na Kiarabu. [2] Biblia ya leo, hata hivyo, haitoki kwa miswada ya Kiaramu, bali kwa matoleo ya Kigiriki na Kilatini.





 Kunukuu utabiri wa Biblia haumaanishi ya kwamba Waislamu wanakubali kuwa Biblia ya leo kwa ukamilifu wake ni ufunuo wa Mungu. Kwa imani ya Kiislamu kuhusu maandiko yaliyopita, tafadhali bofya hapa





 Sio sharti kwa nabii kukubalika kuwa lazima atabiriwe na manabii wa awali. Musa alikuwa nabii kwa Farao ingawa hakutabiriwa na mtu yeyote kabla yake. Ibrahimu alikuwa nabii wa Mungu kwa Nimrodi, lakini hakuna mtu aliyetabiri kuja kwake. Nuhu na Lutu na wengine walikuwa manabii wa kweli wa Mungu, lakini hawakutabiriwa. Ushahidi wa ukweli wa nabii hautegemei utabiri wa manabii wa zamani, lakini unajumuisha ujumbe halisi ulioletwa naye, miujiza na zaidi.





 Kujadili mambo ya unabii ni suala nyeti. Inahitaji kuangalia kwa kina matoleo ya Biblia na tafsiri zake, miswada iliyogunduliwa hivi karibuni na kutafuta maneno ya Kiebrania, ya Kigiriki, na ya Kiaramu na kuyachunguza. Kazi inakuwa ngumu zaidi wakati: “kabla ya vyombo vya uchapishaji kuvumbuliwa (karne ya 15), nakala zote za Biblia zinaonyesha tofauti za kimaandishi. “[3] Hili si jambo rahisi kwa watu wa kawaida. Kwa sababu hiyo, ushuhuda bora unatoka kwa wataalamu wa kale na wa kisasa katika mambo hayo ambao walikubali utabiri.





 Tuna kumbukumbu za Wayahudi na Wakristo wa kale, watawa na marabi, ambao walishuhudia kwamba Muhammad alikuwa utimilifu wa utabiri mahususi wa Biblia. Wafuatao ni baadhi ya mifano ya watu hawa.





Mtume Anayesubiriwa


Wayahudi na Wakristo wa Arabia kabla ya Uislamu  walikuwa wakisubiri mtume. Kabla ya kutokea kwa Muhammad, Arabia ilikuwa makao ya Wayahudi, Wakristo, na Waarabu Walioabudu masanamu ambao, mara kwa mara, walikwenda vita kati yao. Wayahudi na Wakristo wangesema: 'Wakati umefika wa Nabii asiye andika wala kusoma atakayefufua dini ya Ibrahimu kutokea. Na tutaungana naye, na tutapigana vita vikali dhidi yenu.' Muhammad alipotokea, baadhi yao walimuamini, na wengine walikataa. Hii ndiyo sababu Mungu alifunua:





"Na kilipo wajia Kitabu [Kurani] kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kinacho thibitisha waliyo nayo- na wao walikuwa wakitafutia ushindi kuwashinda makafiri- yalipo wajia yale waliyo kuwa wakiyajua waliyakanusha. Basi laana ya Mwenyezi Mungu juu yao wakanushao." (Kurani 2:89)





Shahidi wa kwanza alikuwa Buhra, mtawa Mkristo, aliyetambua unabii wa Muhammad alipokuwa bado mdogo na kumwambia mjomba wake:





"…Mpwa wako ana bahati kubwa mbele yake, hivyo mrudishe nyumbani haraka."[4]





Shahidi wa pili alikuwa Waraqah ibn Nawfal, msomi Mkristo aliyefariki punde baada ya mkutano wa faragha na Muhammad. Waraqah alimshuhudia Muhammad kuwa alikuwa Nabii wa wakati wake na kupokea ufunuo kama Musa na Yesu.[5]





Wayahudi wa Madina walikuwa wakisubiri kwa hamu kuwasili kwa nabii. Mashahidi wa tatu na wa nne walikuwa Marabi wao maarufu wa Kiyahudi, Abdullah ibn Salam na Mukhayriq.[6]





 Mashahidi wa sita na wa saba walikuwa pia rabi wa Kiyahudi wa Yemeni, Wahb ibn Munabbih, na Ka'b al-Ahbar (alikufa 656 BK). Ka'b alipata vifungu vingi vya sifa na maelezo ya Nabii yaliyotabiriwa na Musa katika Biblia.[7]





Quran inasema:





"Je! Haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua haya wanazuoni wa Wana wa Israili?" (Quran 26:197)


Kumbukumbu la Torati 18:18  "Mimi (Mwenyezi Mungu) nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe (Musa), nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.'





Wakristo wengi wanaamini utabiri huu uliotabiriwa na Musa unahusu Yesu. Hakika Yesu alitabiriwa katika Agano la Kale, lakini kama itakavyokuwa wazi, utabiri huu haufanani naye, bali unaafikiana zaidi na Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake. Musa alitabiri yafuatayo:





1.       Mtume huyo atakuwa kama Musa


.





Kipengele cha Ulinganisho





Musa





Yesu





Muhammad





Kuzaliwa





alizaliwa kawaida





alizaliwa kimiujiza, mama yake alikuwa bikira





alizaliwa kawaida





Lengo





Mtume tu





Inasemekana ni mtoto wa Mungu





Mtume tu





Wazazi





baba na mama





mama pekee





baba na mama





Maisha ya kifamilia





alioa na kuzaa watoto





hakuoa





alioa na kuzaa watoto





Kukubaliwa na watu wake





Wayahudi walimkubali





Wayahudi walimkataa[1]





Waarabu walimkubali





Mamlaka ya kisiasa





Musa alikuwa nao (Hesabu 15:36)





Yesu aliukataa[2]





Muhammad alikuwa nao





Ushindi juu ya wapinzani wake





Farao alikufa majini





inasemekana alisulubiwa





Watu wa Makka walishindwa





Kifo





Kifo cha kawaida





inadaiwa kuwa alisulubiwa





Kifo cha kawaida





Kuzikwa





alizikwa kwa kaburi





kaburi tupu





alizikwa kwa kaburi





Uungu





si mungu





wakristo wanaamini ni mtoto wa mungu





si Mungu





Alianza uhubiri kwa umri wa





40





30





40





Kufufuka duniani





hakufufuka





inadaiwa alifufuka





hakufufuka





 





 


2.       Nabii aliyesubiriwa atatoka kati ya Ndugu wa Wayahudi


Aya tunayoongelea ni wazi kwa kusema kwamba nabii atatokea miongoni mwa Ndugu wa Wayahudi. Ibrahimu alikuwa na wana wawili: Ishmaeli na Isaka. Wayahudi ni wazao wa mwana wa Isaka, Yakobo. Waarabu ni watoto wa Ishmaeli. Hivyo, Waarabu ni ndugu wa taifa la Kiyahudi.[3] Bibilia inasema:





‘Naye (Ishmaeli) atakaa mbele ya uso wa ndugu zake wote.’ (Mwanzo 16:12)





‘Naye (Ishmaeli) akakata pumzi, akafa. Akakusanywa kwa watu wake.’ (Mwanzo 25:18)





Wana wa Isaka ni ndugu wa Waishmaeli. Vivyo hivyo, Muhammad ni miongoni mwa ndugu wa Waisraeli, kwa sababu alikuwa mzao wa Ishmaeli mwana wa Ibrahimu.





 


3.       Mungu Ataweka Maneno Yake katika Mdomo wa Nabii Anayesubiriwa


Kurani inasema kuhusu Muhammad:





"Wala hatamki kwa matamanio. Hayakuwa haya ila ufunuo ulio funuliwa (Kurani 53:3-4)





Hii inafanana sana na fungu la Kumbukumbu la Torati 18:18:





"nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao, mfano wako wewe (Musa), nami nitatia maneno yangu kinywani mwake; naye atawaambia yote nitakayomwamuru." (Kumbukumbu la Torati 18:18)





 Nabii Muhammad alikuja na ujumbe kwa walimwengu wote, na kutoka kwao, Wayahudi. Wote, ikiwa ni pamoja na Wayahudi, wanapaswa kukubali unabii wake, na hii inasadikishwa na maneno yafuatayo:





"MWENYEZI MUNGU, Mungu wenu atawateulieni nabii aliye kama mimi kutoka miongoni mwenu, nanyi mtamsikiliza huyo." (Kumbukumbu la Torati 18:15)





 


4.       Onyo kwa Watakaokataa


Utabiri unaendelea:





Kumbukumbu la Torati 18:19  "Yeyote ambaye hatasikia maneno atakayosema nabii huyo kwa jina langu, mimi mwenyewe nitamwadhibu."





Waislamu, kwa upande mwingine, huanza kila sura katika Kurani kwa jina la Mungu kwa kusema:





Bismillah ir-Rahman ir-Raheem





"‘Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu"





 Yafuatayo ni masimulizi ya baadhi ya wasomi walioamini kuwa utabiri huu unamfaa Muhammad.





Shahidi wa Kwanza





Abdul-Ahad Dawud, ambaye alikuwa Mchungaji zamani, ambapo aliitwa kwa wakati huo David Benjamin Keldani, BD, padri Mkatoliki wa madhehebu ya Umoja wa Wakaldayo (soma wasifu wake hapa).Baada ya kukubali Uislamu, aliandika kitabu kinachoitwa, 'Muhammad katika Biblia. ' Anaandika kuhusu utabiri huu:





“Kama maneno haya hayamuongelei Muhammad, basi bado hayajatimia. Yesu mwenyewe hakudai kamwe kuwa yeye ndiye nabii aliyetajwa. Hata wanafunzi wake walikuwa na maoni sawa: walisubiri ujio wa pili wa Yesu ili utabiri utimie (Matendo ya Mitume 3:17-24). Hadi sasa ni dhahiri kwamba ujio wa kwanza wa Yesu haukuwa ujio wa Nabii huyo na ujio wake wa pili hauwezi kutimiza maneno hayo. Yesu, kama inavyoaminiwa na Kanisa lake, atatokea kama Hakimu wala si kama mtoaji sheria; lakini aliyeahidiwa atakuja na “sheria ya moto” katika mkono wake wa kuume."[4]





Shahidi wa Pili





Muhammad Asad alizaliwa kama Leopold Weiss mwezi Julai 1900 katika mji wa Lvov (Lemberg ya Kijerumani), ambao sasa upo nchini Poland, ambayo ilikuwa chini ya Dola la Austria. Alikuwa mzawa wa ukoo ambao ulikuwa na mstari mrefu wa marabi , mstari uliovunjwa na baba yake, ambaye alichagua kuwa wakili. Asad mwenyewe alipata elimu nyingi ya dini ambayo ingemruhusu kuendeleza mila ya familia ya urabbi. Alikuwa mjuzi katika Kiebrania akiwa mdogo na pia alikuwa akifahamu Kiaramu. Alikuwa amejifunza Agano la Kale  katika mfumo wake asili pamoja na maandishi na maoni ya Talmud, Mishna na Gemara, na alikuwa amejiingiza katika mambo ya undani ya ufafanuzi wa Biblia, Targum.[5]





Akiongelea aya ya Kurani:





"Wala msichanganye kweli na uwongo na mkaificha kweli nanyi mnajua." (Kurani 2:42)





Muhammad Asad anaandika:





“Kwa 'kuichanganya ukweli kwa uwongo '  maana ni kupotosha maandishi ya Biblia, ambayo Qur'ani mara nyingi huwashtaki Wayahudi (na ambayo tangu hapo imethibitishwa kwa upinzani wa kweli wa maandishi), huku 'kuficha ukweli' inahusu kutokujali kwao au kupeana tafsiri ya uongo kwa makusudi kuhusu maneno ya Musa katika kifungu cha Biblia, 'Mungu wenu atawateulieni nabii aliye kama mimi kutoka miongoni mwenu, nanyi mtamsikiliza huyo." (Kumbukumbu la Torati 18:15) na maneno yanayosemekana ni ya Mungu mwenyewe, 'nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao, mfano wako wewe (Musa), nami nitatia maneno yangu kinywani mwake; naye atawaambia yote nitakayomwamuru." (Kumbukumbu la Torati 18:18) “Ndugu” wa wana wa Israeli ni wazi kuwa ni Waarabu, na hasa kundi la Musta'riba ('Walioarabishwa') miongoni mwao, ambalo linaingilia ukoo wa Ishmaeli na Ibrahimu; na kwa kuwa ni kundi hili ambalo kabila la Nabii wa Arabia linatoka, yaani Quraish, vifungu vilivyo juu vya Biblia vinapaswa kuchukuliwa kumaanisha ujio wake."[6]








 



Machapisho ya hivi karibuni

Uislamu Ni dini ya ma ...

Uislamu Ni dini ya maumbile na akili na furaha

UJUMBE KUTOKA KWA MUH ...

UJUMBE KUTOKA KWA MUHUBIRI MUISLAMU KWA MKRISTO

FADHILA YA KUFUNGA SI ...

FADHILA YA KUFUNGA SIKU SITA ZA SHAWAL