Mga Artikulo

Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


Muandaaji


Muhammad Al-shahriy





3


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


Kwa Jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu


Utangulizi


Baada ya hayo


Amewatukuza Mwenyezi Mungu wanadamu na akawafanya kuwa bora zaidi kuliko viumbe wake wengi, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na hakika tumewatukuza wanaadamu} (58),


Ana majina mazuri na sifa za hali ya juu amezithibitisha sifa hizo yeye mwenyewe, na akamthibitishia sifa hizo Mtume wake -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- sifa hizo zimefikia upeo wa ukamilifu na uzuri, hakuna chochote mfano wake naye ni mwenye kusikia na mwenye kuona.


Al- rahmaan: Mwenye huruma ya hali ya juu, na yenye kuenea viumbe vyake vyote.


Al- qadiir" Mwenye uwezo uliokamilika hawi mwenye kushindwa wala kuchoka.


Al- malik: yeye ni mwenye kusifika na sifa ya tukufu na ushindi na upangiliaji wa mambo, mwenye kumiliki mambo yote na kuyaendesha atakavyo.


Al- samiiu: Ambaye ana diriki kuvisikia vyote vyenye kusikika kwa siri na kwa wazi.


Al- salaam: Aliye salimika na kila upungufu ubaya na aibu.


Al- baswiir: ambaye uoni wake umezunguka kila kitu hata kikiwa cha ndani mno na kidogo, mwenye uoni wa vitu, mwenye kuvijua na mwenye kuviona undani wake.


4


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


Al- wakiil: Mwenye kusimamia Riziki za waja wake, na kuwasimamia masilahi yao, na mwenye kuwapenda vipenzi vyake na akawafanyia wepesi na akawatosheleza mambo mbalimbali.


Al- khaaliq: Mletaji wa vitu na mgunduzi wake kwa namna ambayo hakuna mfano wake kabla yake.


Al- latwiif: Ambaye anawakirimu waja wake na kuwarehemu na kuwapa wanachomuomba.


Al- kaafi: Ambaye huwatosheleza waja wake mambo yote wanayoyahitajia kwake.


Al- ghafuur: Ambaye anawakinga waja wake na shari ya madhambi yao, na wala hawaadhibu kwa madhambi hayo.


Anafikiria muislamu maajabu ya muumba na uwepesi wake, na miongoni mwa ajabu ni kutilia umuhimu viumbe kwa udogo wake, kwa kupupia kuwalisha na kuwachunga mpaka waweze kujitegemea wenyewe, basi kutakasika kwa machafu ni kwake yeye muumba wa viumbe na mwenye kuvihurumia, na katika kuvionea huruma viumbe, ameviandalia vitu vyenye kuvisaidia na vyenye kutengeneza hali zake licha yakuwa viumbe hivyo vina madhaifu makubwa.


Mtume wangu Muhammad - Rehema na amani za Allah ziwe juu yake-


Muhammad - Rehema na amani za Allah ziwe juu yake- ni Rehema iliyotolewa zawadi.


Naye ni Muhammad mtoto wa Abdillah -Rehema na amani za Allah ziwe juu yake- mwisho wa manabii na mitume, alimtuma Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa dini ya uislamu kwa watu wote, ili awajulishe mambo ya kheri na mambo makubwa katika hiyo kheri ni


5


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


Tauhiid, na anawakataza mambo ya shari na jambo kubwa la shari ni ushirikina.


Ujumbe wake na ujumbe wa manabii wote waliokuwa kabla yake ni kulingania katika kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake hana mshirika wake.


Qur'ani tukufu ni maneno ya Mola wangu


Qur'ani tukufu ni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ambayo ameyateremsha kwa Mtume wake Muhammad- Rehema na amani za Allah ziwe juu yake- ili awatoe watu kutoka katika giza kuwapeleka katika nuru na kuwaongoza katika njia iliyonyooka.


Yeyote atakayeisoma atapata malipo makubwa, na atakayeufanyia kazi muongozo wake basi atakuwa amefuata njia iliyo sawa.


Najifunza nguzo za uislamu.


Amesema Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake: "Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: (Uislamu umejengwa juu ya mambo matano: Ni kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila ni Mungu mmoja na kwamba Muhammad ni mtume wa Mwenyezi Mungu na kusimamisha swala na kutoa zaka na kufunga Ramadhan na kuhiji katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu".


1- Ni kushuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake na Muhammad ni mtume wa Mwenyezi Mungu.


6


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


Amesema Allah Mtukufu:





"Basi tambua ya kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu" [Surat muhammad 19]


Maana ya kushuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu: yaani hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu.


Kusimamisha swala kunakuwa kwa kutekeleza kwa namna ambayo ameelekeza Mwenyezi Mungu Mtukufu na akatufundisha Mtume wake-Rehema na amani za Allah ziwe juu yake-.


Nguzo ya tatu: Kutoa zakah.


Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:





(Na toeni zaka) [Al-baqara 110].


Nayo ni haki ya wajibu katika mali itakapokuwa imefikia kiwango maalumu, hupewa aina nane alizozitaja Mwenyezi Mungu katika Qur'ani tukufu, miongoni mwao ni mafukara na masikini.


Na katika kuitekeleza kwake kuna kusifika kwa sifa ya huruma na upole, na kusafisha tabia za muislamu na mali yake, na kuziridhisha nafsi za mafukara na masikini na kuyapa nguvu mafungamano ya kimapenzi na udugu kati ya mtu mmoja mmoja katika jamii ya kiislamu, na kwa hivyo muislamu mwema huitoa zaka kwa moyo safi na kufurahia utekelezaji wake, kwa sababu kutoa zaka kunafurahisha watu wengine.


7


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


Na kiwango cha zaka ya mali ni 2.5% katika mali iliyolimbikizwa miongoni mwazo ni Dhahabu na fedha, na pesa tasilim na bidhaa za biashara zilizo andaliwa kwa ajili ya kuuza na kununua ili kupata faida; zinapofikia thamani yake kiwango maalumu na zikazungukiwa na mwaka mzima.


Kama ambavyo ni wajibu kutoa zaka kwa mwenye kumiliki idadi maalumu ya wanyama wafugwao (Ngamia, Ngo'mbe, na mbuzi) ikiwa wanakula majani ya malishoni mwaka mzima pasina kulishwa na mwenye wanyama.


Na hivyo hivyo ni wajibu kutoa zaka kwa kinachotoka katika ardhi miongoni mwa nafaka na matunda, madini na hazina ikiwa zitafikia kiwango maalumu.


Nguzo ya Nne: kufunga Ramadhani:


Amesema Allah Mtukufu:





{Enyi mlioamini Mmefaradhishiwa kufunga, kama Walivyofaradhishiwa wale waliokuwa kabla yenu, ili mpate kumcha Mwenyezi Mungu}. [Al-baqara 110].


Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wa tisa katika mwaka wa mpangilio wa Hijria (kuanzia kuhama mtume) nao ni mwezi mtukufu kwa waislamu, na una nafasi yake maalumu kuliko miezi mingine katika mwaka, na kuufunga mwezi huo ni moja ya nguzo tano za uislamu.


Kufunga mwezi wa ramadhani: ni kumuabudu Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kujizuia na kula na kunywa na kufanya tendo la ndoa,


8


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


na vyote vyenye kufunguza, kwanzia kuchomoza jua mpaka kuzama jua katika siku zote za mwezi wa ramadhani wenye baraka.


Nguzo ya tano Kuhiji nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu.


Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:





"Na Mwenyezi Mungu amewawajibishia watu wafanye hijja katika nyumba hiyo tukufu kwa mwenye kuweza kufunga safari ya kwenda huko ". [Al-Imran: 97].


Hijja inakuwa kwa mwenye uwezo wa kufunga safari kwenda huko mara moja katika umri wake, nako ni kukusudia nyumba tukufu na viwanja vitukufu vya Makkah kwa ajili ya kutekeleza ibada maalumu katika wakati maalumu, na hakika alifanya hijja Mtume -Rehema na amani za Allah ziwe juu yake- na pia mitume wengine walifanya hijja kabla yake, na akamuamrisha Mwenyezi Mungu ibrahim -Amani iwe juu yake- awaite watu kuja kutekeleza ibada ya hijja kama alivyolieleza hilo Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur'an tukufu akasema:


"Na tukamwambia utangaze kwa watu habari za hijja watakujia wengine kwa miguu na wengine juu ya kila mnyama aliyekonda kwa uchovu wa safari watakujia kutoka kila njia ya mbali " [Al Haji: 27].


Najifunza nguzo za imani:


Na kutenda kwa viungo vya nje: kama vile swala na kuhijji, na kufunga n.k. na viungo vya ndani vyenye kuhusiana na moyo kama kumpenda Mwenyezi Mungu na kunyenyekea, na kutegemea kwake na kumtakasia ibada yeye.


9


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


Na wanaielezea wabobezi kwa ufupi kuwa Imani ni kuitakidi moyoni, na kutamka kwa ulimi na kutenda kwa viungo, nayo inazidi kwa kutii na hupungua kwa maasi.


Kumuamini Mwenyezi Mungu kunapelekea kupwekesha katika uumbaji wake na uungu wake na majina yake na sifa zake, na kunajumuisha mambo yafuatayo:


Kuamini uwepo wake kutakasika na machafu ni kwake na mtukufu.


Kuamini uumba wake kutakasika na machafu ni kwake na mtukufu, na kuwa yeye ni mmiliki wa kila kitu, na muumba wake na mwenye kuruzuku na mwendeshaji wa mambo yake.


Kuamini Uungu wake -kutakasika ni kwake- na kuwa yeye ndiye anayestahiki kuabudiwa peke yake hana mshirika wake kwa chochote, ibada hizo ni: kama vile swala, na dua, na kuweka nadhiri, na kutaka msaada, na ibada zingine zote.


Kuamini majina yake mazuri na sifa zake za hali ya juu ambazo amezithibitisha yeye mwenyewe au mtume wake Muhammad- Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- na akapinga sifa alizozipinga katika nafsi yake au kazipinga Mtume- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- miongoni mwa majina na sifa, na kuwa majina yake na sifa zake zimefika ukomo wa ukamilifu na uzuri, na kuwa yeye hakuna chenye kufanana naye naye ni mwenye kusikia na kuona.


Nguzo ya pili: Kuwaamini Malaika:


Na hao Malaika ni viumbe wakubwa hakuna awezaye kudhibiti nguvu zao na idadi yao isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kila mmoja katika wao ana sifa na majina na kazi zao ambazo


10


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


amezifanya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa maalumu kwao tu, na miongoni mwao ni Jibrili- Amani iwe juu yake- aliyewakilishwa kwa ajili ya wahyi anateremka nao kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwenda kwa mitume wake.


Nguzo ya tatu: Kuamini vitabu:


Na vitabu vya mbinguni ambavyo amevitaja Mwenyezi Mungu katika kitabu chake ni:


Qur'ani tukufu: Aliiteremsha Mwenyezi Mungu kwa mtume wake Muhammad - Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-


Zabuur: Aliiteremsha Mwenyezi Mungu kwa mtume wake Daudi- Rehema na amani ziwe juu yake


Nguzo ya Nne : Kuwaamini mitume.


Ni kusadikisha kusikokuwa na shaka kwamba Mwenyezi Mungu ametuma katika kila umma mtume, anawalingania watu kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake hana mshirika wake, na kupinga kila kinachoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu Mtukufu.


Na kuwa mitume wote hao ni wanadamu wanaume na ni waja wa Mwenyezi Mungu, nakuwa wao ni wakweli na wenye kukubaliwa, ni wacha Mungu na ni waaminifu, ni waongofu walioongoka, na akawatia nguvu Mwenyezi Mungu kwa miujiza yenye kujulisha ukweli wao, na hakika wao walifikisha yote aliyowatuma Mwenyezi Mungu, na kuwa wao wote walikuwa kwenye haki na muongozo uliokuwa wazi.


Na kwa hakika ulinganiaji wao ulikuwa mmoja kwanzia wa mwanzo wao mpaka wa mwisho wao katika msingi wa dini, nao ni


11


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


kumpwekesha Mwenyezi Mungu- aliyetakasika na Kutukuka- katika kumuabudu na kutokumshirikisha.


Nguzo ya Tano: Kuamini siku ya mwisho.


Amesema Allah Mtukufu:


اللََُّّ لََ إِلَهَ إِلََّ هُوَ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلََ ي وَْمِ الْقِيَامَةِ لََ رَيْبَ فِيهِ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللََِّّ حَدِ يثًا


"Mwenyezi Mungu, Ambaye hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila yeye, Ndiye Atakaye wakusanya nyinyi Siku ya Kiyama isiyokuwa na shaka, kwa kuhesabiwa na kulipwa. Na hakuna yeyote mkweli zaidi wa maneno anayoyatolea habari kuliko Mwenyezi Mungu". [Al-nisaa 87].


Ni kusadikisha kusikokuwa na shaka kila kinachohusiana na siku ya mwisho miongoni mwa yale aliyoyaeleza Mola wetu mtukufu katika kitabu chake kitukufu au aliyotusimulia Mtume Muhammad -Rehema na Amani ziwe juu yake- kama kufa mwanadamu, na kufufuliwa kukusanywa, na uombezi, na mizani, na hesabu, pepo, na moto, na mengine yasiyokuwa hayo yenye kuhusiana na siku ya mwisho.


Nguzo ya sita: Kuamini Qadar kheri zake na shari zake.


Amesema Allah Mtukufu:


إِنََّّ كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَر


"Hakika sisi kila kitu tumekiumba kwa kipimo chake mahsusi". [Al- qamar 49].


12


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


Kuamini kuwa kila jambo linalotokea kwa viumbe miongoni mwa matukio ya duniani, basi hutokea kwa kujua Mwenyezi Mungu, na amelikadiria- kutakasika na machafu ni kwake- na upangiliaji wake yeye peke yake hana mshirika wake, nakuwa haya makadirio yameandikwa kabla ya kuumbwa mwanadamu, na hakika mwanadamu anamatashi, na yeye ndiye mfanyaji wa vitendo vyake kiuhakika, lakini vyote hivyo havitoki nje ya ujuzi wa Mwenyezi Mungu matashi yake na kupenda kwake.


Na Kuamini Qadari kunakuwa katika ngazi Nne nazo ni:


Ngazi ya pili: Kuamini aliyoyaandika Mwenyezi Mungu kwa kila lililopo mpaka kusimama kiyama.


Ngazi ya tatu: Kuamini matashi ya Mwenyezi Mungu yenye kutekelezwa na uwezo wake uliotimia, basi lolote alitakalo huwa na asilolitaka haliwi.


Ngazi ya Nne: Kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ni muumba wa kila kitu, hana mshirika wake katika kuumba kwake.


Ninajifunza Kutawadha (Udhu)


Na Amesema Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- (Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu, hutoka madhambi yake mwilini mwake).


Basi huenda mja kwa Mola wake hali yakuwa ni mwenye kujisafisha usafi wa kihisia (unaoonekana) kwa kutawadha, na usafi wa kimaana (usioonekana, kama usafi wa moyo) kwa kutekeleza ibada hizi, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kufuata muongozo wa Mtume -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-.


Yanayopaswa kufanywa ukiwa na Udhu:


13


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


1- Swala ya aina yoyote sawa iwe ya Faradhi au iwe ya Sunnah.


2- Kutufu Al-qaaba (nyumba tukufu)


Nina tawadha na Ninaoga kwa kutumia maji safi.


Maji safi ni kila maji yaliyoteremka toka mbinguni, au yakachimbuka kutoka ardhini na yakabakia katika asili ya umbile lake, na hayakubadilika moja kati ya sifa zake tatu, nazo ni, Rangi, Ladha, na Harufu, hayakubadilika kwa kitu chenye kuondosha usafi wa maji.


Hatua ya kwanza: (1) Kutia nia na mahala pake ni moyoni, na maana ya nia: ni kuazimia moyoni kufanya ibada kwa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.


Hatua ya pili: (2) kuosha viganja viwili:


Hatua ya tatu (3) kusukutua.


Kusukutua ni Kuingiza maji mdomoni na kuyazungusha humo, kisha kuyatoa.


Hatua ya Nne: Kupandisha maji puani:


Kupandisha maji puani: ni kuyavuta maji kwa pumzi mpaka kwenye kilele cha pua.


Kisha kuyatoa: nako ni kutoa kila kilichoko ndani ya pua miongoni mwa kamasi na vinginevyo kwa kuvuta pumzi.


14


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


Mipaka ya uso:


Na weupe ni ule uliopo kati ya nywele na nyama ya sikio.


Na nywele ambazo ziko juu ya mfupa uliotokeza, unaoelekeana na tundu la sikio lenye kupita mpaka ndani ya kichwa na kutumbukia mpaka kigingi cha sikio.


Na vile vile kunakusanya kuosha uso kila kilichoko wazi kuanzia nywele nyingi za ndevu na zilizo shuka katika ndevu.


Hatua ya sita: Kuosha mikono miwili kwa kuanzia ncha za vidole vya mikono miwili mpaka kwenye fundo mbili.


Na huingia kwenye fundo mbili kuosha mikono miwili iliyofaradhishwa.


Hatua ya saba: Kukipaka maji kichwa kizima pamoja na masikio mawili mara moja .


Ataanza mwanzo wa kichwa chake akienda na mikono yote mpaka kichogoni kisha atairudisha mpaka sehemu aliyoanzia.


Na ataingiza vidole vyake viwili ndani ya masikio yake.


Na akifuatishia kwa vidole gumba juu ya mgongo wa masikio yake, na atapaka hivyo nje ya masikio yake na ndani.


Hatua ya Nane: Kuosha miguu miwili kuanzia vidole vya miguu miwili mpaka kwenye kongo mbili, na huingia kwenye kongo mbili kuosha miguu miwili iliyofaradhishwa.


Kongo mbili ni: mifupa miwili iliyoota chini ya miundi.


Na udhu huharibika kwa mambo haya yafuatayo:


15


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


1- kutoka kitu katika moja ya njia mbili kama mkojo, na haja kubwa, na upepo, na manii, na madhii.


2- Kuondokwa na akili kwa kulala usingizi au kuzimia, au kulewa, au kupatwa na wenda wazimu.


3- kila chenye kulazimisha kuoga kama janaba, na Hedhi, na Nifasi.


Na akikidhi mwanadamu haja yake anapaswa kuondosha najisi, ima kwa maji safi, na hii ndiyo njia bora zaidi, au pasina kutumia maji safi kwa vitu vinavyoondosha najisi kama mawe na karatasi na vitambaa na mfano wake. na kwa sharti iwe kuondoa huko ni kwa kufuta mara tatu au zaidi kwa kitu chenye kutakasa na kilicho safi na halali kukitumia.


Kufuta juu ya Khofu mbili au soksi mbili


Katika hali ya kuvaa khofu mbili au soksi mbili, basi yawezekana kufuta juu yake pasina kuwa na haja ya kuosha miguu miwili, kwa masharti ambayo ni:


1- Ziwe zimevaliwa baada ya twahara iliyokamilika iliyosababishwa ima na hadathi ndogo au kubwa ambapo ilioshwa katika twahara hiyo miguu miwili.


2- Ziwe khofu au soksi mbili ni twahara na si zenye najisi.


Na iwe upakaji ni katika muda uliowekwa kwa ajili hiyo.


4- Na khofu hizo au soksi ziwe ni halali, zisiwe kwa mfano ni za wizi au za kupora.


Khofu mbili: ni zile zenye kuvaliwa katika mguu, na hutokana na ngozi nyembamba na mfano wake, na mfano wa khofu ni viatu vinavyositiri miguu miwili.


16


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


Soksi mbili ni: ni zile ambazo huzivaa mtu mguuni mwake zinazotokana na kitambaa na mfano wake na ndiyo zinazojulikana kwa jina la (Shurraab).


Hekima ya kuweka sheria ya kufuta juu ya khofu mbili:


Hekima ya kuweka sheria ya kufuta juu ya khofu mbili: nikufanya wepesi kwa waislamu, ambao inakuwa kwao ni taabu kuvua khofu na soksi na kuosha hasa miguu miwili katika wakati wa masika na baridi kali na safarini.


Muda wa kupaka:


Mkaazi: (asiye kuwa msafiri) atapaka usiku na mchana (masaa 24)


Na Msafiri: atafuta siku tatu na usiku wake (masaa 72)


Ataanza kuhesabu muda wa kufuta kuanzia mwanzo wa kufuta khofu mbili au soksi mbili baada ya kupatwa na hadathi.


Sifa za ufutaji juu ya khofu mbili au soksi mbili:


1- Hulowanishwa mikono miwili:


2- Hupitishwa mkono juu ya unyayo kuanzia kwenye vidole mpaka mwanzo wa muundi


3- Hupakwa unyayo wa kulia kwa kutumia mkono wa kulia na unyayo wa kushoto kwa mkono wa kushoto.


Venye kuharibu ufutaji:


1- Vyote vyenye kuwajibisha kuoga:


2- Kuisha muda wa kupaka:


17


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


Kuoga :


Ikitokea kwa mwanaume au mwanamke kitendo cha kujamiiana, au wote wawili yakawatoka manii kwa kutamani wakiwa katika hali ya kulala au kuamka, ni wajibu juu yao kujitwaharisha, na vile vile mwanamke akitwaharika kutoka kwenye Hedhi na nifasi ni wajibu kwake kuoga kabla ya kuanza kutekeleza swala au kufanya mambo ambayo yanalazimu twahara.


Na sifa ya kuoga ni kama ifutavyo:


Na aueneze muislamu mwili wake wote kwa maji kwa njia yoyote ile, na katika hayo ni kusukutua, na kupandisha maji puani, na ikiwa ataeneza mwili wake kwa maji, itaondoka kwake hadathi kubwa, na itakuwa imetimia twahara yake.


Hutahadharishwa mwenye janaba kufanya mambo yafutayo mpaka aoge:


01- Kuswali:


02- Kutufu Al-qaaba (nyumba tukufu)


03- Kukaa msikitini na yafaa kwake kupita tu pasina kukaa.


04- Kushika msahafu


05- Kusoma Qur'ani


Kutayammam


Ikiwa hajapata muislamu maji ambayo atajitwaharishia au hakuweza kuyatumia maji kutokana na maradhi na mfano wake na akahofia usimpite wakati wa swala basi atatayamamu kwa kutumia udongo.


18


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


Na sifa zake ni apige pigo moja kwa mikono yake miwili kisha apake kwa mikono hiyo uso wake na viganja vyake tu, na ni sharti udongo uwe twahara.


Na Tayamamu huharibika kwa mambo yafuatayo:


1- Huharibika Tayamamu kwa kila chenye kuharibu Udhu.


2- Yakipatikana maji kabla ya kuanza ibada ambayo ametayamamu kwa ajili yake


Amemfaradhishia Mwenyezi Mungu Muislamu kusali swala tano usiku na mchana nazo ni: Al-fajiri, na Adhuhuri, na Alaasiri, na Magharibi, na Ishaa.


Najiandaa kwa ajili ya swala


Ukiingia muda wa swala hujitwaharisha muislamu kutokana na hadathi (Uchafu) ndogo na kubwa, ikiwa amepatwa na hadathi kubwa.


Na hadathi kubwa ni: kila kinachomlazimisha muislamu kuoga.


Na hadathi kubwa ni: kila kinachomlazimisha muislamu kutawadha.


Husali muislamu akiwa katika twahara na katika sehemu safi kutokana na Najisi, akiwa ameusitiri uchi wake.


Anajipamba muislamu kwa mavazi yanayofaa wakati wa swala na husitiri kwa mavazi hayo mwili wake, na haifai kwa mwanaume wakati wa kuswali aache wazi sehemu yoyote kuanzia sehemu ya kitovuni mpaka magotini.


Ni wajibu kwa mwanamke kuusitiri mwili wake wote ndani ya swala isipokuwa uso na viganja viwili.


19


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


Hazungumzi muislamu akiwa katika swala maneno yasiyokuwa maalumu kwa ajili ya swala, na kumsikiliza imamu, na wala asigeuke geuke katika swala yake, na ikiwa atashindwa kuyahifadhi maneno maalumu kwa ajili ya swala, basi atamtaja mola wake na kumsabbihi mpaka amalize swala.


Ninajifunza Swala:


Hatua ya kwanza 1: Kutia nia kwa ajili ya faradhi ninayotaka kuitekeleza, na mahala pake ni moyoni.


Baada ya kutawadha naelekea Qibla, na ninaswali nikiwa nimesimama ikiwa naweza kufanya hivyo.


Hatua ya pili 2: Nina inua mikono yangu miwili usawa wa mabega mawili na ninasema (Allahu Ak-baru) huku nikinuia kuingia katika swala


Ninasoma baada ya suratil faatiha kilicho chepesi kwenye Qur'ani katika rakaa ya kwanza na ya pili tu katika kila swala, na kusoma huku siyo lazima lakini kufanya hilo kuna malipo makubwa.


Hatua ya 6; Ninasema (Allahu akbaru) Mwenyezi Mungu ni mkubwa-kisha nina rukuu mpaka unakuwa mgongo wangu umelingana sawa na mikono yangu miwili inakuwa juu ya magoti mawili hali ya kutawanya vidole, kisha ninasema katika kurukuu (Ametakasika Mola wangu Mtukufu).


Hatua ya 7: Ninainuka kutoka kwenye kurukuu kwa kusema (Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumuhimidi)


Hatua ya Nane 8: Ninasema (Mwenyezi Mungu ni mkubwa)


Hatua ya tisa 9: Ninasema: Allahu akbaru (Mwenyezi Mungu ni mkubwa na ninainuka kutoka kwenye kurukuu mpaka ninalingana


20


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


sawa) hali ya kunyoosha mgongo huku nikikalia mguu wa kushoto na nikiusimamisha mguu wa kulia, na ninasema (Rabbihg-firly)- ewe Mola wangu nisamehe.


Hatua ya kumi 10: Ninasema (Allahu akbaru) Mwenyezi Mungu ni mkubwa -na ninasujudu mara nyingine tena mfano wa sijda ya kwanza.


Hatua ya kumi na moja 11: Nina inuka kutoka katika sujudu na ninasema: (Allahu Ak-baru) mpaka niwe sawa nikiwa nimesimama, na ninafanya hivyo katika rakaa zilizobakia kama nilivyofanya katika rakaa ya kwanza.


Hatua ya kumi na mbili 12. Kisha baada yake nitageuka upande wa kulia na kusema "Assalaam alaikum warahmatullahi" kisha nageuka upande wangu wa kushoto nakusema Assalamu alaikum warahmatullahi" na kwa kufanya hivyo ninakuwa nimekamilisha sala.


Stara ya mwanamke wa kiislamu:


Na huchunga mwanamke wa kiislamu katika mavazi yake mipaka:


Kwanza: Vazi kuenea mwili mzima.


Pili: Lisiwe vazi analolivaa mwanamke ni kwa ajili ya kujipamba.


Tatu: Na lisiwe jepesi linaloonyesha mwili wake


Nne: Liwe pana na siyo finyu likasifu sehemu ya mwili wake


Katika sifa za waumini:


Ni mkweli katika mazungumzo yake wala hasemi uongo.


Anatekeleza ahadi na miadi.


21


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


Hatendi uovu katika ugomvi.


Anatekeleza amana.


Anampendelea ndugu yake muislamu anayoyapenda katika nafsi yake.


Ni mkarimu.


Anaridhika na alichokipanga Mwenyezi Mungu na anamshukuru katika hali ya raha na husubiri katika hali ya matatizo.


22


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


Anasifika nakuwa na haya.


Moyo wake umesalimika na vinyongo na mwili wake umesalimika na kuwashambulia watu wengine.


Anawasamehe watu.


Hali Riba wala hafanyi miamala ya riba.


Hafanyi zinaa.


Hanywi pombe.


Anawatendea wema majirani zake.


Hadhulumu wala kufanya hiyana.


Haibi walala hafanyi hila za kuiba.


Ni mwenye kuwatendea wema wazazi wawili, hata kama siyo waislamu, na huwatii kwenye mambo mema.


Na huwalea watoto wake kwa tabia njema, na anawaamrisha kutekeleza wajibu wa sheria, na anawakataza kufanya mambo machafu na ya haramu.


Hajifananishi kwa matendo yasiyokuwa ya waislamu katika mambo yao maalumu ya kidini au Ada zao ambazo zimekuwa alama na nembo yao.


Na kwa hakika ametuweka Mwenyezi Mungu katika ulimwengu huu kwa hekima kubwa na wala hakutuumba kimchezo mchezo; na lengo ni kumuabudu yeye peke yake hana mshirika wake, na akatuwekea dini ya kimalezi iliyotimia na kuenea, hupangilia mambo yetu yote maalumu na yasiyokuwa maalumu, na imehifadhi sheria hii yenye uadilifu mambo ya dharura katika maisha, na mambo hayo


23


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya


ni: kuhifadhi Dini yetu, na nafsi, na heshima, na akili, na mali, na mwenye kuishi kwa kufuata maamrisho ya sheria na akawa ni mwenye kujiepusha na mambo ya haramu kwa hakika mtu huyo atakuwa kahifadhi dharura hizi, na ataishi kwa furaha na mwenye matumaini katika maisha yake bila shaka.


Na mahusiano haya makubwa ni hali ya hisia zinazobebwa na kuneemeka kwa kumuabudu mwingi wa rehema, na kuwa na shauku ya kukutana naye na kuuchochea moyo wake kupaa katika anga ya furaha kwa kuhisi kwake utamu wa imani.


Ndiyo ikiwa atahisi mwanadamu kila wakati yuko mbele ya muumba wake, na akamjua kwa majina yake na sifa zake zilizo nzuri, na akamuabudu kama vile anamuona, na akatakasa ibada yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na wala hakukusudia katika Ibada hiyo isipokuwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu -kutakasika ni kwake-, ataishi maisha mazuri yenye furaha katika dunia na mwisho mzuri huko akhera.


Hata matatizo ambayo yanamtokea muumini katika dunia, kwa hakika joto lake huondoka kwa baridi ya yakini, na kuridhia Qadari ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumshukuru yeye kwa Qadari zake kheri zake na shari zake na kuridhika kwa hayo yote kwa ukamilifu.


Na rehema na amani za Allah ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad na ali zake na Maswahaba zake.


Yaliyomo


Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya .......................... 1


Utangulizi ....................................................................................... 3


Qur'ani tukufu ni maneno ya Mola wangu .................................... 5


Nguzo ya tatu: Kutoa zakah. .......................................................... 6


Nguzo ya Nne: kufunga Ramadhani: .............................................. 7


Nguzo ya Tano: Kuamini siku ya mwisho. .................................... 11


Mipaka ya uso: ............................................................................. 14


Kuoga :.......................................................................................... 17


Anasifika nakuwa na haya. ........................................................... 22


Yaliyomo ....................................................................................... 24



Kamakailang Mga Post

BIYAYA NG PAG-AAYUNO ...

BIYAYA NG PAG-AAYUNO NG ANIM NA ARAW NG SHAWAL

KINIKILALA NG MGA KRI ...

KINIKILALA NG MGA KRISTIYANONG ISKOLAR ANG MGA PAGKAKASALUNGAT SA BIBLIYA

Muhutasari wenye faid ...

Muhutasari wenye faida kwa muislamu mpya